Rafiki yangu mpendwa,

Kwenye makala iliyopita nilikushirikisha nguvu tatu muhimu unazopaswa kuwa nazo ili uweze kupata chochote kile unachotaka kwenye maisha yako.

Pia nilikupa nafasi nzuri kwako kuweza kuzipata na kuzitumia nguvu hizo ili mwaka huu 2020 uwe wa kipekee sana kwako.

Kwenye makala ya leo nakwenda kukupa ushuhuda wa mwenzetu ambaye nguvu mbili kati ya zile tatu zimemwezesha kufanya makubwa.

Huyu nguvu moja tayari alikuwa nayo, lakini haikuweza kufanya kazi peke yake, ila alipopata nguvu nyingine mbili, mambo yakawa bora sana.

Nice-Thoughts-Of-Success.jpg

Kwanza kabisa napenda Kumshukuru Mungu kwa kunikutanisha na Kocha Amani kupitia rafiki yangu Victor. Nimejifunza mengi kupitia KISIMA CHA MAARIFA na AMKA MTANZANIA, huko ndio kumenipa hamasa ya kutambua umuhimu wa kuwa na MENTOR katika safari ya mafanikio.

  • Programu hii imenifanya kujisukuma zaidi na kutojionea huruma ambapo;
  • Nimeweza kukuza biashara yangu ya mtando iliyokuwa inasuasua, kiukweli nimepiga hatua kubwa tofauti na awali.
  • Kwa muda wa mwezi mmoja nimeweza kuongea na Watu zaidi ya 70 na kuwashirikisha biashara ninayoifanya.
  • Nimeweza kuunga mtu 1 kwa biashara na wa 4 watajiunga mwezi huu, kwangu ni ushindi mkubwa sana.
  • Nimeweza kuifanya page yangu ya Instagram kuwa page ya biashara na kupata followers wapya kila siku.
  • Kupitia programu hii nimeweza kuanza ufugaji wa kuku ambao nilikuwa naghairi kila mara kuanza.
  • Nimekuwa na nidhamu binafsi katika mambo yangu.
  • No plan B nitayaendeleza haya ili kufikia uhuru wangu ninaoutaka. Asante sana Kocha

Symphorose James

Symphorose James ni mmoja wa watu wanne walioshiriki programu ya GAME CHANGERS kwa msimu wa mwezi Januari 2020. Katika programu hii, Symphorose alikuwa na majukumu makuu mawili, kukuza biashara yake ya mtandao kwa kuwafikia watu wengi na kuwaunganisha pamoja na kuuza bidhaa zaidi. Lakini pia wakati programu inaendelea, kwa hamasa aliyoipata kutoka kwa mshiriki mwingine, alianza ufugaji wa kuku ambacho ni kitu alikuwa akikiahirisha kwa muda mrefu.

Kwa mpango bora kabisa ambayo tuliuweka pamoja, pamoja na mwongozo wa Kocha na msukumo wa washiriki wengine kwenye programu hii, Symphorose aliweza kutekeleza vizuri mipango hiyo.

Pamoja na kuwa kwenye biashara hiyo ya mtandao kwa zaidi ya mwaka mmoja, hakuwa amewafikia watu wengi na hakuna hata mmoja aliyekuwa amejiunga. Lakini kwa siku 30 ameweza kuwafikia watu 70, mmoja kujiunga ndani ya siku hizo na wengine kuahidi kujiunga karibuni.

Je wewe hutaki kupata matokeo bora na makubwa kama ya rafiki yetu Symphorose? Kama jibu ni ndiyo, karibu upate nguvu mbili unazokosa sasa.

NGUVU MBILI UNAZOKOSA ILI UFANIKIWE.

Rafiki, tuliona nguvu tatu unazohitaji ni SHAUKU, MWONGOZO na JUMUIA.

Shauku wengi wanayo, ndiyo maana huwa wanapanga malengo na mipango mbalimbali, na hata kufikia hatua ya kuanza kutekeleza. Lakini wengi hawafiki mbali.

Mwongozo wa kocha ndiyo kikubwa ambacho watu wanakosa, badala ya kufanya kitu kwa uhakika, wanajaribu, wakikutana na ugumu wanaishia hapo. Kocha anakuwezesha kujisukuma zaidi mpaka upate ulichotaka, licha ya kupitia magumu.

Jumuia ni kitu kingine muhimu unachokosa, hujazungukwa na wale ambao wanapiga hatua kubwa kama unazotaka kupiga. Umezungukwa na watu wanaokuambia usijitese, huwezi na maneno mengine ya kukatisha tamaa. Ukiweza kuzungukwa na wanaofanya makubwa, na wewe utafanya makubwa pia.

Rafiki, kama nilivyokueleza kwenye makala iliyopita, njia pekee ya wewe kuweza kupata nguvu hizi na kufanya makubwa ni kushiriki kwenye programu ya GAME CHANGERS.

Kwa sasa tunaelekea kuanza msimu wa MACHI 2020, ambapo una nafasi ya kwenda kufanya makubwa sana kwa mwaka huu 2020.

Napenda kukufahamisha kwamba leo ndiyo siku ya mwisho ya kupata nafasi ya kushiriki programu ya GAME CHANGER MACHI 2020.

Kama umekuwa unafuatilia taarifa ambazo nimekuwa nakupa kuhusu GAME CHANGERS na roho yako inakuambia hiki ndiyo unachohitaji kwa hapo ulipo sasa, isikilize roho yako. Inajua umekwama na kujikwamisha kiasi gani, na sasa imeona fursa ya wewe kutoka hapo ulipokwama sasa.

Usiendelee kufikiria zaidi, usiendelee kusubiri tena, bali tuma ujumbe sasa wenye maneno NITASHIRIKI GAME CHANGERS MACHI 2020 kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 ili usiikose nafasi hii.

Nafasi ya kipekee kwako ndiyo hii rafiki, karibu leo twende pamoja kufanya makubwa mwaka huu 2020.

UTARATIBU WA GAME CHANGERS.

GAME CHANGERS ni programu maalumu ya ukocha ambayo inaendeshwa na Kocha Dr Makirita Amani ambayo inawalenga wale wanaotaka kuleta mabadiliko makubwa kwenye maisha yao na kwa muda mrefu.

Programu hii inakupa manufaa mawili kwa wakati mmoja, ambayo ni COACHING (ambapo unapata mwongozo wa kocha) na MASTER MIND (ambapo unapata msukumo wa wengine wanaofanya makubwa kama wewe). Hizi ni nguvu mbili ambazo zinakuwezesha kufanya makubwa sana zikitumika pamoja.

Kwa kuingia kwenye programu hii ya GAME CHANGERS, utapata nafasi ya kufanya kazi moja kwa moja na Kocha Dr Makirita pamoja na watu wengine wanne ili kutoka pale ulipokwama sasa na kupiga hatua kubwa.

Utapata nafasi ya kujadili ulipokwama kwa kina na Kocha, na kisha kwa pamoja mtaweka mkakati utakaofanyia kazi kwa siku 30.

Utawekwa kwenye kundi maalumu la wasap la programu hii ambapo huko utakuwa pamoja na wengine wanaofanyia kazi mabadiliko kwenye maisha yao. Ndani ya kundi hili kila siku kunakuwa na mijadala ya hatua ambazo kila mtu anapiga kwenye mipango aliyojiwekea kwa wiki husika.

Kila siku ya jumamosi, kuanzia saa 11 jioni kutakuwa na simu ya pamoja ya watu wote watano waliopo kwenye programu hii pamoja na kocha kwa ajili ya kupitia hatua ambazo kila mtu amepiga kwa juma zima. Katika simu hii ya pamoja, kila mtu anapata nafasi ya kumshauri mwenzake katika hatua anazochukua na changamoto anazokutana nazo.

Kila siku kwa siku 30 utapata somo moja la misingi ya GAME CHANGERS ambalo litakupa maarifa ya kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako. Kwenye kila somo na kila msingi, kutakuwa na mafunzo au kitabu cha rejea ambapo utaweza kujifunza kwa kina zaidi.

Kwa siku zote 30 za programu hii, una uhuru wa kuwasiliana na kocha katika muda wowote, kuuliza chochote na kupatiwa majibu au ushauri wa kitu sahihi kufanya kwa pale ulipokwama.

Unaweza kushiriki programu hii ukiwa sehemu yoyote nchini Tanzania, na ambapo una mtandao wa simu na mtandao wa intaneti.

NAFASI ZA KUSHIRIKI GAME CHANGERS MACHI 2020.

Rafiki, kama nilivyokushirikisha kwenye utangulizi, programu hii ya GAME CHANGERS huwa inaendeshwa kwa misimu, na msimu mmoja unachukua siku 30 ambazo ni mwezi mmoja.

Tunakwenda kuanza msimu mwingine wa programu hii ya GAME CHANGERS mwezi Machi 2020, kuna nafasi tano pekee za kushiriki programu hii kwa msimu huo wa mwezi Machi. Hivyo karibu sana uchukue hatua sasa.

HATUA ZA KUCHUKUA ILI KUSHIRIKI GAME CHANGERS.

Kama kwa kusoma hapa umeona GAME CHANGERS ni kitu unachohitaji ili kutoka hapo ulipokwama sasa (na ni kitu unachohitaji kweli), basi chukua hatua sasa ili kuweka nafasi yako ya kushiriki programu hii.

Hatua ya kuchukua ni kutuma ujumbe kwa njia ya wasap wenye majina yako na maelezo kwamba utashiriki programu ya GAME CHANGERS MACHI 2020.

Kwa kufanya hivi unajihakikishia nafasi ya kushiriki programu hii na kunufaika nayo.

Chukua hatua sasa kwa sababu nafasi zilizopo ni chache (tano pekee) na uhitaji ni mkubwa. Tuma ujumbe sasa kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253.

ADA YA GAME CHANGERS NA TAREHE YA KUANZA MSIMU WA MACHI 2020.

Ada ya kushiriki kwenye programu ya GAME CHANGERS ni tsh laki tatu (300,000/=) ambayo ni sawa na uwekezaji wa tsh elfu 10 kwa siku.

Kwa uwekezaji huu ambao unaonekana ni mkubwa, utaweza kupata thamani ambayo ni mara kumi ya ulichowekeza. Ninakuhakikishia kwamba kama utajitoa kweli kwenye programu hii, basi utaweza kupata thamani mara 10 ya uwekezaji huo. Yaani kwa kiwango cha chini sana, matokeo utakayopata thamani yake itakuwa shilingi milioni 3.

Msimu wa mwezi Machi wa programu hii ya GAME CHANGERS 2020 utaanza rasmi siku ya jumamosi tarehe 07/03/2020 na kumalizika siku ya jumamosi ya tarehe 04/04/2020.

Ili kupata nafasi ya kushiriki programu hii unapaswa kulipa ada ya ushiriki, tsh 300,000/= kabla ya tarehe 03/03/2020. Pia tuma mapema taarifa ya ushiriki ili uweze kupata nafasi hii, kwa kutuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye majina yako na kwamba utashiriki GAME CHANGERS JANUARI 2020.

Nafasi za kushiriki programu hii kwa mwezi machi ni 5 pekee, na nafasi zinatolewa kwa wale wanaowahi. Yaani nafasi zikishajaa hakuna tena nyingine itakayopatikana.

Hivyo nikushauri sana uchukue hatua mara moja unapopata ujumbe huu ili usikose nafasi hii. Kwa sababu programu hii inakuja mara chache chache sana.

Mwisho wa kutuma ada ili kupata nafasi ya kushiriki programu ya GAME CHANGERS MACHI 2020 ni tarehe 03/03/2020. Na kwa wale watakaokuwa wamepata nafasi, siku ya tarehe 05/03/2020 nitakuwa na maongezi ya simu na kila mmoja ili kujadili kwa kina alipokwama na kuweka mipango ya kufanyia kazi.

Tarehe 07/03/2020 tutaanza rasmi programu yetu na siku hiyo jioni saa 11 tutakuwa na maongezi ya simu ya kwanza kwa ajili ya kutambuana na kupeana mikakati ya kila mmoja wetu.

Karibu sana kwenye GAME CHANGERS, programu pekee inayoweza kukutoa hapo ulipokwama sasa.

Kama una nia ya kushiriki kwenye programu hii, tuma ujumbe sasa kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye maneno GAME CHANGERS ili kujiwekea nafasi.

Naamini hutaiacha nafasi hii adimu sana kwako kuondoka kwenye mkwamo ikupite. Chukua hatua sasa ili uweze kufanikiwa zaidi na kuondoka hapo ulipokwama sasa.

Tuma ujumbe sasa kwenye wasap namba 0717396253 kujiwekea nafasi ya SIKU 30 ZA KUONDOKA KWENYE MKWAMO NA KUKUA ZAIDI.

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,

Kocha Dr Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha