Rafiki yangu mpendwa,

Mambo ya kufanya ni mengi lakini muda tulionao wa kufanya mambo hayo ni mchache. Tangu enzi na enzi muda tulionao kwenye siku yetu ni masaa 24, lakini mambo ya kufanya kwenye muda huo yamekuwa yanaongezeka kila siku.

Ubaya zaidi ni kwamba, kila kinachokuja mbele yetu kinaonekana ni muhimu kwetu kufanya. Na hilo linapelekea sisi kuhangaika na mambo mengi kwenye siku zetu. Unaimaliza siku ukiwa umechoka kweli kweli, lakini ukiangalia, hakuna kikubwa ulichofanya.

Ukiacha mambo yako mengi ya kufanya, bado kuna wengine wanaokuja kwako na mambo yao ya kufanya, wakitaka uwasaidie au kushirikiana nao. Japokuwa unajua huna muda wa kufanya, unakubaliana nao na kinachotokea ni mnaanza kuzungushana na kusumbuana.

Leo nakwenda kukushirikisha mwongozo sahihi ambao ukiutumia utaweza kujiwekea vipaumbele sahihi na kutokuhadaiwa na chochote kile. Mwongozo huo unakuonesha wazi kipi ni muhimu na kipi ni sumbufu na hautoi nafasi ya kujidanganya. Kama utachagua usumbufu baada ya kutumia mwongozo huo, hapo utakuwa umechagua mwenyewe na hutaweza kusingizia kwamba hukujua.

Karibu ujifunze mwongozo mkuu wa kujiwekea vipaumbele vya maisha ya mafanikio.

Kwenye KISIMA CHA MAARIFA, tunao mwongozo mkuu wa kuweka vipaumbele vya maisha ya mafanikio ambao tunaufuata kila siku.

Mwongozo huo mkuu una maneno matatu; AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA. Haya ni maeneo matatu ambayo ukiyazingatia vizuri lazima utaweza kujiwekea vizuri vipaumbele vyako na kupiga hatua kubwa sana kwenye maisha yako. Haijalishi unaanzia wapi au uko kwenye mazingira gani, hakuna anayesimamia hayo na kusumbuka na usumbufu wa yale yasiyo na manufaa kwa maisha yake.

AFYA.

Rasilimali ya kwanza na muhimu tuliyonayo kwenye maisha yetu ni afya zetu. Bila ya kuwa na afya imara, mengine yote hayawezekani. Haijalishi unataka mafanikio makubwa kiasi gani, kama huna afya imara, hutaweza kuyafikia.

Hivyo afya inapaswa kuwa kipaumbele cha kwanza kwako. Kabla hujafanya jambo lolote lile, jiulize kwanza kama linachangia wewe kuwa na afya bora au linazorotesha afya yako.

Kwa kuzingatia kipaumbele hiki muhimu cha afya, utaepuka kufanya mambo mengi ambayo umekuwa unashawishika kufanya, kwa sababu hayana mchango kwa afya yako. Pia unajua hatua sahihi za kuchukua ili kuifanya afya yako kuwa bora na kuweza kufikia mafanikio makubwa.

Afya yetu imegawanyika katika maeneo matatu;

Eneo la kwanza ni afya ya mwili, hii ni afya ya miili yetu, ambayo ni muhimu kwa sababu mwili unahitaji kuwa na nguvu ya kupambana ili ufanikiwe. Ili kuwa na afya bora ya mwili unapaswa kula kwa usahihi, kufanya mazoezi na kupumzika. Pia unapaswa kuepuka vyakula visivyo vya afya, kuuweka mwili kwenye msongo kwa muda mrefu na kutokufanya mazoezi.

Eneo la pili ni afya ya kiroho, hili ni eneo letu la kiroho na kiimani, ambalo linatupa msukumo mkubwa wa kupiga hatua kubwa kwenye maisha yetu. Roho ndiyo inausukuma mwili kuchukua hatua za kufanikiwa. Ili kuwa na afya bora ya kiroho unapaswa kujijengea matumaini, kuomba na kufanya tahajudi. Pia unapaswa kuepuka hali za kukatisha tamaa na kuwa na chuki au vinyongo na wengine.

Eneo la tatu ni afya ya akili, hili ni eneo linalohusisha akili zetu ambazo ndiyo zinatuongoza katika kufikiri na kufanya maamuzi sahihi. Akili ndiyo inatoa mwongozo kwa mwili na roho. Ili kuwa na afya bora ya akili unapaswa kulisha akili yako maarifa sahihi, kutumia akili yako kufikiri na kuibua ubunifu ndani yako. Pia unapaswa kuepuka matumizi ya vilevi, epuka habari na taarifa nyingine hasi na kataa kuiga vitu vya wengine.

Unapoanza na kigezo cha afya, zingatia maeneo yote matatu na hakikisha chochote unachofanya kinachangia wewe kuwa na afya bora zaidi.

UTAJIRI.

Kuna watu wakisikia neno utajiri wanajisikia vibaya, wanaona ni kitu kibaya au tamaa ya kujilimbikizia mali ambazo mtu anachukua kwa wengine. Hivyo ndivyo jamii imewaharibu watu kwenye utajiri.

Lakini nikuambie kitu kimoja, utajiri ni kanuni ya asili, ndiyo namna pekee asili imeweza kuwepo mpaka leo na kutuwezesha kuishi hapa duniani.

Chukua mfano mdogo wa vitu tunavyotumia kila siku, mfano samaki ambao tunakula. Kwa hakika hatutengenezi samaki hao, bali tunawavua kutoka kwenye maeneo ya maji. Sasa fikiria miaka yote ambayo sisi binadamu tumekuwa tunavua samaki, lakini hawaishi! Hii ni kwa sababu asili inaendelea kuzalisha kwa wingi kadiri inavyohitajika.

Huo ndiyo msingi mkuu wa utajiri, kuendelea kuzalisha zaidi na siyo tu kile kinachokutosha.

Hivyo unapaswa kuwa tajiri kwenye maisha yako, kwa sababu ndiyo namna pekee unaweza kuwasaidia wengine na dunia kwa ujumla. Asili ina msaada kwetu kwa sababu inazalisha zaidi.

Utajiri ni kigezo muhimu unachopaswa kukitumia wakati wa kuweka vipaumbele vyako.

Kabla hujafanya kitu, jiulize kama kinakufanya uwe tajiri zaidi au kinakufanya uwe masikini. Wewe unachotaka ni utajiri, hivyo chochote unachofanya, kinapaswa kuchangia kukufikisha kwenye utajiri huo.

Njia pekee ya kupata utajiri kwenye maisha ni kwa kutoa thamani kubwa zaidi kwa wengine kuliko unavyotoa sasa. Kwa kila unachofanya, nenda hatua ya ziada, yafanye maisha ya wengine kuwa bora kuliko yalivyo sasa na wao watakulipa zaidi. Chochote unachofanya nje ya hapo ni kupoteza muda wako.

Kama unaweka muda na nguvu zako kwenye kitu ambacho hakichangii wewe kuwa tajiri zaidi ya ulivyo sasa, umechagua kuupoteza muda huo.

HEKIMA.

Kufikiri kwa umakini na kufanya maamuzi sahihi kunawezekana kama tu mtu utakuwa na maarifa sahihi na unayoweza kuyatumia. Hiyo ndiyo hekima, kuwa na maarifa unayoyafanyia kazi.

Kuwa na maarifa pekee haitoshi kama huwezi kuyatumia maarifa hayo. Hekima ni pale unapokuwa na maarifa na kuweza kuyatumia kufanya maamuzi sahihi.

Hekima ni kigezo muhimu kutumia katika kuweka vipaumbele vyako. Chochote unachochagua kufanya, kinapaswa

Njia bora kwako kujijengea hekima ni kuwa mtu wa kujifunza kila wakati, kila unapokuwepo, hakikisha kuna kitu unajifunza, kila unayekutana naye, jifunze kitu kutoka kwake na kwa kila unachofanya, jifanyie tathmini kuona ni namna gani unaweza kufanya kwa ubora zaidi wakati mwingine.

Unapoteza hekima pale unapohangaika na mambo yasiyo na manufaa kwako, pale unapokazana kupata taarifa badala ya kupata maarifa na pale unapoamini tayari unajua kila kitu hivyo huna haja ya kujifunza tena.

Kila siku hakikisha unakuwa na hekima zaidi unapokwenda kulala kuliko ulivyokuwa wakati unaamka. Na ukienda hivyo kwa miaka mingi, lazima utakuwa na mafanikio makubwa.

Rafiki yangu mpendwa, hayo ndiyo maeneo matatu ya kuzingatia kwenye mwongozo mkuu wa kuweka vipaumbele vya maisha ya mafanikio, AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA. Zingatia maeneo hayo matatu kila siku na kila mahali, na mara zote utafanya maamuzi sahihi ya kuwa na vipaumbele sahihi vitakavyokufikisha kwenye mafanikio makubwa.

Kwa kila unachoshawishika kufanya kwenye siku yako, kichuje kwanza kwa kutumia vigezo hivyo vitatu. Utaweza kukichuja kwa kujiliza maswali haya matatu na kujipa majibu sahihi kabla hujachukua hatua.

1. Je hiki ninachotaka kufanya kinachangia mimi kuwa na afya bora zaidi ya mwili, akili na roho kuliko niliyonayo sasa?

2. Je hiki ninachotaka kufanya kinanifanya niwe tajiri zaidi ya nilivyo sasa?

3. Je hiki ninachotaka kufanya kinanifanya kuwa na hekima zaidi nitakapomaliza kukifanya kuliko niliyokuwa nayo kabla ya kuanza kukifanya?

Katika maswali hayo matatu, hakikisha unapata angalau jibu moja la ndiyo  ndipo ufanye kitu hicho. Kama majibu yote ni hapana basi hupaswi kufanya kitu hicho, haijalishi ni nani anakutaka ukifanye, hakuna manufaa yoyote kwako na pia hakitakuwa na manufaa kwa wengine.

Na uelewe kabisa hufanyi hivi kwa ubinafsi, bali kwa sababu unawajali wengine. Unapoweka vipaumbele kwenye AFYA yako, UTAJIRI wako na HEKIMA yako, hunufaiki tu wewe mwenyewe, bali kila anayekuzunguka pia ananufaika sana. hivyo usijisikie vibaya kukataa kile ambacho hakina mchango kwenye hayo matatu.

Karibu kwenye mazingira yatakayokuwezesha kuishi mwongozo huo kila siku.

Rafiki yangu mpendwa, tunaishi kwenye jamii ambazo kila mtu anakutaka ukubaliane naye. Mtu anapokuja kwako akitaka ufanye kitu fulani, anategemea ukubaliane naye bila ya kuhoji. Ukikataa kufanya anakuona wewe ni mtu mbaya na usiyejali.

Hivyo ndivyo jamii imekutega na kukuingiza kwenye makubaliano ambayo yanakutesa kwa sababu hayana mchango wowote kwako, lakini pia huwezi kuyaacha maana ulishaahidi.

Unakuwa unajua kabisa kwamba kitu hakina manufaa kwako, na hata kwa hao wengine, lakini huthubutu kusema HAPANA. Unakubali ili kuwaridhisha wengine, lakini unaishia kujiangusha wewe mwenyewe.

Hivyo ni vigumu sana kuweza kuishi kwa mwongozo huu ukiwa ndani ya jamii ya kawaida, kwa sababu jamii hiyo itatumia kila mbinu kuhakikisha unaanguka na kuondokana na msimamo wako.

Unafikiri kwa nini vyakula visivyo vya afya vinapata matangazo mengi kwenye vyombo vya habari? Kila mtu anajua vyakula hivyo ni vibaya kwa afya, lakini bado vinatangazwa na watu kushawishiwa wavitumie. Unadhani kwa nini jamii nyingi zinaona utajiri ni kitu kibaya na matajiri kuonekana ni watu waovu? Hata upande wa hekima, angalia kwenye jamii nyingi, watu hawataki ufikiri au kuhoji, wanataka ukubaliane na kile ambacho kimeshazoeleka.

Kwa mazingira haya, ni vigumu sana kuishi kwa mwongozo huu wa kujiwekea vipaumbele vitakavyokufikisha kwenye mafanikio makubwa.

Kuna mazingira yanayokuwezesha kuishi mwongozo huu wa kuweka vipaumbele kwa mafanikio kila siku, bila ya kuacha, kuchoka au kukatishwa tamaa.

Mazingira hayo ni KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kuwa kwenye KISIMA, kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI inayokupa nafasi ya kufikiri kwa kina na kuianza siku yako ukiwa na mtazamo sahihi. Pia katika tafakari hiyo unapata nafasi ya kujikumbusha mwongozo huu muhimu wa mafanikio. Hutaianza siku kabla hujajikumbusha AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA, hivyo hata atakapokuja mtu kwako akikutaka ufanye kitu fulani, utakichuja kwanza kwa mwongozo wako wa kujiwekea vipaumbele kabla hujakubali kufanya kitu hicho.

Ndani ya KISIMA CHA MAARIFA unazungukwa na watu wengine ambao wanaishi mwongozo huu mkuu wa mafanikio hivyo hilo linakupa na wewe hamasa ya kuishi kuwa na mwongozo huo pia. Unapokuwa pekee kwenye eneo ambalo hakuna anayeishi miongozo hii inakatisha tamaa, lakini unapozungukwa na wengine wanaoishi miongozo hiyo, inakupa moyo wa kuendelea kuiishi miongozo hiyo.

Rafiki yangu mpendwa, kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, basi jua unajichelewesha sana kufikia mafanikio makubwa. Unajiweka kwenye hatari ya kuendelea kuhangaika na mambo ambayo siyo kipaumbele kwako na wala hayawezi kukufikisha kwenye mafanikio makubwa.

Karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo hii, ili upate nafasi ya kuishi mwongozo huu muhimu wa mafanikio na uweze kuepuka kupoteza muda wako kwa yale yasiyo na mchango kwenye mafanikio makubwa unayotaka kwenye maisha yako.

Kupata maelezo ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA soma maelezo hapo chini.

KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi bila vitendo.

Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;

1. Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.

2. Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)

3. Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

4. Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.

5. Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.

6. Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.

7. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.

8. Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.

9. Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.

10. Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.

Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.

Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.

Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.

Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.

Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo kwa kulipa ada tsh 100,000/= kwa namba 0717396253 na utapata nafasi ya kuingia kwenye jamii hii ya tofauti kabisa itakayokuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail  

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania