“It is much easier to recognise error than to find truth; for error lies on the surface and may be overcome; but truth lies in the depths, and to search for it is not given to every one.” – Johann Wolfgang von Goethe

Ni rahisi kuona makosa kuliko ilivyo kuona ukweli.
Hii ni kwa sababu makosa yanaonekana kirahisi kwa nje,
Wakati ukweli unapaswa kuchimbwa zaidi ndani.

Ni rahisi kukosoa kuliko kushauri,
Kwenye kukosoa unaangalia yale ya nje, lakini ili kushauri ni lazima kwanza ujue na ya ndani pia.

Kwa kujua haya, usikimbilie tu kuangalia nje na kukosoa, badala yake zama ndani, elewa kwa kina kisha shauri kwa usahihi.

Siyo kila mtu anaweza kuuona ukweli,
Kwa sababu una gharama kuufikia,
Wewe chagua kuwa upande wa ukweli, ndiyo upande sahihi, wenye manufaa kwako na wengine pia.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu tangazo la kuokoa maisha, soma zaidi hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/09/22/2092

Rafiki yako,
Kocha Dr Makirita Amani.