Kama leo hii itaamuliwa kwamba fedha zote duniani zikusanywe na kisha kila binadamu apewe kiwango sawa, ndani ya mwaka mmoja, waliokuwa matajiri watakuwa wamekuwa matajiri zaidi na waliokuwa masikini watakuwa wamekuwa masikini kupindukia.

Hiyo ni kwa sababu kinachowatofautisha matajiri na masikini siyo fedha walizonazo, bali mtazamo walionao juu ya fedha na tabia ambazo wamejijengea kwenye eneo la fedha.

Kuna tofauti nyingi kati ya matajiri na masikini, lakini hapa nakwenda kukushirikisha mbili ambazo ukianza kuzifanyia kazi, basi utaweza kuituliza fedha inayopita kwenye mikono yako.

Uzuri ni kwamba, matajiri na masikini wote kuna kiasi fulani cha fedha kinapita kwenye mikono yao, ila matajiri wanaweza kuituliza, huku kwa masikini ikiwaponyoka na kubaki hawana chochote.

Tofauti kubwa ya kwanza ya matajiri na masikini ni mtazamo wa kifedha, kwa matajiri fedha wanayoingiza ni kama mbegu, hawatumii yote, badala yake wanatenga kiasi fulani ili iweze kuzalisha zaidi. Kwa upande wa masikini, fedha kwao ni kitu cha kutumia, wanapoipata wanatumia yote haraka mpaka iishe na kama hawajatosheka na matumizi wanakopa ili kutumia zaidi.

Nimekuwa nasikia vilio vya wengi, ambao kabla hawajawa na fedha wanakuwa na mawazo mazuri ya kufanya mambo makubwa. Lakini wakishakamata fedha, wanasahau mawazo yote mazuri, wanaona vitu vizuri vya kutumia mbele yao, wanatumia mpaka fedha inapoisha ndiyo wanakuja kuyakumbuka mawazo mazuri waliyokuwa nayo awali.

Kwa watu wa aina hii, hakuna kiwango cha fedha kinachoweza kuwatosha wala kuwatoa kwenye umasikini, mpaka pale watakapobadili mtazamo wao wa ndani kuhusu fedha, waache kuiangalia kama kitu cha kutumia na waanze kuiangalia kama mbegu ya kupanda ili kuvuna zaidi.

Kama ungependa njia bora ya kujijengea mtazamo huu, nina zawadi nzuri hapo chini kwa ajili yako, endelea kusoma.

Tofauti kubwa ya pili kati ya matajiri na masikini ni tabia walizonazo kwenye fedha. Kwa matajiri, fedha ni kitu wanachokitumikisha, wanakituma kikafanye kazi na kinawaletea faida. Matajiri hawatumii nguvu kubwa kwenye kupata fedha, na hivyo wanakuwa hawana ukomo. Lakini kwa upande wa masikini, wao ndiyo wanaoitumikia fedha, wanapata fedha pale tu wanapofanya kazi, wasipofanya kazi hakuna fedha. Wanakuwa watumwa wa fedha maisha yao yote.

Sasa ukichukua hii ya kutumikia fedha, ukajumlisha na matumizi ya fedha hiyo yote pale anapoipata, ndiyo sababu hata fedha zikigawanywa zote, mwisho wa siku zitarudi kwa matajiri.

Zinarudi kwa matajiri kwa sababu wao wana mifereji ya kutiririsha fedha zije kwao, wakati masikini hawana mifereji hiyo.

Chukua mfano rahisi kwa hapa Tanzania, kama fedha zote zitagawanywa kwa usawa kwa watu wote, hata kama umepewa bilioni moja, mwisho wa siku utaanza kutumia, utanunua vitu mbalimbali na wanaokuuzia vitu hivyo ni matajiri ambao walishajijengea mifumo ya kuchuma fedha. Hivyo mwisho wa siku, fedha zote zinarudi kwao.

Kama unataka kutoka kwenye umasikini na kuifanya fedha ije kwako, lazima na wewe utengeneze njia ya fedha zako kufanya kazi na kukuletea faida hata kama wewe haupo moja kwa moja. Na njia za kufanya hivyo ni mbili, biashara na uwekezaji.

Ondokana kabisa na tabia ya kuwa mtumwa wa fedha, kufanya kazi ndiyo ulipwe na anza mapema kutengeneza mfumo wa kulipwa bila hata kufanya kazi, kwa kuwa na mfumo mzuri wa fedha zako kukufanyia kazi.

Sasa ni wakati wa zawadi.

Kwa kuwa nakupenda sana wewe rafiki yangu, na kwa kuwa msingi mkuu wa huduma ninazotoa ni kuhakikisha wewe unafanikiwa kwanza ndiyo mimi niweze kufanikiwa, leo nakupa zawadi ya kitabu cha KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI.

Hiki ni kitabu ambacho kinaeleza sababu 25 zinazowafanya watu kubaki kwenye umasikini, hapa tumeziona mbili tu, kuna nyingine 23 ambazo bado hujaziona, ambazo nyingi unaziishi na ni kikwazo kwako, lakini hakuna ambaye amewahi kukuambia.

Sasa nafasi umeipata ya kuzijua, pata leo kitabu hiki cha KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI na uweze kujifunza, uchukue hatua na kuondoka kwenye umasikini.

Kitabu ni nakala tete na kinapatikana kwenye App ya SOMA VITABU, hii ni App mpya na rahisi ya kusoma vitabu kupitia simu yako au tablet yako, unaipakua na kujiandikisha na kisha kulipia na kusoma kitabu moja kwa moja.

Kitabu hiki cha KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI kwenye app bei yake ya kawaida ni tsh elfu 3 (3,000/=), lakini kwa kuwa sitaki wewe uwe na sababu ya kubaki kwenye umasikini, siku ya leo tarehe 23/09/2020 utakipata kwa kulipia tsh elfu moja tu (1,000/=).

Chagua leo kutokununua soda au gazeti au kingine unachonunuaga kwa elfu moja na lipia kitabu cha KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI, kwani maarifa utakayoyapata kwenye kitabu hicho, yatakuwa na manufaa makubwa kwako.

Nikusihi uchukue hatua sasa rafiki yangu, kwa sababu zawadi hii ni ya siku moja tu, nikitaka upate maarifa haya ili uache kuwa kikwazo kwako mwenyewe kupiga hatua.

Kupata maelekezo ya jinsi ya kuipakua app na kuitumia, fungua kiungo hiki; https://amkamtanzania.com/somavitabuapp

MUHIMU; Zawadi hii ipo kwenye kitabu kupitia App ya SOMA VITABU pekee, na app kwa sasa inapatikana kwa Android pekee, hivyo kwa wale wanaotumia mifumo mingine, niwasihi muwe na subira, app ya mifumo hiyo itakapokuwa tayari na nyie mtapata zawadi zenu.

Ni wakati wa kuvunja tabia za kimasikini zinazokurudisha nyuma, anza leo na zawadi hii ya kitabu cha KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI na uchukue hatua kwenye yale unayojifunza, kwa hakika hutabaki hapo ulipo sasa.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania