“During the day you should behave in such a way that you can sleep at night in peace; and in your youth you should behave in such a way that you can live in your old age in peace.” — Indian proverb
Kwa kila unachotaka kufanya, usiangalie tu manufaa unayopata wakati wa kufanya,
Bali fikiria pia madhara ya baadaye ya kile unachotaka kufanya.
Wakati wa mchana, kila unachotaka kufanya jiulize kama utalala kwa amani usiku.
Hakimu wa kwanza kwako ni wewe mwenyewe, ukifanya chochote ambacho siyo sahihi, hata kama utanufaika, usiku hutalala kwa amani.
Nafsi yako itakusuta sana kwa kile ulichofanya.
Kila maamuzi unayotaka kufanya na kila hatua unayopanga kuchukua, jiulize kama utaweza kulala kwa amani usiku.
Unapokuwa kijana, fikiria uzee wako kabla hujafanya chochote.
Kwa chochote unachotaka kufanya, jiulize kama utaishi kwa amani wakati wa uzee wako.
Ukiwa kijana unaweza usijali sana, unaweza kuamua kufanya chochote kwa manufaa ya wakati huo, lakini uzeeni utaumia na kujutia kwa mengi uliyofanya au kushindwa kufanya ulipokuwa kijana.
Kwa kila unachofanya au kutokufanya, unaweza kujisikia vizuri sasa, lakini baadaye ukawa na majuto makubwa.
Hivyo kigezo chako cha maamuzi kisiwe tu unapata nini sasa, bali pia utajutia nini baadaye.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Ukurasa wa kusoma leo ni kuhusu uimara wa msingi, soma hapa; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2020/12/11/2172
Rafiki yako anayekupenda sana,
Kocha Dr Makirita Amani.
Asante sana kocha kwa ujumbe
LikeLike
Karibu.
LikeLike