
Ipo kauli maarufu kwamba hakuna kipya chini ya jua, tungekuwa tunaielewa kauli hii, tungejiepusha na mengi. Lakini huwa hatuielewi, huwa hatujifunzi kwa historia na hivyo kurudia makosa yale yale.
Angalia kwenye utapeli, hakujawahi kuja utapeli mpya kabisa, utapeli wowote ule unatumia uongo au tamaa kuwanasa watu. Hii ina maana kama tungekuwa tunautafuta ukweli mara zote na kudhibiti hisia zetu wakati wa kufanya maamuzi, tusingetapeliwa kamwe.
Kadhalika kwenye mafanikio, historia inatuonesha wengi ambao walijinufaisha kwa njia zisizo sahihi na baadaye kupoteza kila kitu. Lakini bado watu wanarudia njia hizo kila wakati.
Kabla ya kufanya kitu chochote jiulize kama kitu hicho ni kweli na sahihi kufanya. Kisha hakikisha hisia zako hazikutawali katika kufanya maamuzi hayo.
Njia za kweli na sahihi huchelewa, lakini matokeo yake ni mazuri. Njia za uongo na zisizo sahihi huwahi, lakini matokeo yake ni mabaya.
Ukurasa wa leo ni kuhusu wewe siyo mtakatifu na mjuaji sana, soma; http://www.kisimachamaarifa.co.tz/2021/01/24/2216