2273; Marudio…
Kumbuka wimbo ambao unaupenda sana, umeusikiliza au kuuangalia mara ngapi?
Kumbuka chakula unachokipenda sana, umekila mara ngapi kwenye maisha yako?
Kumbuka somo ambalo umewahi kufaulu kuliko mengine ulipokuwa shuleni, ulilisoma mara ngapi?
Yale yote muhimu na unayoyapenda, umekuwa unayarudia rudia kila mara.
Mziki unaoupenda huwa unausikiliza au kuuangalia kila mara, bila ya kuchoka.
Chakula unachopenda huwa unakila mara kwa mara na hukichoki.
Na somo ulilolipenda zaidi shuleni, ulikuwa unarudia kulisoma zaidi kuliko masomo mengine na ukalifaulu ziadi.
Sasa inapokuja kwenye mafanikio, kwa nini hutaki kutumia kanuni hiyo muhimu kufanikiwa?
Kwa nini unataka ufanye kitu mara moja tu uwe umefanikiwa?
Kwa nini unataka usome kitabu mara moja tu uwe umekielewa?
Kwa nini unataka uwaambie watu kitu mara moja wakuelewe na kukubaliana na wewe?
Hivyo sivyo maisha yalivyo, chochote unachohitaji kifanikiwa kwenye maisha yako, kinahitaji marudio yasiyo na mwisho.
Kazi au biashara yako, lazima urudie kuifanya wakati wote ili kupata na kudumu kwenye mafanikio.
Vitabu unavyosoma, lazima uchague ambavyo utavirudia mara kwa mara ili uvielewe na kuviishi ka wakati.
Na hata wale unaotaka kuwashawishi wafanye kitu fulani, iwe ni kukubaliana na wewe au kununua unachouza, lazima urudie mara kwa mara ndiyo wasukumwe kuchukua hatua.
Hakuna utakachofanya mara moja kikakutosha, bali kila unachofanya unahitaji marudio yasiyo na ukomo ndiyo ufikie mafanikio makubwa.
Tunaishi kwenye zama za kelele na usumbufu mkubwa, ambapo kila mtu hana muda na amevurugwa, usipotumia marudio, hutaweza kufanya makubwa, kujifunza na kuwashawishi wengine.
Angalia matangazo ya makampuni makubwa ya simu au vinywaji, huwa yanarudiwa kila siku na kila mara, hata kama umeshalisikia tangazo linarudiwa tena na tena na tena. Makampuni hayo yanajua bila marudio hakuna matokeo.
Je ni marudio gani unatengeneza kwenye maisha yako?
Vitu gani unapanga kufanya kila siku ya maisha yako?
Vitabu gani umechagua kurudia kuvisoma mara kwa mara?
Ujumbe gani umechagua kujiambia mara kwa mara ili ukusukume kufanikiwa?
Karibu ushirikishe kwenye maoni hapo chini na mara kwa mara nitakuwa narudia kukukumbusha usisahau.
Kocha.
Nataka kurudia kusoma vitabu vifuatavyo kila mwaka mpaka mwisho wa maisha yangu
Think and grow rich, school of money, laws of success, elimu ya msingi ya fedha, elimu ya msingi ya biashara, una nguvu za kutenda miujiza, Almanack of naval ravikant, kuran.
Vilevile kila mwezi ninarudia kuweka 10% mapka 20% ya kipato changu kwa ajili ya kuwekeza maisha yangu yote.
Kila siku napenda kupata ujumbe uhusio njia za kujiongezea kipato
LikeLike
Vizuri sana Samizi.
LikeLike
Ahsante saana kocha makirita Amani mimi kwa kipindi hiki ntakuwa na marudio ya mara kwa mara katika usomaji wa vitabu vifuatavyo, kitabu cha Tano za majuma 50ya mwaka, nguvu ya kutenda miujiza, usomaji wa makala unayo post kila siku katika, mtandao wa kisimachamaarifa, amka mtanzania, kundi la usomaji vitabu Tanzania, n.k.
LikeLike
Vizuri sana Emanuel.
LikeLike
Ama kwa hakika marudia ndio njia pekee ya kufanikisha jambo.
Katika hatua za kuwafundisha wanafunzi kuna kipengele kinahusu kukazia maarifa, reinforcement. Hapa ndipo wanaojifunza wanarudia kwa kina yale waliyojifunza na kuyaelewa vizuri. Mimi pia nitairudia, nitairudia na kurudia na tena na tena ili kupata matokeo bora.
Nitarudia kusoma vitabu,
Nitarudia kuwapigua watu wa karibu simu I’ll kuboresha uhusiano,
Nitarudia kuweka akiba,
Nitarudia kuwaambia wateja Asante na karibu tena…
Nitarudia kuandika makala,,,
Nitarudia kufanya kwa ubora wa hali ya juu na ubunifu,
Nitarudia kupangilia muda wangu..
Nitarudia kuamka mapema…
Nitarudia,na kurudia kila kitu.
Asante sana kocha
LikeLike
Vizuri Stephano.
LikeLike
Asante Sana kocha kwa kweli marudio ndiyo Mafanikio kwenye chochote ambacho mtu anafanya. Leo nimepata muda wa kurudia kusoma diary yangu ya mwaka 2017 nimepata hamasa kubwa Sana. Ushindi upo kwenye marudio. Asante Sana tena kocha.
LikeLike
Vizuri Tumaini
LikeLike