Rafiki yangu mpendwa,
Uwekezaji ni moja ya mahitaji muhimu sana kwenye safari ya mafanikio.
Unapaswa kufanya uwekezaji endelevu, ambao baadaye utakulipa sana.
Lakini karibu kila uwekezaji huwa una hatari fulani ya kupoteza.
Pale uchumi unapoyumba, uwekezaji ambao mtu amefanya unaweza kukosa thamani kabisa na hivyo mtu akawa amepoteza.
Pamoja na kujinyima kwa miaka mingi ili kuwa na uwekezaji, unaweza kupoteza kila kitu ndani ya muda mfupi.
Na hilo limekuwa linawavuruga wengi, kwani wanakuwa hawakutegemea na hivyo hawakuwa na maandalizi.
Rafiki, upo uwekezaji mmoja muhimu ambao ukiufanya hakuna hatari ya kupoteza kabisa.
Yaani hata uchumi uyumbe kiasi gani, uwekezaji wako unabaki ukiwa na thamani kubwa na kukuwezesha kuvuka nyakati ngumu kama hizo.
Uwekezaji huo ni ule unaoufanya kwako binafsi, yaani uwekezaji wa ndani yako mwenyewe.
Kila uwekezaji unaoufanya ndani yako, kwa kupata elimu, maarifa, hamasa, uzoefu na mtandao unaoujenga, utaendelea kubaki na wewe milele.
Unaweza kuibiwa uwekezaji mwingine wote, lakini huwezi kuibiwa uwekezaji uliofanya ndani yako mwenyewe.
Hivyo katika mipango yako ya uwekezaji, kipaumbele cha kwanza kinapaswa kuwa uwekezaji ndani yako. Maana ukifanya uwekezaji huo, uwekezaji mwingine utakaofanya utakuwa bora zaidi.

Moja ya uwekezaji binafsi ambao unapaswa kuufanya ndani yako ni kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.
Kwenye semina hii unakwenda kupata maarifa, hamasa, uzoefu na mtandao utakaokuwezesha kufanya makubwa kwenye maisha yako.
Lakini pia utapata nafasi ya kusimamiwa kwa karibu kwa mwaka mzima kwenye kile unachofanya, ili uweze kukifanya kwa viwango vya juu na usiishie njiani.
Rafiki, nikukumbushe kwamba nafasi za kushiriki semina hiyo zimebaki chache na muda wa kupata nafasi hizo ni mdogo sana.
Kwani mwisho wa kupata nafasi ya kushiriki ni tarehe moja Oktoba.
Chukua hatua sasa kama bado hujajihakikishia nafasi. Na kama hujakamilisha kulioa ada yako ya kushiriki semina, kamilisha sasa.
Kujiwekea nafasi wasiliana na 0717 396 253.
Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.
LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.
WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.
MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.
ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.
MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa; 0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.
MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.
HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.
Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.
Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz