Rafiki yangu mpendwa,
Takwimu za biashara zinatisha na kuumiza sana.
Katika kila biashara 10 mpya zinazoanzishwa kila mwaka, 8 zinakuwa zimekufa ndani ya miaka miwili tangu zimeanzishwa.
Na miaka 5 baadaye, ni biashara moja tu inayokuwa na mafanikio.
Takwimu hizi zinatisha na kusikitisha kwa sababu unapoingia kwenye biashara, uwezekano wa kushindwa ni mkubwa kuliko wa kushinda.
Lakini kama ambavyo tumekuwa tunashirikishana, biashara ndiyo njia pekee ya kupata uhuru kamili kwenye maisha.
Kama mtu unataka kupata mafanikio yatakayokupa uhuru mkubwa, unapaswa kumiliki biashara.
Sasa swali linakuja, unawezaje kuwa na biashara ambayo itavuka huo ugumu na kufika kwenye mafanikio makubwa?
Kwenye kila aina ya mafanikio, sehemu ya kwanza ya kujifunza ni kwa wale waliofanikiwa.
Na inapokuja kwenye biashara, zipo ambazo zimedumu kwa muda mrefu licha ya nyingi kufa katika kipindi hicho.

Biashara hizo ambazo zimedumu kwa muda mrefu, zimekuwa na sifa ambazo biashara nyingine zinakosa.
Hapa tunakwenda kujifunza sifa hizo ili tuweze kuzijenga kwenye biashara zetu nazo ziweze kudumu muda mrefu.
1. Kutoa thamani inayohitajika.
Biashara zote zinazodumu kwa muda mrefu huwa zinatoa thamani ambayo ina uhitaji mkubwa kwa watu.
Inakuwa inatatua tatizo au changamoto ambayo watu wanayo na hawapo tayari kuivumilia, hivyo wanakuwa tayari kulipa ili kupata suluhisho hilo.
Kadiri changamoto inavyokuwa kubwa na inavyowaathiri wengi, ndivyo biashara inanufaika zaidi.
Mfano; Kampuni ya Amazon inatoa suluhisho la mtu kupata bidhaa anayoihitaji, kwa bei nzuri na kwa haraka bila hata ya kutoka nyumbani kwake. Na inatoa suluhisho hilo kwa watu wengi, kitu ambacho kimeipa mafanikio makubwa.
2. Kitu cha kujitofautisha (ukiritimba binafsi).
Biashara zote zinazodumu kwa muda mrefu huwa zina kitu ambacho zinatoa na hakiwezi kupatikana kwenye biashara nyingine yoyote.
Hata pale kunapokuwa na ushindani mkali, kuna vitu wateja wanavipata kwenye biashara hiyo ambavyo hawawezi kuvipata kwenye biashara nyingine yoyote.
Vitu hivyo ndiyo vinawafanya wateja waache biashara nyingine zote zinazofanana na hiyo na kuja kwenye biashara hiyo.
Kitu hicho kinachoitofautisha biashara hiyo huwa ni siri kubwa au kina hati miliki hivyo wengine hawawezi kukiiga.
Mfano; Kampuni ya Cocacola ina kanuni ya kutengeneza kinywaji chake ambayo ni siri. Hakuna mshindani anayeweza kujua kanuni hiyo na kuiiga. Ndiyo maana kuna soda nyingi zinafanana na Cocacola, lakini hakuna hata moja yenye ladha kama ya Cocacola.
3. Akiba kubwa ya mtaji.
Biashara huwa zinapitia nyakati ngumu ambapo biashara inakuwa haiendi vizuri.
Nyakati hizo zipo kabisa nje ya uwezo wa yeyote, lakini zinakuwa na athari kubwa pale biashara inapokuwa haina akiba kubwa ya mtaji ya kuiwezesha kumudu kipindi hicho kigumu.
Chukua mfano wa janga la Corona ambalo lilipelekea nchi nyingi kufunga uchumi wake, biashara nyingi zimekufa ambazo haziwezi kufufuliwa tena.
Biashara inapokuwa na akiba kubwa ya mtaji, itaweza kuvumilia nyakati ngumu na kuvuka ikiwa salama.
Lakini biashara inapotegemea mauzo ndiyo iweze kujiendesha, ipo kwenye hatari kubwa ya kufa kwa sababu uchumi hautabiriki.
Mfano; Kampuni ya Microsoft huwa ina utaratibu wa kuwa na akiba ya kuweza kuendesha biashara kwa mwaka mzima hata kama hakuna mauzo kabisa. Hilo linaipa kinga ya kuweza kuendelea hata pale nyakati zinapokuwa ngumu.
4. Mfumo wa kujiendesha yenyewe.
Biashara yoyote inayomtegemea mwanzilishi kuwepo wakati wote ndiyo iende haiwez kudumu milele.
Hata kama mwanzilishi huyo atakuwa tayari kufanya kazi usiku na mchana ili biashara iende, yeye pia hatadumu milele.
Atafika mahali na kuchoka au maisha yake yatafika ukingoni na hapo ndiyo unakuwa mwisho wa biashara.
Kama umekuwa unajiuliza kwa nini baadhi ya biashara huwa zinakufa pale waanzilishi wanapokufa, jibu ni hilo, zinakuwa hazina mfumo wa kujiendesha zenyewe.
Mfano; Biashara za kifamilia ambazo zimedumu vizazi na vizazi, mfano Rockerfeller, Edison, Ford na Walmart ni kwa sababu kuliwekwa mfumo wa kuziendesha hivyo kila kizazi kipya kinapokuja kinafuata mfumo huo.
5. Kuepuka kiburi na majivuno.
Baadhi ya biashara zinapokuwa, zinaanza kupata kiburi na najivuno. Zinaona kwa ukubwa wake haziwezi kufa (too big to fail) na hivyo kuona zinaweza kufanya chochote.
Kinachotokea ni biashara hizo kuendeshwa kwa mazoea na kuchukua hatari za kijinga kitu ambacho kinazipelekea kupata anguko kubwa.
Biashara zinazodumu muda mrefu huwa zinaepuka sana kiburi na majivuno, zinaendelea kuendeshwa kwa unyenyekevu na kuondoa kabisa mazoea.
Nyingi zimekuwa zinaendeshwa kama vile ndiyo siku ya kwanza na kutengeneza wafanyakazi wake kuweza kufanya maamuzi sahihi katika ngazi za chini ili ukiritimba usiathiri biashara kwa kuchelewesha maamuzi.
Mfano; Kila biashara kubwa iliyowahi kufa, kifo huwa kinaanzia kwenye kiburi na majivuno. Biashara inakuwa inajiamini kupitiliza, inafanya uwekezaji mbaya na kupata anguko kubwa.
Rafiki, hizo ndizo sifa tano za biashara zinazodumu muda mrefu, ambazo unaweza kuzijenga kwenye biashara yako na ikanufaika sana.
Kama unajiuliza unawezaje kujenga sifa hizo kwenye biashara yako, ninazo habari njema kwako.
Ipo fursa ya wewe kuweza kujifunza kwa vitendo kabisa jinsi ya kujenga mfumo wa biashara inayoweza kujiendesha yenyewe na kwa mafanikio makubwa.
Fursa hiyo inapatikana kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ambapo siku ya pili ya semina, imetengwa maalumu kwa ajili ya kwenda hatua kwa hatua kwenye kutengeneza mfumo wa biashara yako.
Hii siyo semina ya kukosa kama kweli unataka kuwa na biashara inayokupa mafanikio na uhuru kamili wa maisha yako.
Pata taarifa kamili hapo chini na uchukue hatua sasa, maana muda uliobaki ni mfupi.
Taarifa muhimu kuhusu SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021.
LINI; Semina itafanyika kwa siku mbili, jumamosi na jumapili, tarehe 16 na 17 Oktoba 2021. Hizo zitakuwa ni siku mbili za kujifunza na kuweka mikakati ya kufanyia kazi kwa mwaka mzima.
WAPI; Semina itafanyika jijini Dodoma, Tanzania. Ni ya kushiriki ana kwa ana ambapo tunakutana kwa pamoja na kuweka mikakati ya kupiga hatua zaidi.
MANUFAA; Kuna manufaa mengi ya kushiriki semina hii, ikiwepo kuongeza kipato chako, kuanzisha na/au kukuza biashara yako, kukuza mtandao wako na kupata usimamizi wa karibu kutoka kwa Kocha kwa mwaka mzima.
ADA; Ada ya kushiriki semina ni tsh laki mbili (200,000/=) kwa siku mbili za semina. Ada hiyo itagharamia ukumbi wa semina, vyakula kwa siku nzima na vifaa vya kuandikia. Ada haitagharamia nauli na malazi, hivyo kila mtu atajigharamia mwenyewe.
MALIPO; Njia za kulipa ada ya kushiriki semina ni zifuatazo; Tigo pesa; 0717396253, Mpesa; 0755953887, CRDB BANK, ACC NO. 0152281977700, NMB BANK, AC NO. 40302535762. Majina; Amani Emanuel Makirita.
Ukishalipia unatuma ujumbe wa kuwa umelipia.
MWISHO WA KULIPIA; Mwisho wa kulipia ada ili upate nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021 ni ijumaa ya tarehe 01/10/2021. Fanya malipo yako mapema ili tuweze kuwa na maandalizi bora ya semina yetu.
HATUA YA KUCHUKUA SASA; Kama bado hujatoa taarifa ya kuthibitisha kushiriki semina, fanya hivyo sasa. Tuma ujumbe kwamba utashiriki semina kwenda namba 0717 396 253 ili kujiwekea nafasi ya kushiriki.
Pia lipa ada yako kama bado hujafanya hivyo, unaweza kulipa kidogo kidogo ila mpaka tarehe 01/10/2021 uwe umekamilisha kulipa ada yako.
Karibu sana rafiki yangu kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2021, usikubali chochote kile kiwe kikwazo kwako kushiriki semina hii. Kwani inakwenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye maisha yako.
Chukua hatua sasa ili kujihakikishia kushiriki semina.
Rafiki yako anayekupenda sana,
Muuza Matumaini Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.somavitabu.co.tz