Rafiki yangu mpendwa,

Ni mwanzo kabisa wa mwaka 2022 ambapo kila mtu yupo kwenye hamasa kubwa ya kuweka malengo ya mwaka huu mpya.

Kila mtu ana matumaini makubwa kwenye huu mwaka, kwamba utakwenda kuwa mzuri na mengi kufunguka.

Lakini kabla hujaendelea na matumaini hayo mazuri uliyonayo, naomba nikurudishe nyuma kidogo.

Hebu kumbuka wakati unauanza mwaka 2021 tulioumaliza. Je hukuwa katika hali kama uliyopo sasa?
Na vipi ulipoanza mwaka 2020, 2019, 2018 na miaka yote ya nyuma?

Rafiki, naamini umeona jinsi ambavyo umekuwa unauanza kila mwaka na matumaini makubwa, ukiwa na malengo na nia nzuri kabisa ya kuufanya mwaka bora kwako.

Lakini haipiti miezi mingi hayo yote yanayeyuka, unajikuta umerudi kwenye mazoea ya mwanzo na hamasa nzima ya mwaka mpya inaisha.

Sasa sitaki urudie tena makosa hayo kwa mwaka huu 2022.
Nataka mwaka huu ukawe wa tofauti kubwa kwako, ukawe mwaka wa kuacha alama fulani kwenye maisha yako.

Na sehemu ya kuanzia ili kukamilisha hilo ni kuachana na malengo.
Najua kwa kusoma hilo la kuachana na malengo hulielewi, kwa sababu kwa miaka yako yote umekuwa unaimbiwa umuhimu wa kuwa na malengo kwenye kila jambo.

Hapa ninachotaka kukusaidia ni uwe na malengo ambayo siyo kikwazo kwako.
Malengo ya mwaka huwa ni kikwazo kwa wengi, kwa sababu wanayafanya kuwa makubwa sana na ya tofauti kabisa na mazoea yao.

Na mwanzo wa mwaka mtu anajiona ana muda mwingi wa kuyafanyia kazi malengo yake hivyo hapati msukumo mkubwa.
Hilo linapelekea ajisahau kwa muda.
Anapokuja kushtuka ni mwaka umekaribia kuisha.
Hapo sasa anajiambia hana tena muda wa kukamilisha malengo yake, hivyo bora asubiri mwaka unaofuata.

Hivyo ndivyo wengi wamekuwa wanaipoteza miaka yao kwa upande wa malengo.

Ninachotaka kukusaidia hapa ni malengo unayojiwekea 2022 yasiwe kimwazo kwako, yaani usione una muda mwingi na wala usione huna muda.
Ninachokwenda kukusaidia ni uweze kufanya makubwa kwa mwaka 2022 tofauti na miaka mingine yote ya maisha yako.

Na kitu kimoja kikubwa ninachokushauri ukomae nacho kwa mwaka 2022 ni MCHAKATO WA SIKU.
Ni kwenye mchakato wa siku ndiyo nguvu ya kufanya makubwa 2022 imelala.

Wacha nikupe mifano ili uelewe vizuri;

Kusoma;
Unaweza kuweka malengo ya vitabu vingapi unataka kusoma kwa mwaka. Lakini hilo halina nguvu kama kupanga kusoma kurasa 10 tu za kitabu kwa siku kila siku.
Kwa kufanya hivyo, kila mwezi utakuwa umesoma kitabu kimoja na kwa mwaka siyo chini ya vitabu 10, ambayo ni mamba kubwa ukilinganisha na wengi ambao hawasomi hata kitabu kimoja.

Kuandika;
Unaweza kuweka lengo la kuandika vitabu kadhaa kwa mwaka. Lakini hilo halina nguvu kama kuamua kuandika maneno 500 tu kwa siku kila siku.
Kwa kufanya hivyo, kila baada ya siku 100 utakuwa umekamilisha kitabu. Hivyo kwa mwaka utakuwa umeandika siyo chini ya vitabu vitatu.

Kipato;
Unaweza kupanga kuongeza kipato chako kwa kiasi fulani kwa mwaka. Ila hilo halina nguvu kama kuamua kuongeza thamani zaidi kila siku kwenye kile unachofanya. Kama unafanya biashara, kila siku pambana kupata mteja mpya au kuuza zaidi kwa mteja aliyepo. Na kama umeajiriwa, kila siku nenda hatua ya ziada kwenye majukumu yako, toa thamani zaidi na kipato kitaongezeka sana.

Akiba;
Unaweza kupanga kuweka kiasi fulani cha akiba kwa mwaka. Lakini hilo halina nguvu kama kuamua kwenye kila kipato uondoe asilimia fulani kabla hujaanza matumizi. Hata kama ni asilimia 1, muhimu ni kufanya kwa msimamo na mwisho wa mwaka utajikuta una akiba ambayo hukuwa nayo awali.

Mazoezi;
Unaweza kupanga upunguze kilo kadhaa ndani ya muda fulani. Unaweza kufanikiwa lakini baada ya muda uzito ukaongezeka tena. Lakini kama utaamua kufanya mazoezi kwa nusu saa tu kila siku, utapunguza uzito na hautarudi tena kwenye uzito mkubwa.

Rafiki, kwa mifano hiyo michache unajionea mwenyewe jinsi mchakato wa siku ulivyo na nguvu kuliko hata malengo ya mwaka.

Ili kukusaidia utumie vizuri nguvu hiyo ya mchakato wa siku, nimekuandalia kitabu kizuri kinachoitwa KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO.
Hiki ni kitabu kinachokuwezesha wewe kujijengea kanuni utakayoifuata kila na itakayokufikisha kwenye mafanikio makubwa.

Kwani mafanikio makubwa kwenye maisha ni mkusanyiko wa siku ambazo mtu umeziishi kwa mafanikio.
Na mafanikio yako kwa mwaka 2022, yatategemea sana jinsi ambavyo umeiishi kila siku ya mwaka huu 2022.

Usikubali tena kuupoteza mwaka huu kama ulivyopoteza miaka ya nyuma.
Pata leo nakala yako ya kitabu cha KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO uanze kuzidhibiti siku zako, ufanye makubwa kwenye kila siku yako na uweze kupata mafanikio makubwa.

Kitabu ni nakala tete (softcopy) na kinatumwa kwa email au unaweza kukipata kwenye app ya SOMA VITABU.

Gharama ya kitabu kwa sasa ni kama zawadi, kwani unachangia tsh 4,500/= tu na unapata maarifa ya kina kabisa kukuwezesha kufanya makubwa mwaka huu na miaka mingine mingi ijayo.

Kukipata kitabu, tuma fedha na email yako kwenda namba 0678 977 007 (Amani Makirita) na kisha utatumiwa kitabu.
Pia unaweza kununua na kusomea moja kwa moja kwenye app ya SOMA VITABU, fungua; http://www.bit.ly/somavitabuapp

Rafiki, huu utakuwa mwaka wako wa kufanya makubwa kama utaweza kuidhibiti kila siku yako na kufanya yale yenye tija.
Hivyo badala ya kuhangaika na malengo makubwa, hebu mwaka huu hangaika na mchakato wa siku na utajionea mwenyewe matokeo yake mazuri.
Pata leo na usome kitabu cha KANUNI YA SIKU YA MAFANIKIO ili kiwe mwongozo mzuri kwako.

Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Muuza Matumaini, Kocha Dr. Makirita Amani.