2953; Fanya machache kufanya makubwa.
Rafiki yangu mpendwa,
Huwa tunadhani ili tuweze kufanya makubwa, basi tunahitaji kufanya mambo mengi sana.
Hilo linapelekea tujihangaishe na mambo mengi na mapya kila wakati.
Lakini cha kushangaza, hata baada ya kuhangaika na mengi, bado matokeo tunayoishia kupata ni ya kawaida sana.
Tunahangaika na mengi, tunachoka sana na mwishowe hakuna tunachoambulia.
Ili tuweze kuzalisha matokeo makubwa, tunachohitaji siyo kufanya mambo mengi.
Bali tunapaswa kufanya machache yaliyo muhimu kabisa na kuyafanya kwa kina.
Unapofanya mengi, unakutana na usumbufu mwingi ambao unapunguza sana ubora wa kile unachofanya.
Unapofanya mengi, unafanya kwa juu juu badala ya kuzama ndani kwa kina.
Unapofanya mengi, unakuwa bize sana, kitu kinachopelekea yale muhimu zaidi yakose nafasi ya kufanyika.
Kuondokana na changamoto hizo, unapaswa kufanya maamuzi ya makusudi kabisa ya kufanya machache ili uweze kufanya makubwa.
Anza kwa kuorodhesha malengo makubwa uliyonayo, kulingana na umuhimu wake. Kisha chagua malengo matatu ya juu na hayo ndiyo unayoyawekea nguvu zako zote kwa sasa.
Kisha orodhesha mambo yote ambayo umekuwa unayafanya kwenye kila siku yako. Weka yote kabisa bila kuacha hata moja.
Sasa basi, oanisha yale unayofanya na mchango wake kwenye malengo makuu matatu. Angalia ni yapi unayofanya ambayo yanachangia kwenye malengo makuu matatu.
Yale tu yenye mchango kwenye malengo makuu matatu uliyochagua kuyawekea umakini ndiyo utapaswa kuendelea kuyafanya kwa sasa.
Mengine yote utapaswa kuacha kuyafanya kwa sasa.
Kwa kupunguza mengi unayofanya, utapata muda zaidi na umakini zaidi wa kuweka kwenye machache uliyochagua.
Bado utapata tamaa ya kuanza mengine mapya utakayoona ni bora zaidi.
Lakini usidanganyike kwa hayo, baki kwenye yale machache uliyochagua kuwa ndiyo muhimu na yafanye kwa kina kabisa.
Hivyo ndivyo mafanikio makubwa yanavyotengenezwa.
Tofauti ya wanaofanikiwa na wanaoshindwa haipo kwenye nini wanachofanya, bali ipo kwenye namna wanavyofanya kile wanachofanya.
Wanaofanikiwa sana wanajua kwa kina kile wanachofanya na wanafanya kwa viwango vya juu sana.
Hilo linawatenga na wengine hivyo kupata fursa nzuri na kubwa.
Wasiofanikiwa wanajua kwa juu juu kile wanachofanya na wanafanya kwa hovyo na mazoea. Hilo linafanya wawe kwenye kundi kubwa la wafanyaki wa kawaida kitu kinachowaweka kwenye ushindani mkubwa.
Kama hakuna kitu ambacho watu wanakipata tofauti kwako, hakuna makubwa unayofanya.
Kama hakuna kitu ambacho watu wanaweza kukipata kwako tu na hakuna pengine wanaweza kupata dunia nzima, watu hawatakuwa na sababu ya kuacha wengine na kuja kwako.
Mara nyingi kukimbilia kufanya mambo mengi ni njia ya kuficha uvivu na uzembe ulio ndani ya mtu.
Mtu anakuwa hayupo tayari kuweka juhudi kubwa zinazohitajika kwenye kitu, kwa kukifanya kwa kina.
Hivyo anakimbilia kufanya mengi yasiyokuwa na tija.
Anachotaka ni aonekane tu yupo bize.
Ingekuwa kuwa ‘bize’ ndiyo kuwa na mafanikio, kila mtu angekuwa tayari ana mafanikio makubwa.
Maana hakuna kipindi ambacho watu wapo ‘bize’ kama sasa.
Lakini matokeo yanajidhihirisha yenyewe, pamoja na watu kuwa bize sana, matokeo hayaridhishi.
Wewe ondoka kwenye huo mkumbo, usikimbilie tu kuwa ‘bize’, badala yake angalia ni hatua zipi za tofauti unazopiga.
Mwanafalsafa Seneca aliwahi kusema tatizo siyo kwamba tuna muda mchache, bali tatizo ni tunao muda mwingi mpaka tunaishia kuutumia vibaya. Na hilo linajidhihirisha na jinsi wengi wanapenda kuwa ‘bize’.
Mahali pengine Seneca pia akasema; siyo kwamba hatufanyi kwa sababu mambo ni magumu, bali mambo ni magumu kwa sababu hatufanyi.
Kuhangaika na mambo mengi mapya ni kuacha kuweka juhudi kubwa kwenye machache muhimu.
Na mwishowe tunalalamika mambo ni magumu, hiyo ni kwa sababu hatufanyi yaliyo muhimu na kwa kina.
Pale unapojikuta unasema upo ‘bize’ na huna muda wa kufanya mambo unayojua ni muhimu, ndiyo wakati wa kufumbuka macho na kupunguza hayo mambo unayofanya.
Mwisho wa siku hautahesabiwa kwa mengi uliyofanya, bali utahesabiwa na makubwa uliyofanya.
Weka kipaumbele chako kwenye makubwa na siyo mengi.
Ukubwa utakupa mengi unayotaka, wakati mengi yakikukosesha ukubwa huo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#BilioneaMafunzoni
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
kipaumbele changu kwenye makubwa na siyo mengi.
LikeLike
Asante sana Kocha, nitachagua machache tu na muhimu na nitafanya makubwa kwenye hayo machache. Sitatawanya nguvu zangu.
LikeLike
Natakiwa kufanya maamuzi ya makusudi kabisa ya kufanya machache kwa umakini ili niweze kufanya makubwa.
Ahsante sana Kocha.
LikeLike
Nitafanya machache kwa viwango vya juu badala ya kuhangaika na mengi kwa juu juu
LikeLike
Asante sana kocha,nitafanya machache muhimu.
LikeLike
Asante sana Kocha. Kipino sio Kwa mengi niliyofanya Bali ni Kwa Yale Bora niliyo yafanya yanayonitofautidha Dunia nizma
LikeLike
Ahsante sana Kocha, nimeona njia pia hata katika hili.
LikeLike
Kweli machache bora dhidi ya mengi ya kawaida.
LikeLike
Chagua machache fanya kea kina , toa thamani kubwa ambayo haipatikani sehemu nyingine, utapata fursa nyingi na kubwa kisha mafanikio makubwa unayostahili.
Asante Kocha kwa kutufundisha na kutukumbusha hili
LikeLike
Asante kocha.Sitahesabiwa kwa mengi niliyofanya bali kwa makubwa niliyofanya.
LikeLike
Asante Koxha. Nitafanya Macha he ili kufanya Makubwa!
LikeLike
Sikimbilii tu kuwa bize,Bali naangalia ni nini cha muhimu na kina matokeo makubwa ninayoweza nikafanya kuliko kuwa bize tu na kufuata mkumbo.
LikeLike
Asante Sana kocha, nitajitahidi kufanya makubwa badala ya kuhangaika na mengi.
LikeLike
Asante sana kocha hakika nitatulia kwenye vichache mpaka nipate vikubwa kuliko kufanya meng
LikeLike
Sitatapanya nguvu zangu kwa kufanya mengi,nitafanya machache kwa ubora wa juu.
LikeLike
Asante nimepata msg nzuri
LikeLike
Kufanya mambo mengi ni kutawanya nguvu. Pale nguvu zinapotawanya ufanisi mkubwa unapungua.
LikeLike
Tuna muda mwingi mpaka tunautumia kufanya Mambo yasiyofaa. Sio kwamba hatufanyi kwa sababu Mambo ni magumu Ila Mambo ni magumu kwansababu hatufanyi by Seneca.
LikeLike
Asante sana kocha kwa somo zuri. Nitalifanyia kazi
LikeLike
Asante kocha,kwa makara.
LikeLike
Kwa kweli hii ni changamoto kwa wengi. Watu wanafanya mengi kwa gharama ya ubora/ufanisi. Hapa nimejifunza kitu kwa ahili ya kuleta ufanisi katika mambo yangu.
LikeLike
Vizuri, fanyia kazi.
LikeLike
Ahsante kocha kwa tafakari hii, ntachagua kufanya machache ili nifanye kwa ubora zaidi
LikeLike
“FOCUS”
LikeLike
Lazima ufanye makubwa na sio madogo
LikeLike
Kabisa,
Maana muda na nguvu ni zile zile utatumia, iwe unafanya makubwa au madogo.
LikeLike