3074; Utekelezaji ni muhimu zaidi.
Rafiki yangu mpendwa,
Kuna watu wanadhani kwamba kinachowazuia wasifanikiwe ni hawajawa na wazo bora kabisa linaloweza kuwapa mafanikio makubwa.
Wengine wengi wanadhani kinachowakwamisha ni hawajapata mtaji kwa ajili ya kuanzisha au kukuza biashara.
Wengine ni ujuzi, koneksheni au kukosa rasilimali muhimu ambazo wanahitaji.
Kuna mengi watu wanaweza kujiambia yanawakwamisha wasifanikiwe, lakini yote siyo sahihi.
Watu wanaofanikiwa huwa wanapata sababu ya kufanikiwa, licha ya mengi wanayokuwa wamekosa.
Na watu wanaoshindwa huwa wanapata sababu ya kushindwa, licha ya mengi wanayokuwa nayo.
Kitu kikubwa sana kinachowakwamisha watu wengi kufanikiwa ni kwenye utekelezaji.
Mawazo ni rahisi sana, kila mtu anayo mazuri.
Ni kutekeleza mawazo hayo ndiyo shida inapoanzia.
Kwenye utekelezaji wa mawazo kuna vikwazo vikuu viwili;
Cha kwanza ni ugumu ambao upo kwenye safari yoyote ya mafanikio.
Wengi huanza vizuri na mawazo wanayokuwa nayo, lakini wanapokutana na ugumu, wanaacha kufanya kwa kuona hayawezekani kabisa.
Cha pili ni usumbufu ambao unatokana na mawazo mengine yanayoweza kuonekana ni mazuri zaidi. Kila wakati kuna mawazo huwa yanakuja ambayo yanaonekana ni mazuri na rahisi kupata mafanikio. Watu wanashawishika kuachana na mawazo waliyokuwa nayo na kwenda kwenye mawazo hayo mapya. Kwa kwenda hivyo wanaishia kuwa wamejaribu mawazo mengi ila hakuna chochote wanachokuwa wamekamilisha.
Mafanikio yanatokana na utekelezaji wa yale ambayo watu wanawaza na kupanga.
Ingekuwa kuwaza peke yake ndiyo kunaleta mafanikio, wengi wangekuwa nayo.
Ingekuwa kupanga ndiyo kunaleta mafanikio, wengi sana wangekuwa nayo.
Lakini vyote hivyo havina mchango mkubwa kwenye mafanikio. Ndiyo maana wengi wanavyo na hawafanikiwi.
Mafanikio makubwa yapo kwenye utekelezaji.
Ni utekelezaji wa tofauti na wa kimsimamo ndiyo unapfanya watu kuweza kuzalisha matokeo tofauti na makubwa, ambayo ndiyo yanaleta mafanikio.
Kinachowapa watu mafanikio siyo kile walichonacho, bali jinsi wanavyotumia hicho walichonacho.
Ndiyo maana watu wawili wanaweza kufanya kazi ya aina moja na wanalipa mshahara unaolingana, lakini mmoja akafanikiwa wakati mwingine akashindwa.
Siyo walichonacho, bali jinsi wanavyokitumia.
Mafanikio ni kutumia vizuri kile ulichonacho ili kuweza kupata kile unachotaka.
Kushindwa ni kusubiri mpaka upate unachotaka.
Uzuri ni kwamba, kila binadamu aliye hai, kuna vitu vingi sana ambavyo anavyo ndani yake.
Mtu akiweza tu kuvitumia vile ambavyo tayari vipo ndani yake, hakuna namna atashindwa kufanikiwa.
Hii safari ya mafanikio hakuna mtu anayeweza kukukwamisha isipokuwa wewe mwenyewe.
Kataa kuwa kikwazo kwako kwa kuwa mtekelezaji mzuri wa yale unayofikiria na kupanga.
Ungepunguza muda unaofikiria kuja na mawazo mapya na kuyapangilia na ukapeleka muda huo kwenye utekelezaji wa wazo lolote ulilonalo, utavuna manufaa makubwa zaidi.
Acha kuhangaika na mawazo,
Acha kuhangaika na mipango,
Acha kuhangaika na uliyokosa,
Anza kuhangaika na utakelezaji.
Tumia vizuri kila ulichonacho sasa ili kuweza kupata yale yote unayoyataka.
Hakuna anayeweza kukuzuia isipokuwa wewe mwenyewe.
Na ufanyaji wenye matokeo siyo ule tu wa kufanya mara moja na kuacha pale matokeo yanapochelewa, bali ni ufanyaji wa msimamo bila kuacha hata kama matokeo ni ya aina gani.
Ukiamua kufanya na ukasema unafanya kweli bila kukwamishwa na chochote, utaweza kufanya makubwa sana.
Usiendelee tena kujizuia kupata matokeo makubwa zaidi ya ambayo unayo sasa.
Nenda hatua ya ziada kwenye utekelezaji na utaweza kufanya makubwa sana.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kwanza tumia kilicho kwako na uanze nacho na uwe unafanya kila mara kwa msimamo bila kuacha tekeleza kile ulichopanga na utayafikia mafanikio yako
LikeLike
Hakika
LikeLike
Utekelezaji ndiyo unakufanya kuwa mtu mpya kabisa, kupanga unabaki pale ulipo.
Asante sana
LikeLike
Karibu
LikeLike
Nakwenda kuwa mtekelezaji mzuri wa kila ninachopanga na kwa msimamo.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ni kweli kocha shida ni kuchukua hatua wengi tunapanga Sana Utekelezaji wa unakuwa zero. Serikalini wa mpango mkakati,upembuzi yakinifu n.k
Lakini wanafeli
LikeLike
Mipango ingekuwa ndiyo mafanikio, kila mtu angekuwa ameshafanikiwa.
LikeLike
Mafanikio ni kutumia vizuri kile ulichonacho ili kuweza kupata kile unachotaka, nitatumia vizuri rasilimali nilizonazo ili kuzifikia ndoto zangu, Asante sana kocha kwa makala hii ambayo kwangu ipo kwenye michakato ya utekelezaji wa moja kwa moja.
LikeLike
Safi sana. TEKELEZA.
LikeLike
Ufanyaji wenye matokeo sio ule tu wa kufanya mara moja na kuacha pale matokeo yanapochelewa bali ni ufanyaji wa msimamo bila kuacha hata kama matokeo ni ya aina gani.
LikeLike
Fanya. Fanya. Fanya.
LikeLike
Mafanikio makubwa yapo kwenye utekelezaji. Naweka malengo na mipango yangu ya kila siku na kila wiki, na kufuata mipango hiyo bila kuacha. Asante sana Kocha
LikeLike
Hapo ndipo penye kila kitu tunachotaka.
LikeLike
Asante Kocha nitapambana kutekeleza yale ambayo yapo mawazo kuliko kuyafikiria tu
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Utekelezaji ndiyo kila kitu kwenye kufikia mafanikio yoyote yale. Asante kocha kwa makala hii.
LikeLike
Karibu sana.
LikeLike
Asante Kocha,
Nimejifunza mafanikio yanatokana na UTEKELEZAJI wa tofauti na wa msimamo wa yale tunayowaza na kupanga kwa kutumia vizuri kile tulichonacho ili kupata kile tunachotaka.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Nitakuwa mtekelezaji makini wa mchakato wa mauzo siku zote
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ukiamua kufanya na ukasema unafanya kweli bila kukwamishwa na chochote, utaweza kufanya makubwa sana.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Mafanikio makubwa yapo kwenye utekelezaji.
Asante sana
LikeLike
Karibu
LikeLike
Nitatekeleza yale niliyopanga kufanya badala ya kuhangaika na mipango mingi.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Mafanikio ni kutumia vizuri kile ulichonacho kupata unachotaka
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Sitaendelea kujikwamisha kwenye kufanya mafanikio makubwa.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Utekelezaji wa yale tunayopanga ndiyo password ya kuingia kwenye mafanikio makubwa.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante kocha,Nitaanza na utekelezaji kwenye mipango yangu na akuna mtu wa kunikwamisha isipokuwa mimi mwenyewe.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Mafanokio makubwa yapo kwenye utekelezaji.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Safari ya mafanikio hakuna mtu anaeweza kukukwamish
a isipokuwa ni wewe mwenyewe.
Asante kocha.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante Kocha,Kinachowapa watu mafanikio siyo kile walichonacho, bali jinsi wanavyotumia hicho walichonacho.✍️
LikeLike
Hakika.
LikeLike
ahsante,
mafanikio sio ulichonacho bali jinsi unavyokitumia.
LikeLike
Kweli kabisa.
LikeLike
Mtapambana kwenye kutekeleza mara zote
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike