3079; Hapana sahihi kwako.
Rafiki yangu mpendwa,
Kama ambavyo tunajua, tupo kwenye msimu wa kusema HAPANA.
Ni msimu wa kupeleka umakini na juhudi zote kwenye vitu vichache na kuachana na vingine vyote.
Watu hudhani kusema hapana ni rahisi sana, kwa sababu vitu unavyokataa ni ambavyo huvitaki.
Lakini hilo siyo sahihi.
Hapana sahihi kwako ni ile inayokuuma kusema.
Hapana unayofurahia kuisema ni ile ambayo inahusisha kitu ambacho hukuwa unakihitaji kabisa.
Na hivyo ni kitu ambacho hakikuwa na madhara kabisa.
Hapana inayoumiza kuisema ni ile ambayo inahusisha kitu ambacho unakipenda na kukikubali sana na pia upo vizuri kwenye kukifanya.
Ni kitu kinachokuuma kuacha kufanya kwa sababu kina fursa ya kufanya makubwa zaidi.
Hapana sahihi kusema, ambayo pia inaumiza kusema ni ile unayosema kwa vitu ambavyo umeshapata mafanikio fulani.
Yaani ni sawa na kuwaua baadhi ya watoto wako ili ubaki na wachache ambao watafany vizuri zaidi.
Hiki ni kitu ambacho wakulima wanakielewa kwa asili.
Wakati wa kutunza mazao yao, huwa wanalazimika kupunguza baadhi ya matawi au matunda yaliyoanza kutokeza ili kubaki na machache yatakayokuwa bora zaidi.
Kwa mtu mgeni kwenye kilimo, akiona matawi mengi yenye maua anaona atapata mazao mengi. Anayatunza yote asipoteze hata moja.
Matokeo yake anapata mazao mengi lakini yaliyo hafifu, yanakuwa madogo na yasiyo na ubora.
Kwa mkulima mzoefu anajua kadiri mche mmoja unavyokuwa na maua mengi, ndivyo mazao yanayozalishwa yanavyokuwa hafifu.
Hivyo hupunguza matawi hayo haraka sana ili kubakiza machache ambayo yatazalisha mazao bora sana.
Tukifananisha na masomo, ni sawa na mwanafunzi anayechukua masomo matano na kupata wastani wa B kwenye masomo yote, huo ni ufaulu mzuri.
Lakini ukilinganisha na mwanafunzi mwingine anayechukua masomo mawili na kupata wastani wa A kwenye masomo yote, huo ni ufaulu bora zaidi.
Mambo yote yanayokuwa rahisi kufanya ni ambayo hayana mchango kwenye mafanikio yako makubwa.
Na mambo yote yanayokuwa magumu kufanya ndiyo yenye fursa ya kukupa mafanikio makubwa.
Ili upate mafanikio makubwa, lazima uwe tayari kutoa kafara vitu ambavyo umekuwa unavifanya vizuri na hata kuvipenda, ili kukusanya nguvu zako kwa vitu vilivyo bora zaidi.
Ni bora kuchimba kisima kimoja kwa urefu mkubwa zaidi kuliko kuchimba visima vingi kwa urefu mdogo.
Nguvu zile zile unazotawanya kwenye mashimo mengi, ndizo ambazo ukizikusanya kwenye shimo moja litakuwa refu sana na hivyo kukupa matokeo makubwa.
Kitu kinavyokuwa kigumu kwako usikikimbie, kina ugumu kwa sababu ndani yake kina fursa kubwa.
Kutokana na ugumu wake, kila mtu anakimbia kukifanya.
Hivyo basi, ukikifanya wewe, unakuwa mbele zaidi ya wengine na hivyo kupata manufaa makubwa.
Kagua vitu vyote unavyovifanya kwa muda wako na ona ni wapi unapotawanya nguvu ambazo ungezikusanya zingezalisha matokeo makubwa na bora zaidi.
Hili ni zoezi la kufanya mara kwa mara kwa sababu huwa ni rahisi sana kujisahau na kutoka kwenye mchakato mkuu unaokuwa nao.
Moja ya kazi kubwa kwenye safari yako ya mafanikio ni kujirudisha kwenye njia kuu. Kabla hujaongeza kasi kwenye yale unayofanya, ni muhimu sana kuhakikisha ni sahihi kuyafanya.
Sema HAPANA kwenye mambo mazuri kwako kufanya ili uweze kusema NDIYO kwenye mambo ambayo ni bora zaidi kwako kuyafanya.
Na kama HAPANA zako hazikuumi wewe binafsi, jua hizo siyo hapana sahihi kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Hapana sahihi kwako ni zile zinazokuuma.
LikeLike
Kabisa, kama haiumi siyo sahihi.
LikeLike
Kweli kocha asante kutukumbusha hili la kujirudisha njia kuu mara Kwa mara na kusema hapana inayokuuma.
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Asante kocha nitaendelea kusoma hapana
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante sana Kocha kwa msimu wa hapana, ni kweli tunatawanya nguvu zetu kwenye mambo yasiyo sahihi
LikeLike
Karibu
LikeLike
Asante kocha,
Msimu wa hapana ili kukusanya nguvu
Na kufanya yale muhimu.
LikeLike
Kaa humo.
LikeLike
Nitasema hapana kwenye mambo rahisi ambayo hayana mchango katika mafanikio yangu
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Msimu wa HAPANA, naendelea kuonekana wa tofauti kwenye baadhi ya mambo au watu,hasa baada ya kufungua biashara maana mda wangu mwingi naupeleka huko,na sitaacha, hivyo nitaendelea kusema HAPANA kadri niwezavyo .
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Kwa hakika neno hili hapana limeshaniondolea wanyonyaji wengi wa nguvu na rasilimali fedha zangu, na wala sijali japo nilikuwa nmezoea kuwa nao kwa muda mrefu.
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Hapana inayoumiza kuisema ni ile ambayo inahusisha kitu ambacho unakipenda na kukikubali sana na pia upo vizuri kwenye kukifanya.
Ni kitu kinachokuuma kuacha kufanya kwa sababu kina fursa ya kufanya makubwa zaidi.
Asante sana
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Asante kocha,Nitajitahidi kila siku kuweka nguvu na umakini kwa vitu vichache kuliko kutawanya nguvu kwenye vitu vingi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nasema hapana itakayoniuma ili kuweka nguvu na umakini wangu kwa yale machache yatakayonipa matikeo makubwa.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Hapana zinauma, Lakini Hapana ndio zinazotuwezesha kufanya mambo makubwa.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Hakika kusema HAPANA na kuacha kutawanya nguvu kutaketa matokeo Bora na Chanya zaidi. Unajua katika Hali ya kawaida kila kitu natamani kufanya na kuona Ni fursa lkn ukianza kufanya na kukutana na changamoto unagundua umepoteza muda, nguvu na fedha.
Hapana HAPANA HAPANA HAPANA HAPANA
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hapana sahihi ni ile inayouma kuisema. Kama hapana hainiumizi, basi hiyo siyo hapana sahihi kwangu
LikeLike
Kweli.
LikeLike
Kama Hapana yako hikuumi wewe binafsi, basi jua hiyo si hapana sahihi kwako
Nitasema HAPANA kwenye mambo mazuri kwangu kufanya ili niseme NDIYO kwenye mambo ambayo ni bora zaidi kwangu kuyafanya.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Unatakiwa kusema HAPANA inayokuumiza. Kama haikuumizi jua hiyo siyo HAPANA sahihi kwako.
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kitu kinavyokuwa kigumu kwako usikikimbie pambana nacho mpaka ufanikiwe.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Hapana sahihi inapaswa ikuumize haswa,uonekane ni katili
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hapana sahihi inapaswa ikuumize haswa
LikeLike
Ni kweli hapana isiyouma siyo sahihi na kwa upande wangu nimeanza kufanyia kazi japp ona hitaji uamue kufumba macho kabisa na kusema hapana kubwa na ukweli ukiamulia sehemu moja unatoboa na sasa na mimi nimeamua kutoboa shimo moja tu nyinginenazifukia na kuongeza nguvu kwa shimo hili najua kweli hili ji kama imekuja ajili ya mabadiliko yangu
LikeLike
Vizuri, endelea na mkakati huu.
LikeLike
Mambo yote yanayokuwa rahisi ni yale ambayo hayana mafanikio makubwa kwenye maisha yako
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Ili kupata mafanikio ya uhakika, lazima utoe kafara
Vitu ambayo umekuwa unamfanya vizuri pia unavyovi
Penda ili kukusanya nguvu zako kwa vitu vilivyo Bora.
Asante kocha
LikeLike
Hakika
LikeLike
Hapana sahihi kwangu ni kwenye yale ninayopenda kuyafanya .Ni bora kuchimba shimo moja refu kuliko kutawanya nguvu zangu kuchimba mashimo mafupi mengi.
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Hapana kwenye mambo mazuri lakini kwasasa yanahitaji kusubiri kwanza
LikeLike
Kabisa
LikeLike
Kagua vitu vyote unavyovifanya kwa muda wako na ona ni wapi unapotawanya nguvu ambazo ungezikusanya zingezalisha matokeo makubwa na bora zaidi
LikeLike
Kabisa
LikeLike