3101; Kushindwa mbele na nyuma.
Rafiki yangu mpendwa,
Watu wengi huwa wanaona kushindwa ni kushindwa tu.
Pale wanapopanga kufanya au kupata kitu fulani na wasikipate, hapo ndiyo wanaona wameshindwa.
Lakini hilo siyo sahihi,
Kushindwa huwa hakufanani.
Kwa uhakika ni kuna aina mbili za kushindwa, ambazo ni kushindwa mbele na nyuma.
Kushindwa nyuma ni kule ambapo kunasababishwa na uzembe. Hapo mtu anakuwa anajua anachopaswa kufanya, lakini hakifanyi.
Mambo mbalimbali yanamzuia mtu asichukue hatua kabisa.
Kwa kutokufanya, mtu anashindwa vibaya mno.
Kushindwa mbele ni pale ambapo mtu anakuwa amechukua hatua kubwa na za tofauti na vile alivyozoea.
Kwa kufanya mambo mapya na makubwa, hata kama hutapata matokeo uliyotegemea, unakuwa umepiga hatua kuelekea kwenye mafanikio unayoyataka.
Kushindwa nyuma ni kujirudisha nyuma na kwenda mbali zaidi na mafanikio unayokuwa unayataka.
Kushindwa mbele ni kujisogeza karibu na mafanikio ambayo umeyapanga.
Maisha huwa yanaendelea kuwa bora kadiri unavyokuwa unaendelea kuyafanyia kazi.
Kadiri unavyoendelea kuchukua hatua mpya na kubwa ndivyo unavyojiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kupata unachotaka.
Maisha huwa yanakuwa hovyo pale ambapo hakuna hatua mpya, kubwa na za tofauti zinazochukuliwa.
Pale mtu anapopanga lakini asichukue hatua ni tatizo.
Na pale mtu anapoacha kuchukua hatua mpya baada ya kupata matokeo fulani mazuri pia ni tatizo.
Ni kawaida yetu binadamu kulinda kile ambacho tayari kimeshapatikana.
Lakini inapokuja kwenye safari ya mafanikio makubwa, mashambulizi ni muhimu kuliko kulinda.
Kuendelea mbele hata baada ya kupata ushindi fulani ni hitaji muhimu sana kwenye safari hiyo ya mafanikio.
Mafanikio mara zote huwa yapo kwenye mwendo.
Hata kwenye asili, maji yanayotiririka ni bora kuliko maji yaliyotuama.
Kaa kwenye mchakato na ushindwe kwa kufanya kuliko ushindwe kwa uzembe.
Jisukume mpaka ukamue tone la mwisho la uhai wako kwenye kufanya.
Na hata kama utashindwa, kitu ambacho ni kwa muda mfupi tu, utakuwa umejifunza mengi, hivyo utakarudia tena kufanya, haitakuwa kama ndiyo unaanza, badala yake utatumia uzoefu ambao tayari ulishaupata na kuepuka makosa ya nyuma.
Sasa hebu fikiria mtu anayejisukuma kuwa bora kwa kujaribu vitu vipya na vikubwa kila mara bila kuchoka hata kama matokeo siyo mazuri.
Kitendo cha kuwa tayari kuendelea kufanya bila ya kujali matokeo yanayopatikana, ni uhakika wa mafanikio.
Shindwa kwa kufanya makubwa na kupata matokeo madogo kuliko kushindwa kwa kutokufanya kabisa.
Unaweza kuboresha kitu ambacho kimeshaanza kufanyika, huwezi kuboresha kitu ambacho hakijafanyika kabisa.
Fanya vitu vipya, vikubwa na vya tofauti kila siku bila kuacha,
Matokeo utakayoyapata ni makubwa sana.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Nitafanya vitu vya tofauti kila siku ili kuhakikisha kuwa naweka juhudi kubwa kwenye biashara yangu
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Shindwa kwa kufanya makubwa na kupata matokeo madogo kuliko kushindwa kwa kutokufanya kabisa.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Hakika kocha
Kinachoboreshwa ni kile kinachoendelea kufanyiwa Kaz
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante kocha nitaendelea kufanya makubwa hata nikishindwa nitakuwa nimeusogelea ushindi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Shindwa kwa kufanya na sio kutofanya kabisa
LikeLike
Hakika
LikeLike
Huwezi kuboresha kile ambacho hakijafanyika.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Huwezi kuboresha kitu ambacho hakipo. Kwa kufanya utaweza kupata kitu cha kuboresha.
Kukaa kwenye mchakato ndiyo asili ya dunia.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asante kocha nimejifunza kitu kipya hapa kwamba nikawaida yetu Sisi binadamu kulinda kile tulichonacho kwa kweli mimi ni mmoja wapo kuna wakati nashindwa kurudisha fedha kwenye biashara kwasababu yakuogopa ugumu wa kuuza naamua nibaki na hela Kwa hiyo nimejifunza bora kushambulia kuliko kulinda
LikeLike
Shambulia.
LikeLike
Unaweza kuboresha kitu ambacho kimeshafanyika lakini kitu ambacho hakijafanyika huwezi kukiboresha. Nitajitahidi kuwa mtu wa kufanya vitu vya tofauti ili niweze kuboresha kutoka hapo. Asante sana kocha
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Asante kocha,Nitajitahidi kufanya vitu vipya,na vikubwa kila siku bila kuacha.ni kwenda mbele tu.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante Kocha,
Mafanikio mara zote yako kwenye mwendo.
Nitakaa kwenye mchakato nishindwe kwa kufanya kuliko kushindwa kwa uzembe.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Natakiwa nifanye yale niliyopanga kufanya kwa sbabu nitakuwa nanafasi ya kufanya kwa Mara nyingine kwa ubora, kwani kama sitofanya chochote nitakuwa Sina cha kuboresha. Asante sana kocha.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Maisha huwa yanaendelea kuwa bora kadiri unavyokuwa unaendelea kuyafanyia kazi.
Kadiri unavyoendelea kuchukua hatua mpya na kubwa ndivyo unavyojiweka kwenye nafasi nzuri zaidi ya kupata unachotaka.
Asante sana
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Mashambulizi ni muhimu kuliko kulinda goli.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante sana naendelea mbele
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nukuu nzuri Sana hii
‘Shindwa kwa kufanya makubwa na kupata matokeo madogo kuliko kushindwa kwa kutokufanya kabisa.
Unaweza kuboresha kitu ambacho kimeshaanza kufanyika, huwezi kuboresha kitu ambacho hakijafanyika kabisa.
NITAKAA HUMO
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Kila siku nitachukua hatua kuelekea mafanikio yangu bila kujali matokeo ninayopata.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Huwezi kuboresha kile ambacho hujafanya na pia kujaribu siyo kushindwa kushindwa ni pale utakapoacha kufanya jambo kwa kuogopa
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Shindwa kwa kufanya makubwa na kupata matokeo madogo kuliko kushindwa kwa kutokufanya kabisa.
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Mafanikio Mara zote huwa yapo kwenye mwendo,
Mimi nitaendelea kukaa kwenye mchakato. bora nishindwe kwa kufanya kuliko kushindwa kwa uzembe.
Asante kocha
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Shindwa kwa kufanya makubwa na kupata matokeo madogo kuliko kushindwa kwa kutokufanya kabisa.✍️
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Shindwa kwa kufanya makubwa na kupata matokeo madogo kuliko kushindwa kwa kutokufanya kabisa.
Unaweza kuboresha kitu ambacho kimeshaanza kufanyika, huwezi kuboresha kitu ambacho hakijafanyika kabisa.
LikeLike
Kweli
LikeLike