3136; Ukatili wa asili.
Rafiki yangu mpendwa,
Asili huwa inafanya maamuzi yake kwa namna yake yenyewe.
Maamuzi yanayofanywa na asili huwa hayaangalii matakwa ya watu.
Kama asili ingekuwa ni mtu kwenye hayo maeneo yote yanayofanyiwa maamuzi, angeonekana kuwa mtu mwenye roho mbaya sana na asiyejali.
Hiyo ni kwa sababu watu watakuwa na maelezo mengi na mazuri ambayo wanajua yatamnasa mtu akubali, lakini asili huwa haifanyi mambo yake kwa kuangalia watu wanataka au wanafikiria nini.
Ili kuelewa zaidi fikiria mifano hiyo hapo chini.
1. Panda juu ya mti mrefu au jengo refu kisha jiachie uelee hewani kama ambavyo ndege huwa wanafanya, kisha upime matokeo yake. Utaishia kuwa na anguko kubwa na litakalokuumiza sana. Hata kama wewe ungejali kiasi gani, asili haijali, kuna nguvu ya mvutano ambayo inavuta vitu vyote kwenda chini, bila ya kujali ni kitu au mtu gani.
2. Misitu huwa inashika moto mara kwa mara na kuunguza mimea na viumbe wengine wengi. Hii ni njia ya asili ya kusafisha mazingira yake pale yanapokuwa hayajasafishwa kwa muda mrefu.
Moto unaowaka kwenye misiti hiyo unaweza kuwa na madhara makubwa, lakini asili haijali, inakuwa inahitaji zaidi kujisafisha.
3. Ukiwaangalia wanyama simba na swala unapata picha ya jinsi ukatili wa asili ulivyo dhahiri.
Simba huwa wanawala swala, ni chakula muhimu kwao.
Unapoona simba wengi wakiwa hai, maana yake hapo ni swala wengi wamegeuzwa kuwa chakula kwa simba hao.
Kadhalika unapowaona swala wengi wakiwa hai, kuna simba ambao hawajapata chakula.
Haijalishi swala atatamani kiasi gani kuishi, simba anapotokea kitakachomwokoa ni mbio zake.
Pale simba anapokuwa anamkimbiza swala, kila mmoja anakimbia kwa ajili ya uhai wake. Simba anamkimbiza swala ili kupata chakula, wakati swala akimkimbia simba ili kunusuru maisha yake.
Kwa mifano hiyo michache, tumejionea dhahiri jinsi asili inavyofanya mambo yake bila kujali.
Asili inafanya kile kilicho sahihi kwa wakati sahihi, bila kujali kama watu wanataka au hawataki.
Hivyo pia ndivyo unavyopaswa kufanya kama unataka kujenga na kutunza mafanikio makubwa kwenye maisha yako.
Mara zote fanya kile kilicho sahihi.
Kwa muda mfupi kuna fursa unaweza kuzipoteza kwa kusimamia yale yaliyo sahihi, lakini utapata fursa nyingine kubwa na nyingi baadaye kwa kusimamia yaliyo sahihi.
Nyooka kama asili ilivyonyooka na utajiepusha na changamoto nyingi ambazo watu huwa wanazitengeneza pale wanapofanya maamuzi kwa kutumia hisia badala ya fikra.
Binadamu tunajua kudanganyana kwa kutumia hisia, ila asili huwa haidanganyiki kwa hisia zetu.
Unapotaka mambo makubwa na muhimu yafanyike, unajua wazi kwamba lazima ufanye kile kilicho sahihi mara zote.
Huwa kunakuwa na mwingiliano mwingi unaogusa hisia katika maamuzi hayo, lakini wajibu wetu ni kuvuka hisia hizo ili kufanya maamuzi sahihi.
Unapoamua kunyooka kama asili ilivyonyooka, unapoamua kufanya yaliyo sahihi mara zote bila kujali watu wanataka au kujisikiaje, utaonekana kama mtu mwenye roho mbaya sana.
Kama haupo tayari kuchukuliwa kama mtu mbaya na mwenye roho mbaya, tayari unakuwa umepishana na mafanikio makubwa.
Kama unataka kupata mafanikio makubwa, halafu pia hutaki kuonekana una roho mbaya, tayari unakuwa umeshashindwa.
Mafanikio makubwa huwa hayaendani na matakwa ya walio wengi.
Kwa sababu wengi ni wavivu na wazembe na huwa wana sababu na visingizio vingi kwenye kila jambo.
Ukisikiliza na kupokea sababu na visingizio hivyo, hakuna hatua yoyote kubwa utakayoweza kupiga.
Chagua kwenda kama asili inavyoenda, nyooka kwenye mambo yako yote, hakikisha maamuzi unayofanya hayaathiriwi na hisia zako binafsi.
Kwa kwenda hivyo utaweza kufanya makubwa sana, lakini inahitaji ngozi ngumu ya kuvumilia maneno mengi mabaya yatakayosemwa kuhusu wewe.
Asili inaendelea kufanya mambo yake wakati wote bila kujali tunaichukuliaje.
Hivyo ndivyo tunavyopaswa kuwa pia.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Ndio, nahitaji kuhakikisha nanyooka kama asili, japo watu wanaweza wasinipende lakini angalau wataniheshimu.
LikeLike
Na hilo la kuheshimiwa ni muhimu kuliko kupendwa.
LikeLike
Asante Kocha. Mara zote nitafanya kile kilicho sahihi.
Kwa muda mfupi kuna fursa ninaweza kuzipoteza kwa kusimamia yale yaliyo sahihi, lakini nitapata fursa nyingine kubwa na nyingi baadaye kwa kusimamia yaliyo sahihi.
Nitanyooka kwenye mambo yote kama asili.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nimechagua kufanya mambo yangu kwa kunyooka na kwa msimamo kama asali inavyofanya mambo yake ,sitajali wengine wanasemaje au kunichukuliaje kikubwa nafanya yaliyo sahihi mara zote atakaependa apende na atakae chukia achukie tu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asili, Haina huruma wala hijali. Ni jukumu langu Kufanya kile kilichokuwa sahihi kwangu na Kwa asili. Asante kocha.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ujanja ni kunyooka tuu, hatuwezi kupendwa na Kila mtu lakini hiyo ndiyo njia ya kufikia mafanikio makubwa na kupiga hatua.
Nachagua kunyooka kama asili bila kusukumwa na hisia
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha nikweli mahitaji kunyooka kama asili
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Mafanikio makubwa yanaletwa na kutokujali mtu anakuonaje wewe fanya kile sahihi na yenye tija kwako na utaona jinsi ambavyo asili itakuwa pamoja na wewe nenda kama asili inavyoenda haitumii hisia kama sisis
LikeLike
Kabisa
LikeLike
katika safari ya ubilionea tunapaswa kuishi kama asili inavyoenda, kwa kunyooka kwenye mambo yetu yote na kuhakikisha maamuzi tunayofanya hayaathiriwi na hisia zetu binafsi.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Nitajitahidi kufanya kama asili inavyofanya kwa kufanya yale yaliyosahihi kwangu bila kujali wengine wanasema nini juu yangu. Asante sana kocha
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Siku zote ni kunyooka tu ili kukaa sawa na kuepuka lawama
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Kama asili inavyofanya ,nitafanya mambo sahihi bila kuangalia watu wananichukuliaje
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asili huwa inatusaidia kuweka mambo mengi sawa. Yale ambayo kwetu tunaona hayawezekani lakini asili inatusaidia kuweka kila kitu sawa bila upendeleo.
Asante sana
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ishi kulingana na asili na utakuwa na maisha Bora fanya kilicho sahihi mara zote na usiangalie watu we fanya kiicho sahihi
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitajitahidi kunyooka kama ilivyo asili,acha watu wasinipende,walalamike na kulaumu mi sitajali,n kweli hadi sasa napata lawama.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante kwa ujumbe huu mzuri.
LikeLike
Karibu
LikeLike
Mara zote ninapaswa kufanya sahihi bila kujali wengine wanachukuliaje.
Asante kocha.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Ahsante sana kocha, asili haijali mimi nataka au sitaki itamipe kile ninachostahili bila kujali matakwa yangu
LikeLike
Hakika
LikeLike
Asante kocha,Nitafanya kama asili inavyotaka,na nitafanya mambo yangu kwa kunyooka tu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asili inafanya kile kilicho sahihi kwa wakati sahihi.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Asili huwa unaendelea kufanya mambo yake wakati wote bila kujali tunaichukuliaje. Hivyo ndivyo Nina Topas wa
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Nahakikisha nanyooka kwenye mambo yangu. Asante Kocha.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Asante sana ninelichukua kama lilivyo
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Mafanikio makubwa huwa huwa hayaendani Na matakwa ya waliowengi
LikeLike
Hakika
LikeLike
Nitanyooka kama asili ilivyonyooka ili kupata mafanikio makubwa.
LikeLike
Vizuri
LikeLike