3157; Akili na Kipaji.
Rafiki yangu mpendwa,
Hapa nina habari nzuri na mbaya kwako.
Na tutaanza na habari mbaya.
Habari mbaya ni kwamba ili upate mafanikio makubwa unahitaji kuwa na akili kubwa na kipaji cha kipekee.
Na ubaya wa habari hiyo ni kwamba hivyo ni vitu viwili ambavyo huwezi kuvibadili.
Huwezi kujiongeza akili wala kujipa kipaji.
Hizo ni habari mbaya na za kusikitisha, kwamba kuna vikwazo unavyoweza kuwa navyo ambavyo vinakuzuia usifanikiwe.
Sasa ni wakati wa kwenda kwenye habari nzuri.
Na habari hizo nzuri ni kwamba kuna vitu unaweza kufanya na ukahakikisha akili na kipaji haviwi kikwazo kwako.
Vitu hivyo vipo ndani ya uwezo wako kabisa kuvifanyia kazi.
Kwa kuchukua hatua kwenye maeneo hayo mawili makuu, inakupa uhakika wa kujenga mafanikio makubwa.
Moja; kama huna akili nyingi, kuwa na shauku kubwa.
“Being enthusiastic is worth 25 IQ points.” –Kevin Kelly
Kevin Kelly alinukuliwa akisema kuwa na shauku ni sawa na alama 25 za akili.
Hiyo ina maana kwamba mtu ukiwa na shauku kubwa, inaondoa kikwazo cha akili kwenye mafanikio.
Unapokuwa na shauku kubwa, unakuwa na nguvu ya kuwashawishi wengine kukubaliana na wewe.
Na uwezo wako wa kuwashawishi watu wengine ndiyo akili muhimu kwa mafanikio.
Mbili; kama huna kipaji, amka mapema.
“I don’t have talent, so I just get up earlier.” – Henry Rollins
Henry Rollins alisema yeye hana kipaji, hivyo huwa anaamka mapema.
Wale wenye vipaji huwa wanafanya mambo kwa urahisi kuliko wasiokuwa na kipaji.
Lakini wasiokuwa na kipaji wakiweza kuweka juhudi kubwa, wanaweza kupata matokeo makubwa kuliko hata wenye vipaji.
Lakini hilo linahitaji sana mtu kuweka kazi kubwa na kwa muda mrefu.
Kwa kuamka mapema na kuweka juhudi za kipekee, utaweza kufanya makubwa kuliko hata wale ambao wana vipaji vikubwa.
Nidhamu kali ya kufanya bila kuacha inakuwezesha kufidia palipopelea kwa kipaji.
Rafiki, tumeona jinsi ambavyo akili na kipaji ni mahitaji muhimu kwenye mafanikio.
Lakini pia tumeona jinsi ya kuhakikisha vitu hivyo viwili haviwi kikwazo kwako kufanikiwa.
Kwa kuwa na shauku kubwa ambayo inakuvusha kwenye akili na kuamka mapema ambako kunakuvusha kwenye kipaji.
Sasa basi, hebu fikiria ukiwa na akili halafu pia ukawa na shauku kubwa, utakuwa wa moto sana.
Kadhalika fikiria una kipaji halafu pia ukawa unaamka mapema na kuweka juhudi kubwa, utafanya makubwa mno.
Amua kufanyia kazi maeneo hayo mawili, iwe unajiona una akili na kipaji au la.
Mara zote juwa na shauku kubwa huku pia ukiamka mapema na kuweka juhudi kubwa.
Lazima utaweza kufanya makubwa sana.
Huwa hatupo vizuri kwenye kujikadiria, hivyo ni vyema kuchukua hatua sahihi iwe tuna sifa au hatuna.
Unapofanya yale yaliyo ndani ya uwezo wako, unajiweka kwenye nafasi ya kupata matokeo bora kabisa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Asante sana kocha.
LikeLike
Karibu
LikeLike
Kweli kuweka kazi kubwa kunakosukumwa na shauku kubwa nyuma yake mara nyingi kunazidi hata kipaji.
Ndio maana Thomas Edison anasema, “Genius is 1% inspirational 99% perspiration”.
Nilikuwa naamini kwamba mtu kuwa na mafanikio makubwa sana au kuwa bilionea kunahusisha kuwa na akili sana, hata hivyo hiyo ni “added advantage”, inabidi u-take advantage of that, kama uko nayo.
Mchanganyiko wa juhudi akili kubwa sana na kipaji ndio unaishia kuws Elon Musk, Bill Gates, Mengi etc.
LikeLike
Umefafanua vyema.
Tutumie vyote ili kupata matokeo bora kabisa.
LikeLike
Tunapaswa kuamka mapema na kufanya kwa bidii huku tukiwa na shauku kubwa na tena tufanye kwa kurudiarudia bila kuacha
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Ni vyema nichukie hatua sahihi iwe nina sifa au Sina.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Asante sana kocha, nitaendelea kufanya yaliyo ndani yangu kwa kuwa na shauku kubwa
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Nitajitahidi kuwa na shauku kubwa na kuamka mapema maana haya yapo kwenye uwezo wangu. Asante sana kocha
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kwa kuamka mapema na kuweka juhudi za kipekee, utaweza kufanya makubwa kuliko wale wenye kipaji
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Asante kocha,Nitafanya yale yaliyondani ya uwezo wangu na nitakuwa kwenye njia ya kupata mafanikio nikianza na shauku na kuamka mapema.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Ahsante sana kocha, nitaamka mapema, nitakuwa na shauku na kuweka juhudi katika kufanya na kutekeleza mipango ninayoiweka
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Haijalishi nikoje,lakini nikikomaa na hivi viwili Shauku kubwa pamoja na kuamka mapema ni vitu viko ndani ya uwezo wangu kuvifanya na vikaniletea matokeo makubwa.
LikeLike
Komaa navyo kwa uhakika.
LikeLike
Asante sana kocha inatubidi tufanye vyote kwa pamoja ili tupate matokeo Bora
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Akili,kipaji shauku na kuamka mapema ukitumie vizuri na Kwa msimamo tunapapata hakika tunapata mafanikio makubwa
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Nidhamu Kali na shauku kubwa unakuwa karibu na mafanikio.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Kama huna akili kubwa basi kuwa na shauku kubwa,
Na kama huna kipaji basi amka mapema.
Kipaji na shauku kubwa ni moto wa kuotea mbali.
LikeLike
Kabisa.
LikeLike
Akili، kipaji ، shauku، kuamuka mapema vyote ni muhimu kwa mafanikio
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
KIPAJI NA AKILI
Sina akili nitakuwa na shauku kubwa na Sina KIPAJI nitakuwa naamka mapema na kufanya makubwa
LikeLike
Tukae humom
LikeLike
Nitakuwa na shauku kubwa na kuamka mapema ili nipate mafanikio makubwa.
LikeLike
Vizuri, kila la kheri.
LikeLike
Kwa kuamka mapema na kuweka juhudi za kipekee utaweza kufanya makubwa kuliko wenye vipaji.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Amua kufanyia kazi maeneo hayo mawili, iwe unajiona una akili na kipaji au la.
Mara zote juwa na shauku kubwa huku pia ukiamka mapema na kuweka juhudi kubwa.
Lazima utaweza kufanya makubwa sana.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Sina hakika na Akili ila kipaji ninacho, nitaweka nidhamu kwenye kuamka mapema na shauku kubwa Sana nipate mafanikio
LikeLike
Vizuri, chukua hatua.
LikeLike
Kweli kocha akili,kpaji, shauku kubwa ,kuamka mapema na kuwa na nidhamu Kali , pamoja na kufanya mara nyingi Kwa kurudiarudia ni uhakika wa kufanikiwa bila Shaka yoyote
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Nitaweka juhudi kubwa ili niweze kufanikiwa Na nitahakikisha naamka mapema ili niikuze akili yangu
LikeLike
Vizuri
LikeLike