3195; Kuwa mchezaji hatari kwenye mashindano.
Rafiki yangu mpendwa,
Kama tukiyachukulia maisha kama mchezo na wewe kama mchezaji, unaweza kuwa mchezaji hatari sana kwenye hayo mashindano.
Utakuwa na hatari pale unapokuwa unaanzia chini kabisa na huna chochote cha kupoteza.
Kwenye mashindano ya aina yoyote ile ni wachezaji wanaoanzia chini kabisa na hawana cha kupoteza ndiyo huwa wanaleta matokeo ya kushangaza.
Mtu ambaye tayari yupo chini, hana hofu ya kuanguka, kwa sababu hana pangine pa kwenda isipokuwa juu.
Kwa kuwa anaanzia chini kabisa, uelekeo pekee anaokuwa nao ni wa kwenda juu.
Mtu huyo anakuwa hana chochote cha kulinda na hivyo umakini wake wote unakuwa kwenye kitu kimoja tu, kwenda juu.
Hiyo ndiyo inawafanya wawe washindani hatari na wenye nyenzo kubwa ya kupata ushindi.
Hofu ya kushindwa au kuanguka ni kikwazo kikubwa sana kwa walio wengi kupiga hatua kwenye maisha yao.
Kugawa umakini wako kati ya kushinda na kuepuka kushindwa kunafanya umakini huo kupungua.
Ni pale umakini wako wote unapokuwa kwenye kitu kimoja ndiyo unakuwa na nguvu ya kuleta matokeo makubwa.
Kama ambavyo jua likitawanyika linamulika, lakini likikusanywa mahali pamoja linachoma moto.
Steve Jobs alikuwa na kauli yake; baki na njaa, bali mjinga (stay hungry, stay foolish). Nadhani unajua jinsi ukiwa na njaa unavyohangaika ili kupata chakula, mbele ya njaa hakuna hofu wala aibu yoyote, utafanya kila uwezalo ili tu uweze kupata chakula.
Lakini ukishashiba, unapunguza makali, unaanza kuwa na ustaarabu mwingi ambao unapelekea ukose yale unayotaka.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye safari yoyote ya mafanikio makubwa.
Mtu anapoanzia chini kabisa anakuwa ni mwenye njaa kali hivyo anapambana hasa kupata shibe, hasikilizi wala kuhofia kingine chochote. Na hilo ndilo linamfanya awe mshindani hatari na anayepata matokeo makubwa na ya tofauti.
Ni pale mtu anapoanza kupanda ngazi za mafanikio ndiyo njaa yake ya mafanikio inapungua na hivyo kasi yake ya ukuaji kupungua kitu kinachopunguza hatari yake.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye kujifunza, wengi wanaoanzia chini kabisa wanakuwa tayari kujifunza mengi ili kutoka kwenye hali hizo.
Ni pale wanapoanza kupiga hatua ndiyo wanaona hawahitaji tena kujifunza kwani wameshajua kila kitu.
Na hilo linapunguza makali ya ukuaji wao, kitu kinachofanya wapate matokeo ya kawaida.
Unapokuwa unaanzia sifuri kabisa, huo msukumo mkubwa tayari unakuwa ndani yako, ni wewe tu uufanyie kazi kwa ukubwa bila kujizuia.
Lakini unapoanza kupiga hatua ndiyo unahitaji kujilazimisha kubaki chini kifikra ili ule msukumo mkubwa unaokuwa nao usiondoke.
Uendelee kupata msukumo ambao unakupeleka kwenye matokeo makubwa kuliko ambavyo umewahi kupata.
Hata kama umeshiba, jione bado una njaa na tafuta chakula zaidi bila ya kujali wengine wanasema nini juu yako.
Hata kama tayari vitu unavijua, jichukulie hujui kitu na jifunze tena. Kama kuna kitabu umeshasoma chukulia hujakisoma na kisome tena. Kwa kufanya hivyo kuna mengi utakayojifunza ambayo hukuyapata ukiposoma kitabu hicho kwa mara ya kwanza.
Ukiweza kubaki na mtazamo huo wa chini na wa kupambana mara zote bila kuwa na hali ya kuridhika na kulinda ambayo umeshayapata, hakuna kinachoweza kukuzuia kupanda ngazi za juu zaidi ya pale ulipo sasa.
Acha kulinda hapo ulipo sasa, hilo linakushikilia usipige hatua.
Acha kuhalalisha hapo ulipo sasa, bado ni chini sana ukilinganisha na unakopaswa kuwa.
Mara zote kuwa na njaa kali ya kutaka mafanikio makubwa zaidi na kuwa mjinga wa kujifunza na kuchukua hatua.
Nguvu kubwa ya kupata mafanikio yoyote makubwa unayoyataka tayari ipo ndani yako.
Unachohitaji ni kuiamsha na kuitumia.
Hali unazokuwa nazo zinaweza kuamsha uwezo huo kwa kiasi.
Lakini unapouamsha makusudi, utaweza kuutumia kufanya makubwa zaidi.
Baki na njaa na baki mjinga maisha yako yote, utakuwa mchezaji hatari sana kwenye haya mashindano ya maisha.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Kila wakati unapaswa kuwa mchezaji hatari anayetaka kushinda. Na kushambulia kwenye mchezo wetu ndiyo kukaa kwenye mchakato wa kujifunza.
Kila wakati ona huna unachojua na hiyo itakusukuma kujifunza zaidi.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Hakika, tubaki kuwa hatari zaidi.
LikeLike
Baki na njaa, baki mjinga.
LikeLike
Tukae humo
LikeLike
Ni maneno ambayo toka nimeyasikia toka kwa Stev Jobs yameendelea kuwa moto wangu BAKI NA NJAA,BAKI MJINGA!
LikeLike
Yaendelee kuchochea moto mkubwa ndani yetu ili tufanye makubwa zaidi.
LikeLike
Asante kocha,Nguvu kubwa ya kuweza kupata mafanikio iko ndani yangu hivyo nitajitahidi kuiamsha na kuitumia.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Ukiaa na njaa utapambana kutafuta chakula hivyo tuwe na njaa mara zote ili tuendelee lutafuta kwa bidii na pia tuendelee kuwa wajinga ili kupata au kutafuta maarifa zaidi na kusonga mbele bila kujalisha mtu
LikeLike
Hakika, tukae humo.
LikeLike
Mimi ni mchezai hatari, silindi goli nashambulia kwa mshambulizi hatari mpaka mwisho wa mchezo.
LikeLike
Safi sana, kaa humo.
LikeLike
Mimi ni mchezaji hatari sana kwenye huu mchezo wa kuelekea ubilionea
LikeLike
Endelea kuwa hatari zaidi.
LikeLike
Mara zote kuwa na njaa kali ya kutaka mafanikio makubwa zaidi na kuwa mjinga wa kujifunza na kuchukua hatua.
LikeLike
Tusimamie hayo.
LikeLike
Tuwe na Hali ya njasa mara zote hata Kama tumeshiba na tuwe na Hali ya kujifunza hata Kama tunajua kila itu
Asante sama
LikeLike
Hivyo ndivyo tunavyoweza kuendelea kuwa hatari.
LikeLike
asee manenoazito ya Steve
LikeLike
Hakika.
LikeLike
Asante Kocha,
Ninabaki na njaa ili niwe mchezaji hatari safu ya ushambuliaji kuupata ushindi.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Baking na njaa baki mjinga maisha yako yote, utakuwa mchezaji hatari sana kwenye haya mashindano ya maisha.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Nabakia na njaa muda wote nataka kuwa na Ari ya kutafuta mafanikio Kama ninavyotafuta chakula au pumzi.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Wale wanaoanzia chini hawana kitu cha kupoteza na ndio maana hufanya makubwa. Naacha kuhalalisha hapa nilipo sasa maana bado ni chini sana ili niwe mchezaji bora kabisa
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike