3202; Asilimia 100.
Rafiki yangu mpendwa,
Kuna namna ya kufikiri tuliyonayo ambayo imekuwa ni kikwazo kwetu kuweza kupiga hatua kubwa.
Namna hiyo ni kutaka uhakika kwenye kila jambo ndiyo tulifanye.
Na siyo tu uhakika, bali uhakika wa asilimia 100.
Yaani tunataka kitu kiwe cha uhakika kabisa ndiyo tukifanye.
Madhara ya hilo ni pale tunapokutana na changamoto na magumu mbalimbali, tunakata tamaa haraka na kutokuendelea tena.
Jambo lolote lenye fursa ya kuweza kufanya makubwa haliwezi kuwa na uhakika wa asilimia 100.
Hivyo hali ya kutaka huo uhakika pekee inakutenganisha na matokeo makubwa ambayo ndiyo yangekupa mafanikio unayoyataka.
Mambo yote yenye uhakika mkubwa, huwa pia yanafanywa na watu wengi na hivyo matokeo yake huwa hayana nguvu ya kumpa mtu mafanikio makubwa.
Vitu vya uhakika tayari vinafanywa na kila mtu.
Ni vile vitu vyenye hatari kubwa ya kushindwa ndiyo huwa vinakimbiwa na walio wengi na hivyo kuwa na fursa kubwa na nzuri kwa anayekuwa tayari kukabiliana na hatari hizo.
Sheria ya asili inadhihirisha hilo wazi kabisa.
Ukiangalia mwituni, chakula cha swala ni majani, ambayo yapo mengi na rahisi kupatikana kwa uhakika mkubwa. Na swala wapo wengi, ambapo pia wanaishia kuwa chakula cha wanyama wengine.
Ukiangalia upande mwingine wa mwitu huo huo, chakula cha simba ni wanyama kama swala, ambao kuwapata kuna shughuli kubwa ya kufanyika kuwakimbiza mpaka kuwapata kama chakula. Simba wapo wachache, lakini ndiyo wafalme wa mwitu.
Swala ana uhakika wa chakula kuliko simba.
Swala hahitaji nguvu kubwa kupata chakula chake kama simba.
Simba ana mamlaka makubwa kuliko swala.
Tunachokiona kwa swala na simba, ndiyo pia kinachotokea kwenye maisha yetu halisi.
Tuchukue mfano wa kampuni au taasisi kubwa na wafanyakazi wawili ndani yake.
Mmoja wa ngazi ya chini, labda mfanyaji usafi na mwingine wa ngazi ya juu kabisa, labda mkurugenzi mtendaji.
Ukiangalia muda wa kufanya kazi unaweza kuwa hautofautiani sana.
Lakini inapokuja kwenye malipo, wa ngazi ya juu atakuwa analipwa sana kuliko wa ngazi ya chini.
Na tofauti yao kwenye malipo siyo ndogo, bali ni kubwa sana, ni tofauti ya mara 10 mpaka mara 100.
Ukiangalia tofauti kubwa ya kazi kwa watu hao wawili tunarudi kwenye uhakika.
Mfanyakazi wa chini anafanya majukumu ambayo ni ya uhakika, yaani yana njia ya uhakika ya kuyatekeleza na matokeo ya uhakika pia.
Lakini hata akiondoka kwenye kazi, kupata mwingine anayeweza kushika nafasi yake ni uhakika pia.
Inapokuja kwa mfanyakazi wa ngazi ya juu, majukumu yake siyo ya uhakika sana. Ni majukumu yanayomtaka kila wakati kufikiri kwa tofauti na kujaribu vitu ambavyo hana uhakika navyo.
Na kama ataondoka, kupata mwingine wa kushika nafasi yake siyo zoezi jepesi.
Kupata matokeo makubwa na yatakayokupa mafanikio, usihangaike sana na mambo yenye uhakika wa asilimia 100.
Badala yake nenda kwenye yale mambo yenye kiasi fulani cha hatari ya kukosa.
Hatari hiyo ndiyo inawakimbiza walio wengi na kuwaacha wachache waliojitoa kweli kweli.
Hamu yako kwenye mambo yasiyokuwa na uhakika inapaswa kuwa kubwa kuliko ilivyo kwa wengine.
Hiyo ndiyo itakupa msukumo wa kuchukua hatua kwenye mambo hayo na kupata matokeo ya tofauti yanayokupa mafanikio makubwa.
Dhana hii pia inahusisha kasi ya utekelezaji wa mambo.
Kusubiri mpaka kupata uhakika mkubwa huwa inachukua muda mrefu na hivyo kumchelewesha mtu.
Lakini kuwa tayari kuchukua hatua hata kabla ya kuwa na uhakika mkubwa inachukua muda mfupi, hatari kubwa zaidi na fursa ya kupata matokeo makubwa.
Kutaka kitu kiwe na uhakika wa asilimia 100 ndiyo ukifanye unakuwa umejilazimisha kufanya kitu ambacho ni cha kawaida sana na hivyo matokeo yake hayawezi kuwa makubwa.
Kutaka uhakika wa asilimia 75 ni mkubwa, lakini pia unakusubirisha sana, kitu kinachokukosesha fursa nzuri.
Uhakika wa asilimia 50 ndiyo namba nzuri ya kwenda nayo. Hiyo ni namba nzuri kuondoa hali ya kubahatisha, lakini pia ambayo inawaondoa wengi ambao hawapo tayari kujisukuma hasa.
Ukishajua unachotaka, kinachofuata ni wewe kufanya kila unachopaswa kufanya ili kupata kile unachotaka.
Usikubali kukwamishwa na jambo lolote lile.
Hivyo ndivyo unavyoweza kufanya makubwa kwenye maisha yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Uhakika wa 50% ndio namba nzuri ya kwenda nayo.
LikeLike
Hakika
LikeLike
Ukishajua unachotaka, kinachofuata ni wewe kufanya kila unachopaswa kufanya ili kupata kile unachotaka.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Ilimradi uwezekano qa kusonga nayo mbele upo wewe usiangalie uhakika wa asilimia 100 maana wengine watakua aanakimbilia huko kwenye hilo la uhakika ila lisilo na uhakika maana yake ni gumu na ukikomaa nalo unafanikiwa na kuvuka upande wapili nalo
Mfano ni kwenye biashara yangu yale mambo marahisi yanafanywa na wengi mfano kusambaza vitu vidogo tuko wengi maana ni rahisi lakini ukija kwenyevikubaa ni wachache ndiyo wanayosambaza sasa huko ndiyo kwenda japo ni garama lakini ukienda ni uhakika kupatamatokeo makubwa
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Asante Kocha.
Sitakubali kukwamishwa na chochote ili niweze kufanya makubwa
LikeLike
Safi sana.
LikeLike
Oooh ukurasa huu naona kama unaongea kwa mimi mara mingi mimi huwa napenda sana vitu vya uhakika hatua ambayo nakwenda kuchukua kwasababu lengo langu nikuufikia ubilionea nitakuwa nakwenda kwenye yale Mambo yenye kiasi fulani cha hatari yakukosa. Asante sana kocha
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Vitu vya urahisi ni uhakika kuvipata ila vitu vikubwa na muhimu inataka kujitoa hasa ili kuvipata
Asante sana
LikeLike
Lazima tujitoe sana.
LikeLike
Asante kocha,Sintakubali kukwamishwa na lolote lile,hivyo ndivyo nitaweza kufanya makubwa kwenye maisha yangu.
LikeLike
Vizuri.
LikeLike
Ilikuwa jasiri usisubiri kuwa na uhakika wa asilimia 100 wa jambo ndipo ulifanye. Inatosha kuwa na ailimia 50
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Fiftyfifty. Uhakika wa 50% ndio namba nzuri ya kwenda nayo.
Asante sana kocha
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Hamu yako kwenye mambo yasiyokuwa na uhakika inapaswa kuwa kubwa kuliko ilivyo kwa wengine
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ukishajua unachotaka kinachofuata ni wewe kufanya kile unachopaswa kufa ili kupata unachotaka
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Hakika sitakubali kukwamishwa na yeyote.muhimi kwangu ni kuendelea kupambania ninachotaka.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitajisukuma kufanya mambo yenye hatari ilikuweza kufanya makubwa katika maisha yangu.
LikeLike
Kila la kheri
LikeLike
Ni kweli usikubali kukwamishwa na Jambo lolote like kuchukua hatua
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Hakuna chochote ambacho kitanikwamisha katika kufikia malengo yangu
LikeLike
Safi sana.
LikeLike