3205; Chini ya hapo unatafuta matatizo.
Rafiki yangu mpendwa,
Kwenye kitabu cha ujumbe kwenda kwa Garcia, tumejifunza madaraja matano ya watu.
Na tukaona tunahitaji kufanya kazi na watu wa daraja la kwanza ambao wanafanya kitu sahihi bila kuambiwa na daraja la pili ambao wanafanya kitu sahihi baada ya kuambiwa mara moja.
Kufanya kazi na watu wa madaraja ya chini ya hayo mawili ni kutafuta matatizo.
Kwa sababu watakusumbua sana, siyo kwa sababu wanataka kukusumbua, bali ndivyo walivyo.
Katika kuendelea kujifunza sifa za kuangalia kwa watu wa kufanya nao kazi, hasa wa kuajiri, nimekuta mahali pengine wamegawanywa kwenye makundi mawili.
Kundi la kwanza wanawaita wafanyakazi nyota (stars) na kundi la pili ni wafanyakazi nyota maarufu (superstars).
Lengo lako ni kuwa na aina hizo mbili tu za wafanyakazi; nyota na nyota maarufu.
Wafanyakazi nyota ni wale ambao wanafika kazini kwa wakati, wakiwa tayari kufanya kazi na wenye shauku ya kukamilisha majukumu yao ya kazi ambao pia wanaweka mbele maslahi ya wateja wako.
Wafanyakazi nyota maarufu ni wale wenye sifa hizo za nyota, lakini pia wana uwezo adimu wa kuikuza biashara. Hawa hawasubiri waambiwe cha kufanya, bali wanajua kinachopaswa kufanyika na wanakifanya vizuri kabla hata hawajaambiwa.
Tukiangalia makundi hayo mawili, tunarudi kule kule kwenye madaraja mawili; wanaojituma na wanaotekeleza baada ya kuambiwa mara moja.
Changamoto inakuja ni wapi tunawapata watu hao?
Kwa sababu hawapatikani kirahisi na waliopo tayari wanafanya kazi mahali pengine.
Hakuna mfanyakazi nyota au nyota maarufu ambaye hana kazi ya kufanya.
Unapotoa tangazo la kazi na watu wakaomba, kwa sehemu kubwa wanakuwa chini ya hayo makundi mawili.
Mara chache chache unaweza kupata nyota na nyota maarufu kwa kuwaiba mahali pengine.
Lakini hiyo siyo njia ya uhakika na ya kutegemea.
Ipo njia ambayo ikifanyiwa kazi inaweza kurahisisha zoezi la kuwapata watu hao nyota na nyota maarufu, ambayo ni kutafuta watu ambao ni bora kisha kuwapa mafunzo sahihi na usimamizi wa karibu ili kuwafanya kuwa nyota na nyota maarufu.
Hili linakutaka uwe na mchakato sahihi wa kuajiri ambao unawachuja wale ambao siyo bora.
Na wale wanaopita kwenye huo mchujo na kupata kazi, wanapata mafunzo endelevu na ya msimamo ya kuwageuza kuwa nyota na nyota maarufu.
Na hapo kwenye mafunzo na usimamizi ndipo pazuri.
Kwa sababu mara kwa mara kuna ambao siyo sahihi watafanikiwa kupita kwenye mchujo.
Lakini mchakato wa mafunzo endelevu utakuwa mgumu sana kwao.
Na hapo watakimbia wenyewe, kama utachelewa kufanya maamuzi ya kuwaondoa.
Lengo la kuwa na mafunzo na usimamizi endelevu ni kuwageuza wafanyakazi bora kuwa nyota na nyota maarufu.
Hivyo unapokutana na mfanyakazi ambaye siyo bora, unapaswa kuchukua hatua za haraka za kumsukuma awe bora.
Na kama hilo litashindikana, unapaswa kuwaondoa haraka sana, maana tabia yao ya kutokuwa bora huwa inaambukizwa kwa kasi sana.
Pale unapomwacha kwa muda mrefu wakati hana mwelekeo wa kuwa nyota au nyota maarufu, anaishia kuwaharibu wengine waliokuwa na mwelekeo huo.
Mmoja wa viongozi bora wa kibiashara kuwahi kutokea, ambaye alikuwa mkurugenzi wa kampuni ya General Electric ya nchini Marekani, Jack Welch, alikuwa na sera ya kila mwaka kufukuza asilimia 10 ya wafanyakazi wa kampuni yake.
Kwa tathmini za utendaji zilizokuwa zinafanyika kila mwaka, ile asilimia 10 ya chini aliwafukuza bila hata ya kusita au kusubiri.
Kwa sababu alijua biashara huwa inaharibiwa na aina hiyo ya wafanyakazi.
Wapo waliokuwa wanakosoa hilo, wakisema huenda kuna wafanyakazi wazuri aliwafukuza.
Inaweza kuwa kweli kuna wafanyakazi wazuri aliwafukuza, lakini unapokuwa na maelfu ya wafanyakazi, ni kazi ya ziada kufanya maamuzi kwa mmoja mmoja.
Hivyo kigezo chochote kitakachokuwa rahisi kwako kutumia, unapaswa ukitumie.
Kwa sababu manufaa yake ni itapeleka ujumbe kwa wengine kwamba wawe bora sana la sivyo watakwenda na maji.
Sawa, turudi kwetu, tutajuaje wafanyakazi wazuri wa kuacha na wabaya wa kufukuza?
Hilo ni rahisi hasa tunapokuwa tunaanza na wafanyakazi wachache ambao tabia zao tunaziona moja kwa moja.
Tunaanza na ari kwenye kazi; kama mfanyakazi hawahi kazini na kama akiwa kwenye majukumu yake siyo mchapakazi na hana shauku, huyo ni wa kuachana naye. Hilo wala halihitaji mjadala.
Pagumu ni kwa wale wanaovuka ngazi hiyo ya kwanza, ambao wanaouwa na ari ya kazi, lakini bado hawawezi kuwa nyota au nyota maarufu kama unavyotaka.
Ugumu unakuja kwenye kigezo cha kuwaondoa na utayari wa kufanya hivyo, kwa sababu wanaonekana kuwa na manufaa.
Tukianza na vigezo, hapa ndipo mafunzo endelevu yanapohusika.
Weka mfumo wa mafunzo endelevu kwenye biashara yako halafu angalia nani wana shauku ya kujifunza na nani hawana.
Wasiopenda kujifunza hakuna namna wataweza kuwa nyota au nyota maarufu, hivyo ni wa kuachana nao.
Wafanyakazi wenye uwezo wa kuwa nyota au nyota maarufu hawahitaji kuhamasishwa ndiyo wajifunze au kutekeleza majukumu yao.
Tayari ndani yao wana hamasa kubwa ya kujifunza na kuwa bora zaidi ya walivyo sasa.
Unachohitaji wewe ni kuwapa lengo kisha kuwapisha walikamilishe.
Kwa upande wa utayari wa kuwaondoa, ukizingatia wanafanya kazi, utakivuka hicho kwa kila mara kuwa kwenye mchakato wa kuajiri.
Unaandaa mfumo wa kuajiri ambao kila wakati unakuwa na mchakato wa kupata watu, kuwachuja, kuwapa kazi kwa majaribio na kuwapa mafunzo endelevu.
Hivyo kila unapopata mfanyakazi ambaye ana mwelekeo wa kuwa nyota au nyota maarufu, anakwenda kuchukua nafasi ya aliyepo ambaye ni mzuri, lakini siyo bora.
Hivyo kuna wafanyakazi ambao utawaacha kwa muda kwenye biashara yako kwa sababu wanaweza kutekeleza majukumu yao ya sasa, ila hawana ukuaji.
Lakini huwaachi kwa kuridhika, badala yake unakazana kupata na kuendeleza wengine kwa kasi ili waje kuchukua nafasi hiyo.
Kiwango cha juu cha muda cha kukaa na mfanyakazi ambaye hawezi kuwa nyota au nyota maarufu ni miezi mitatu (siku 90). Katika kipindi hicho anapaswa kupewa kila fursa ya kuwa bora zaidi ya alivyo.
Wakati huo huo mtu wa kushika nafasi yake anakuwa anaandaliwa kwa kasi kubwa.
Siku 90 zinapoisha na mtu hajawa bora kama alivyotegemewa, kazi yake inaishia hapo.
Mwingine aliyeandaliwa anachukua nafasi hiyo.
Na zoezi linaenda hivyo kwa uendelevu.
Huenda unafikiria mbona kama itakuwa kazi kubwa sana?
Na mimi nikuambie; karibu kwenye mchakato wa kujenga biashara kubwa inayoweza kujiendesha bila ya uwepo wako wa moja kwa moja.
Ingekuwa rahisi, kila mtu angefanya.
Siyo rahisi, ndiyo maana ni wachache sana wanaofanya.
Kama utakuwa mmoja kati ya hao wachache, utaweza kufanya makubwa.
Je utakuwa?
Shirikisha hapo chini mkakati uliotoka nao hapa wa kwenda kujenga timu bora na hatua unazoenda kuchukua mara moja.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Naenda kujenga timu bora yenye wafanyakazi Nyota na Nyota maarufu pekee nikianza na eneo la mauzo na mengine kufuata.
LikeLike
Chini ya hapo hakuna nafasi.
LikeLike
Kuwaajiri walio bora ili kuwapa mafunzo awe bora zaidi
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Naenda kujenga timu Bora kabisa yenye watu wa nyota na nyota maarufu Kwa Kuanza na kigezo cha kuwafundisha na kuajiri wapya kila.mara
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante kocha,Nakwenda kujenga timu kwa kutumia kigezo cha miezi mitatu kama mfanyakazi haendani na mchakato wa biashara hakuna kusubili ni kumsimamisha .
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Nitahakikisha natoa mafunzo bora kwa kujingatia miongozo na pia Naenda kujenga timu Bora kabisa yenye watu wa nyota na nyota maarufu Kwa Kuanza na kigezo cha kuwafundisha
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Kwa kuweka mafunzo endelevu kwenye Biashara yangu halafu Kuangalia nani ana shauku ya kujifunza na nani haha.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Wafanyakazi wangu lazima wawe na shauku , wawe tayari kujifunza ambazo Hawako tayri kujifunza hawo ni wa kuachana nao.
Ili niweze kupata wafanyakazi nyota na nyota wa nyota nakwenda kufanyia kazi mchakato wa kuajiri endelevu wa kuwapata kwa miezi mitatu mitatu yule ambaye Hawezi kubadilika naachana Naye.
LikeLike
Kila la kheri.
LikeLike
Asante Kocha:
I. Kujituma; kuwahi, umakini, uaminifu
2. Shauku kubwa; hamasa ya kudumu
3. Kujifunza: kuwe endelevu, ushirikiano na wengine
Hayo ndiyo ya msingi kabisa ya kuangalia kwa kila mwana timu.
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike
Nitaongeza kijana mmoja kwenye biashara yangu na kumpa Siku 90 za matazamio. Baada ya kumpata kijana huyu moja kwa moja nitamuandikisha kwenye chuo cha mauzo ili iwe rahisi kumfuatilia namna anavyo kaa kwenye mchakato wa chuo cha mauzo nikiwa nashirikiana kwa ukaribu na mwalimu wake wa chuo.
Asante
LikeLike
Mpango mzuri sana.
Na 2023-2024 CHUO CHA MAUZO kinaenda kuwa moto sana.
LikeLike
Ni kuangalia wafanyakazi nyota na nyota maarufu tu si chini ya hapo.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ni sawa ila mara nyingine wafanyakazi bora wanahamasishwa na malipo na mishahara mizuri. Mimi nitatoa mafunzo endelevu kazini pamoja na motisha
LikeLike
Vizuri, hilo tulishalijadili kwenye ukurasa wa wateke; https://www.kisimachamaarifa.co.tz/2023/05/08/3050-wateke/
LikeLike
Ili kuwapata wafanyakazi star na super star nitaweka mfumo wa mafunzo endelevu kwenye biashara yangu halafu nitaangalia walio na shauku ya kujifunza na nani hawana.
Asante
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Nitaajiri kwa vigezo,na ili awe nyota/nyota maarufu nitampa kipindi cha majaribio na kuhakikisha nampa fursa ya kuwa bora zaidi ya alivyo.
LikeLike
Vizuri
LikeLike
Hakika huo ni mchakato Bora na kama tutafanikiwa kufanya kwenye biashara zetu tutafika kule tunakotaka kufika, tuendelee kuufanyia kazi mchakato huu wa kuajiri ili tupige hatua kwenye biashara zetu
Asant
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Tangu niliposoma ukurasa wa 3165, niligundua Huruma zilikuwa zinaziponza na kuamua kuachana nazo mara moja,na hapohapo mfanyakazi mmoja nirimfukuza mara moja,
Hivyo lengo na mpango ni kujenga timu bora inayozingatia utaratibu,kanuni na miongozo, kinyume na hapo ni kutafutana ubaya, natamani kuona mwaka 2023_2024 kuwa mwaka wa mabadiliko makubwa.
LikeLike
Safi sana,
Mikakati tuliyonayo 2023-2024 ni ya moto sana.
LikeLike
Asante sana. Steve Jobs wafanyakazi alikuwa anawagawa kama A players na B payers. Na kama ulikuwa chini ya hapo alikuwa anakuita ashole.
Yaani, kwake hawakuwa wafanyakazi tu hata watu kwenye maisha ya kawaida. Ni kama alikuwa amechora sehemu mstari usioonekana uliokuwa unagawa watu kwenye pande mbili.
Upande wa watu hora Kuwahi kutokea na upande wa vilaza. Kwa hiyo yeye alikuwa anakuweka upande mojawapo na alipokuwa akikuweka upande wa vilaza ilikuwa ni vigumu kutoa.
Kwa upande mwingine Jack Welch, alikuwa na kanuni ya 20-70-10.
Asilimia 20 Hawa Ndiyo super stars. Hawa wanastahili kuongezea mshahara, bonus stocks na kupewa mafunzo extra.
Asilimia 70 ni stars. Hawa waendelee kufundiahwa Ili wapande kutoka hapa na kuingia kwenye asilimia 20 ya juu.
Asilimia 10 ya mwisho walikuwa wanafukuzwa.
Na hiki kitu ndio ninaenda kufanyia KAZI kwenye Biashara yangu.
LikeLike
Umeeleza vyema,
Hata Elon Musk pia ana utaratibu huo.
Ni vigumu sana kufanya makubwa ukiwa na wafanyakazi wa kawaida.
LikeLike
Ninakwenda Jenga timu Bora . Nitaanza kwa kuchuja waliopo , ambao watakua chini ya viwango nitawaondo
a na nitatafuta walio Bora.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike