3267; Kuzingatia na Kuepuka.
Rafiki yangu mpendwa,
Mara nyingi watu wamekuwa wanafundishwa na kushauriwa kuhusu mambo ya kuzingatia ili kupata mafanikio wanayokuwa wanayataka.
Hayo ni mambo ambayo wanapaswa kuyafanya ili wapate matokeo wanayotaka kupata.
Mambo ya kuzingatia ni muhimu, lakini hayo pekee hayatoshi kumpa mtu mafanikio makubwa anayokuwa anayataka.
Kwani huwa kuna mambo yasiyo muhimu au hata yenye madhara ambayo huwa yanajipenyeza kwenye mipango ya mtu.
Mambo hayo huwa yanajipenyeza kwenye nafasi zinazopatikana kulingana na udhaifu ambao mtu anakuwa nao.
Ni kwa sababu hiyo ndiyo inapaswa mtu pia kuwa na mpango wa mambo ya kuepuka kufanya. Hapa ni kuzuia yale mambo yanayojipenyeza na kumkwamisha mtu kupata mafanikio anayokuwa anayataka.
Kwa kupanga kwa makusudi kuyaepuka hayo mambo, kunayanyima nguvu ya kujipenyeza na kuleta madhara kwenye mipango yako.
Hivyo basi, kama ambavyo unapanga mambo ya kuzingatia ili kufanikiwa, hakikisha pia unapanga mambo ya kuepuka ili yasikukwamishe kwenye mafanikio yako.
Tuangalie mfano wa biashara ili tuelewane vizuri zaidi.
Ili kujenga biashara yenye mafanikio makubwa, unapaswa kuzingatia mambo haya;
1. Kutoa thamani kubwa kwa wateja.
2. Kujenga timu bora ya kuendesha biashara hiyo.
3. Kutengeneza wateja bora na kwa uendelevu.
4. Kutengeneza faida kwa uhakika.
5. Kulitawala soko au eneo fulani la soko.
6. Kuendelea kukua kadiri muda unavyokwenda.
Hayo yote ni mambo ya kujumlisha au kuongeza ili biashara iweze kufanikiwa.
Lakini kufanya hayo pekee bado haitoshi, kwani kuna ambayo huwa yanajipenyeza na kuvuruga.
Hayo ndiyo unapaswa kuyaepuka ili kujenga biashara yenye mafanikio.
Yafuatayo ni mambo ya kuepuka kwenye kujenga biashara yako;
1. Epuka gharama zinazokuwa zinaongezeka kwenye biashara kadiri kipato kinavyoongezeka.
2. Epuka kuhangaika na mambo ambayo hayana mchango kwenye ukuaji wa biashara yako.
3. Epuka watu ambao hawaja mchango kwenye maendeleo ya biashara.
4. Epuka wateja ambao siyo sahihi kwa biashara yako, wale ambao hawaielewi thamani unayoitoa.
5. Epuka kufuata mkumbo au kuiga wengine kwenye yale wanayofanya.
6. Epuka kukimbizana na fursa mpya kila wakati kabla biashara yako haijaweza kujiendesha yenyewe bila kutegemea uwepo wako.
Hayo ya kuepuka ni ya kukataa au kuondoa kabisa kwenye mipango yako ili jugudi kubwa unazoweka zisikwamishwe na mambo madogo madogo ambayo unaweza usione madhara yake kwa haraka.
Kwenye safari yako ya mafanikio usiangalie tu ya kuzingatia, bali pia angalia ya kuepuka ili ifanikiwe.
Kama ambavyo Charlie Munger alikuwa akisema; “ninachotaka kujua ni wapi nikienda nitakufa ili nisiende hapo.”
Wewe kila mara jiambie; “ninachotaka kujua ni nini nikifanya kitaua biashara yako ili nisikifanye.”
Kuepuka matatizo kuna nguvu na manufaa kuliko kuja kuyatatua baada ya kutokea.
Ukizingatia na kuepuka kwa pamoja, inajenga nguvu ya kuzalisha matokeo makubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
#UpekeeUdadisiUbunifu
#UshirikianoUtegemeanoUwajibikaji
#BilioneaMafunzoni
#NajengaBiashara
#HakunaKingineMuhimu
#LazimaNitoboe
#NawekaKaziNifanikiwe
Nitazingatia yale muhimu na kuepuka yale yanayoweza kuwa kikwazo kufikia ndoto kubwa nilizonazo.
LikeLike
Vizuri sana na kila la kheri.
LikeLike
Ninachotaka kujua ni wapi nikienda nitakufa ili niepuke kwenda sehemu hiyo.
Epuka yale yanayofanywa na wengi.
Yale ambayo ukiyafanya yanapelekea wewe kushindwa.
Epuka mkumbo na kuwa mbunifu.
Asante sana Kocha Dr Makirita Amani.
LikeLike
Kuna hekima nyingi sana kutoka kwa Munger, tuzitumie kuwa na maisha bora.
LikeLike
ninachotaka kujua ni nini nikifanya kitaua biashara yangu ili nisikifanye.”
LikeLike
Ukisimama hapo, unakuwa imara.
LikeLike
Jua kuepuka na kukataa kabisa mambo madogo madogo yanayokwamisha mipango na juhudi kubwa unazoweka
LikeLike
Hakika, madogo yanapoteza sana.
LikeLike
Kuchukua tahadhari mapema ni bora kuliko Kupambana na tukio lenyewe au kinga ni bora kuliko tiba.
LikeLike
Ndiyo
LikeLike
Ili kujenga biashara yenye mafanikio zingatia yale ya msingi na kuyafanyia kazi na kuachana na yasio na tija
Asante sana
LikeLike
Hakika
LikeLike
Kuzingatia yale muhimu,
Kuepuka yasiyo ya msingi na
Kujua nini nikifanya ktaua biashara yangu ili nisifanye.
🙏🙏
LikeLike
Tukae humo.
LikeLike
Ni muhimu sana kuyaepuka matatizo kabla, ni muhimu mnoo.
LikeLike
Muhimu sana.
LikeLike
Nawaepuka watu wote wasio na mchango kwenye ukuaji wa biashara yangu.
LikeLike
Hilo ni muhimu, maana wanakuwa kikwazo.
LikeLike
Nitayaepuka Mambo yote yanayoweza kuua biashara yangu.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike
Nitazingatia na kuepuka kwa pamoja, (Kulinda na Kushambulia) inajenga nguvu ya kuzalisha matokeo makubwa.
LikeLike
Kabisa, yote mawili yanakuwa na nguvu kubwa.
LikeLike
Nitazingatiaje na kuepuka,ni kuzingatia miiko,miongozo sahihi ya kile ninachofanya.
LikeLike
Vizuri
LikeLike