
Kakaa/Dadaa Yangu…
Kuna uongo mmoja hatari sana unaoenezwa Kwenye jamii zetu…
Watu wanaambiwa mafanikio ni siku moja kubwa.
Siku moja utajikuta na gari.
Siku moja utakuwa na pesa za kukutosha.
Siku moja utahama mtaa.
Siku moja…
Siku moja…
Siku hiyo haiji bwana.
Mafanikio si sherehe ya ghafla.
Ni safari ya kila siku bila makelele.
Wewe unasema unataka kufanikiwa, sawa…
Lakini unalala hadi saa nne asubuhi.
Simu ndiyo bibi yako.
Series zimekuwa chakula cha akili yako.
Maisha yako yanaenda kwa “autopilot”.
Upo tu.
Ukisubiri muujiza.
Bro, Sister, hakuna muujiza bila jasho.
Hii dunia haitoi zawadi kwa wavivu.
Ina wanyonya.
Na inawatupa bila huruma.
Sikiliza vizuri…
Mafanikio ni mazoea madogo unayorudia kila siku.
Ni kuamka mapema, hata kama hupendi.
Ni kusoma ukurasa mmoja, hata kama huna mood.
Ni kupanga siku yako kabla haijaanza.
Ni kukataa vishawishi vidogo kwa ndoto kubwa.
Wale wanaosema “take it easy, usijibane sana”
Ndiyo wale wale watakucheka ukifeli.
Wakupe pole usiku, mchana wakutangaze.
Usikubali!
Hata kama ni kwa dakika 15.
Soma, tafakari, panga.
Jifunze kitu kipya.
Andika ndoto zako.
Jikumbushe sababu zako.
Chapa kazi hata kama haionekani leo.
Hiyo ndiyo siri.
Mafanikio hujificha ndani ya maumivu ya kila siku.
Na mwishowe hutokeza kwa kishindo.
Mimi ni shahidi.
Nilianza kuandika bila jina.
Nilikuwa naandika status zinasomwa na watu wawili.
Nilikaa hadi usiku nikiandika makala kama hii bila malipo.
Wakati wengine wanalala, mimi nilikuwa naota nikiwa macho.
Leo hii…
Watu wananitafuta.
Wananilipa.
Wananiamini.
Lakini yote yalianza na ile siku niliyoamua kuamka mapema.
Siku niliyoamua… kila siku ni nafasi ya kufika mbali.
Na sitaki nisikie mtu anasema, “wewe ni bahati.”
Hapana.
Ilichongwa kwa jasho la kila siku.
Mafanikio ni kila siku.
Sio mwendo wa kusprint.
Ni marathon ya moyo, bidii, na nidhamu.
Usijilinganishe.
Jilinganishe na wewe wa jana.
Na hakikisha kesho, unamshinda huyo wa leo.
Leo umeamka sasa swali ni moja tu:
Utafanya nini?
Anyway,
Kama bado hujajiunga na wenzake makini kwenye huduma za ukocha, bonyeza hapa 👇 na utapewa utaratibu wa kujiunga.
https://wa.link/i2r67s
Karibu.
0756694090.
Imeandikwa Na Mkufunzi Ramadhan Amir.