
Kakaa/Dadaa Yangu…
Wengi Wanashindwa.
Watu wengi wanatamani sana kuwa na biashara zao.
Wanachoka kuamka asubuhi kwenda kazini kwa mtu.
Wanakasirika kuona pesa zao zikilipia ndoto za wengine.
Lakini kila wakitaka kuanzisha biashara, akili inagoma.
Nakujiambia…
“Mwanangu biashara inahitaji mtaji mkubwa…”
“Aaah, siku hizi biashara ni ngumu bana…”
“Bora nikatae tu, nisijiumize moyo…”
Unasikia hizo sauti?
Zinaonekana kama ushauri, lakini ni mtego.
Mtego wa ubaki pale pale.
Ukiwa na ndoto kubwa, lakini ukiishi maisha madogo.
Inaumiza sana,
Kwa sababu kila siku inaisha bila kupiga hatua yoyote.
Unaamka. Una scroll Instagram.
Unamuona jamaa yako wa zamani anaendesha gari mpya.
Anaposti “Nashukuru Mungu kwa neema.”
Unamjua vizuri kwamba hana hata degree.
Hakusoma sana kama wewe.
Lakini ana biashara. Ana uhuru. Anaishi maisha ya ndoto zake.
Wewe bado upo hapo unajiambia, “Siku moja nitaanza.”
Siku moja haiji. Mwaka unaisha. Maisha yanasonga.
Unakuwa mtaalamu wa kupanga, sio wa kuchukua hatua.
Na hapa ndipo watu wengi wanakosea.
Wanasubiri hali iwe sawa.
Wanasubiri mtaji wa milioni.
Wanasubiri mtu awashike mkono.
Hebu Nikuambie Ukweli,
Na Tuivunje Ile Imani Potofu.
Biashara haianzi na pesa.
Biashara haianzi na duka kubwa.
Biashara haianzi na mkopo wa benki.
Biashara inaanza na wazo + ujasiri + hatua ndogo.
Kama huwezi kuuza kitu cha buku, huwezi kuuza kitu cha elfu 10.
Kama huwezi kupata mteja mmoja, huwezi kupata mia.
Watu wanalala wakisubiri kuamka na mtaji.
Lakini hawajui hata namna ya kuuza idea zao.
Unataka biashara yako ikue?
Acha kufikiria sana. Anza kufanya.
Acha kutafuta approval ya watu.
Anza kutafuta mteja wako wa kwanza.
Sasa Sikiliza Nikuambie….
Na Hizi Hapa Ndizo Mbinu Zenyewe.
(a) Anza na kitu unachokielewa au unachokipenda.
Usianze kwa kufuata pesa. Anza kwa kufuata suluhisho unaloweza kutoa.
(b) Fanya utafiti.
Tafuta watu wenye shida hiyo.
Angalia wanahangaika na nini.
Uwauzie suluhisho.
(c) Tengeneza kitu cha bei rahisi.
Toa sample. Toa ladha ya huduma yako.
Watu waone thamani kabla hawajatoa hela.
(d) Tengeneza jina.
Tumia WhatsApp, status, Facebook, IG.
Simama kama mtu anayeaminika.
(e) Kua pole pole.
Kama leo unapata mteja mmoja, kesho wawili.
Boresha. Rudia. Panua.
Hapo ndipo biashara inapanuka.
Bado namkumbuka….
Dada Yangu Mary Alinifunza Mengi.
Mary alikuwa anauza maandazi kwa shilingi 100.
Watu walimcheka. Walisema, “Hii si biashara.”
Lakini alikuwa na kitu kimoja consistency.
Alikuwa analeta kwa wakati.
Anacheka na wateja.
Anatoa bonus kwa mteja wa tatu.
Miezi mitatu baadaye, alipata mteja wa catering.
Akapika kwenye harusi.
Akapata hela ya kuongeza mtaji.
Sasa ana duka la vyakula.
Ana wafanyakazi wawili.
Wale waliomcheka, sasa wanamuuliza anatoa kazi lini.
Biashara yake ilianza na mafuta ya buku tano na unga wa kilo moja.
Lakini aliweka moyo.
Aliweka ubunifu.
Aliweka tabasamu.
Sasa Ni Zamu Yako
Acha kuogopa.
Acha kungoja hali iwe “shwari.”
Anza na ulicho nacho.
Fanya vizuri kuliko wote.
Fanya kwa moyo.
Fanya kila siku.
Kumbuka Hii:
Biashara si ya matajiri.
Biashara ni ya wale waliochoka kusubiri.
Na kitabu kilichomfungua Dadaa Mary ni kitabu Kinachoitwa ELIMU YA MSINGI YA BIASHARA.
Kama unacho hongera na rudia kuisoma sura ya kwanza.
Lakini kama bado hujakipata bonyeza hapa 👇
https://wa.link/gr5iim
Karibu.
0756694090.
Hii Makala Imeandikwa Na Mkufunzi Ramadhan Amir.