Sikiliza hapa;
Rafiki yangu Mpendwa,
Matamanio ya mafanikio ni makubwa kwa walio wengi. Japo wanaoyapata mafanikio makubwa wakibaki kuwa wachache. Na siyo kwamba wanaoshindwa wanakuwa wavivu, wapo wanaopambana hasa, lakini bado hawapati mafanikio makubwa kama wanavyotaka.
Na siyo kwamba hawajui siri na misingi ya mafanikio. Wengi wamejifunza mengi kuhusu mafanikio, kwa hiyo wanajua. Na hata kwenye kufanya, wanafanya. Na hata baadhi, wanafanya kwa msimamo kweli kweli.
Pamoja na kufanya yale yote yanayoelekezwa kuleta mafanikio, bado wengi hawayapati mafanikio. Na hilo limekuwa linafanya baadhi kudhani labda kuna nguvu za ziada zinazohitajika kwenye mafanikio. Labda bahati au miujiza fulani ambayo mtu hana udhibiti nayo.
Hakuna nguvu za ziada zilizo nje ya uwezo wa mtu zinazohitajika ndiyo mtu aweze kufanikiwa. Ila kuna sharti moja ambalo ni rahisi, kwa sababu ni moja tu, lakini ni gumu kwenye utekelezaji wake, ambalo linatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa. Ni sharti moja tu ambalo mtu akilitimiza, ushindi na mafanikio makubwa ni uhakika kwake.
Kwenye barua hii tunakwenda kuangalia sharti hilo na jinsi unavyoweza kulitimiza ili uweze kupata mafanikio makubwa unayoyataka kwa uhakika.

1. Ukifanya kila kitu, utashinda.
Kabla ya mwaka 1957, bunge la Seneti la Marekani halikuwa limewahi kupitisha sheria za mageuzi makubwa. Licha ya miswada mbalimbali kupelekwa bungeni, mgawanyiko mkubwa ulifanya miswada hiyo kupitishwa na kuwa sheria.
Ni mpaka mwaka huo 1957, ambapo Lyndon B. Johnson, akiwa kiongozi wa Seneti aliweza kubadili kabisa mwelekeo mzima wa Seneti. Aliweza kushawishi Maseneta wengi na miswada mikubwa kupitishwa. Kwenye historia ya taifa la Marekani, Lyndon anachukuliwa kama mtu aliyeweza kubadili kabisa mwenendo wa Seneti.
Hakuishia hapo, aliweza kuwa makamu wa raisi na hatimaye kuwa raisi. Katika vipindi hivyo vya uongozi wa juu kama makamu na kama raisi aliweza kusimamia vyema propramu ya Marekani kupeleka watu mwezini kwa mara ya kwanza.
Lyndon hakuanzia kwenye familia inayotokana kwenye mamlaka au yenye utajiri. Alitoka familia ya chini kabisa, lakini tangu akiwa shule alikuwa mtoto aliyefanya mambo mengi na kushinda nafasi mbalimbali.
Akiwa na umri wa miaka 24 aliingia kwenye siasa na haikumchukua muda mrefu akawa mmoja wa vijana wenye ushawishi mkubwa kwenye siasa. Mengi yameandikwa kuhusu yeye, kwa jinsi alivyoweza kushinda uchaguzi kwa kutumia nguvu kubwa na mabadiliko mengi aliyoleta.
Lakini yote hayo yaliwezekana kwa sharti moja alilolijua mapema na kuliishi wakati wote. Sharti hilo ni; “If you do everything, you’ll win.” Akimaanisha; “Ukifanya kila kitu, utashinda.”
Hiyo haikuwa tu kauli ya kujifariji, bali ulikuwa ndiyo mtindo wa maisha wa Lyndon. Alipotaka kupata matokeo fulani, alifanya kila kitu kuhakikisha anapata matokeo, na kweli aliyapata matokeo.
Alipoanza kama msaidizi wa mbunge, alihakikisha kila kitu kinachomhusu mbunge huyo anakijua na kukifanyia kazi. Hilo lilimfanya aaminike haraka na kupewa majukumu makubwa.
Alipokuwa kiongozi wa Seneti na kutaka kupitisha mswada muhimu, aliwajua Maseneta wote na kuongea na kila mmoja na kuwageuza, mmoja mmoja, wale waliokuwa wanapinga mswada huo.
Kwa kifupi Lyndon alifanya kila kitu, hakuacha kitu chochote kwa kutegemea bahati au mambo yaende vizuri. Yeye alihakikisha kwamba analazimisha mambo yaende vizuri. Na kweli yalienda vizuri, kwa kumwezesha kutimiza mambo ambayo yalikuwa yamewashinda watu wengi.
Kujifunza jinsi ya kutimiza sharti hilo, soma #BaruaYaKocha hapa; #BZK073; Hili Ndilo Sharti Pekee La Kupata Mafanikio Mafanikio Makubwa