Hii Ndiyo Siku Ya Mwisho Kabisa Kupata Nafasi Ya Kushiriki Semina Ya TABIA ZA KITAJIRI, Soma Hapa Na Uchukue Hatua.

Rafiki yangu mpendwa, Kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa nimekuwa nakupa taarifa za semina ya kuuanza mwaka 2019. Semina hiyo inakwenda kwa jina la TABIA ZA KITAJIRI. Ndani ya semina hii tunakwenda kujifunza tabia kumi za kuishi kila siku ambazo ukizielewa na kuzifanyia kazi basi utaweza kutengeneza utajiri na mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Semina... Continue Reading →

Kauli Nane Kuhusu Fedha Za Kuziacha Mwaka 2018 Ili Mwaka 2019 Uwe Wa Mafanikio Makubwa Kifedha Kwako.

Rafiki yangu mpendwa, Watu husema ya kwamba kauli zinaumba. Kile unachofikiri na kusema muda mrefu, ndiyo kinachotokea kwenye maisha yako. Hapo ulipo sasa ni matokeo ya fikra ambazo umekuwa nazo kwa muda mrefu na kauli ambazo umekuwa unazitumia. Na linapokuja swala la fedha, zipo kauli nyingi ambazo umekuwa unatumia na zinachangia wewe kubaki kwenye umasikini.... Continue Reading →

Zimebaki Siku Tano Pekee Upate Nafasi Hii Ya Kipekee Ya Kuagana Kabisa Na Umasikini Kwenye Maisha Yako.

Rafiki yangu mpendwa, Aliyekuwa raisi wa 16 wa taifa la Marekani, Abraham Lincolin amewahi kunukuliwa akisema; “That some should be rich shows that others may become rich, and hence is just encouragement to industry and enterprise.” Akimaanisha kwamba wachache wanapaswa kuwa matajiri ili wengine wajifunze kwamba inawezekana na wao kuwa matajiri pia. Na hili linaleta... Continue Reading →

Salamu Za Likizo Kutoka Kwa Kocha Dr Makirita Amani Na Mambo Matatu Muhimu Sana Kwako Kufanyia Kazi Leo.

Habari rafiki yangu mpendwa, Napenda kuchukua nafasi hii ya kipekee sana kukufikishia salamu za likizo yangu niliyokuwa nayo tangu tarehe 21/12/2018 mpaka tarehe 27/12/2018. Imekuwa ni likizo bora sana kwangu na mengi niliyopanga kufanya nimefanikiwa kuyakamilisha, isipokuwa kwa machache ambayo muda haukuweza kutosha kuyatekeleza. Likizo hii imekuwa ni siku saba za kupata nafasi ya kuwa... Continue Reading →

Ishi Kwa Tabia Hizi Kumi (10) Kila Siku Ya Maisha Yako Na Utaweza Kupata Mafanikio Makubwa Sana Kwenye Maisha Yako.

Rafiki yangu mpendwa, Mtu mmoja amewahi kusema kwamba huwa tunajenga tabia, kisha tabia zinatujenga. Na hili ni kweli kabisa. Mwanzoni wakati tunajifunza tabia yoyote ile, iwe nzuri au mbaya huwa tunaweka kazi hasa. Lakini baadaye ikishakuwa tabia tunajikuta tunafanya bila hata ya kufikiri. Maisha yetu yapo pale yalipo sasa kutokana na tabia ambazo tumejijengea siku... Continue Reading →

Vigezo Vitano (05) Unavyopaswa Kuvitumia Wakati Unaweka Malengo Ili Uweze Kuyafikia.

Habari rafiki yangu mpendwa, Wapo watu ambao wamekuwa wanayaendesha maisha yako kama saa ya mshale ambayo imeharibika. Kwa nje mishale inaweza kuonekana kama inafanya kazi, lakini kwa hakika imesimama. Wapo watu ambao kila mwanzo wa mwaka huwa wanaweka malengo makubwa, malengo yanayowahamasisha sana na kuwafanya waone wanaweza kufanya makubwa kwenye maisha yao. Lakini siku chache... Continue Reading →

Mambo Kumi (10) Ya Kufanya Mwezi Disemba Ili Mwezi Januari Uwe Wa Mafanikio Makubwa Sana Kwako.

Rafiki yangu mpendwa, Mwezi disemba na mwezi januari ni miezi miwili ambayo watu wengi wamekuwa wanaipoteza kwenye maisha yao. Wengi wanaupoteza mwezi disemba kwa kupunguza kasi ya mapambano, kwa kuwa mwaka unakuwa umefika ukingoni, wengi huona hakuna kikubwa wanachoweza kufanya hivyo wanasubiri mwaka mpya uanze. Na mwezi januari huwa unapotea kwa sababu wengi huweka malengo... Continue Reading →

Hivi Ndivyo Elfu Moja Kila Siku Kwa Siku 20 Inavyoweza Kuyabadili Maisha Yako Na Kukufikisha Kwenye Utajiri.

Rafiki yangu mpendwa, Salamu zangu za mafanikio zikufikie popote pale ulipo sasa, wakati unaendelea na mapambano ya kuyaboresha maisha yako na kufikia mafanikio makubwa. Kumbuka nipo na wewe kwenye safari hii, kila wakati nikikushirikisha maarifa bora sana kwako ili uweze kufika kule unakotaka. Kwa sababu kama ambavyo nimekuwa nakusisitizia, hakuna kinachoweza kukuzuia kufanikiwa ila wewe... Continue Reading →

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑