Mambo Kumi (10) Ya Kufanya Mwezi Disemba Ili Mwezi Januari Uwe Wa Mafanikio Makubwa Sana Kwako.

Rafiki yangu mpendwa, Mwezi disemba na mwezi januari ni miezi miwili ambayo watu wengi wamekuwa wanaipoteza kwenye maisha yao. Wengi wanaupoteza mwezi disemba kwa kupunguza kasi ya mapambano, kwa kuwa mwaka unakuwa umefika ukingoni, wengi huona hakuna kikubwa wanachoweza kufanya hivyo wanasubiri mwaka mpya uanze. Na mwezi januari huwa unapotea kwa sababu wengi huweka malengo... Continue Reading →

Hivi Ndivyo Elfu Moja Kila Siku Kwa Siku 20 Inavyoweza Kuyabadili Maisha Yako Na Kukufikisha Kwenye Utajiri.

Rafiki yangu mpendwa, Salamu zangu za mafanikio zikufikie popote pale ulipo sasa, wakati unaendelea na mapambano ya kuyaboresha maisha yako na kufikia mafanikio makubwa. Kumbuka nipo na wewe kwenye safari hii, kila wakati nikikushirikisha maarifa bora sana kwako ili uweze kufika kule unakotaka. Kwa sababu kama ambavyo nimekuwa nakusisitizia, hakuna kinachoweza kukuzuia kufanikiwa ila wewe... Continue Reading →

SEMINA; TABIA ZA KITAJIRI; Ahadi Kumi Za Kuishi Kila Siku Ili Kufikia Utajiri Na Mafanikio Makubwa Kwenye Maisha.

Rafiki yangu mpendwa, Ninayo furaha kubwa sana kukupa taarifa muhimu sana za semina yetu kubwa ya kwenda kuuanza mwaka 2019. Ni semina ambayo itakuwa na maarifa yatakayoleta ukombozi mkubwa sana kwenye maisha yako. Kwani semina hii inakwenda kugusa eneo muhimu sana kwenye maisha yako, eneo ambalo linagusa kila sehemu ya maisha yako ukiacha tu hewa... Continue Reading →

Hivi Ndivyo Unavyoweza Kutumia Majuto Kama Kipimo Cha Kufanya Maamuzi Bora Kwenye Maisha Yako.

Rafiki yangu mpendwa, Kitu kinachojenga au kubomoa maisha yetu, kinachofanya tufanikiwe au kushindwa, ni maamuzi ambayo tunayafanya kwenye maisha yetu. Kila siku tunafanya au kuepuka kufanya maamuzi fulani, na hayo ndiyo yametufikisha pale tulipo sasa. Hapo ulipo leo ni matokeo ya maamuzi ambayo ulifanya au kutokufanya siku zilizopita. Kwa mfano kama hapo ulipo una kipato... Continue Reading →

Taarifa Muhimu Kuhusu Kundi La AMKA MTANZANIA Telegram Na Jinsi Ya Kupata Makala Za Kila Siku Moja Kwa Moja.

Rafiki yangu mpendwa, Kama umekuwa mwanachama na mfuatiliaji wa AMKA MTANZANIA hasa kupitia kundi la Telegram, utakuwa umegundua kwamba kwa siku za karibuni hulioni tena kundi lile. Na wapo ambao wamekuwa wanauliza nini kimetokea mpaka hawapo tena kwenye kundi. Napenda kuchukua nafasi hii kuwataarifu kwamba kundi lile la AMKA MTANZANIA telegram limefutwa. Hii ni kutokana... Continue Reading →

#ONGEA NA KOCHA; Ijue Nafasi Hii Ya Bahati Kwenye Mafanikio Yako Ili Uache Kujidanganya Na Usake Mafanikio Ya Kweli.

Rafiki yangu mpendwa, Nimekuwa nakuambia kwamba kwenye mafanikio, bahati ni pale fursa inapokutana na maandalizi. Kile ambacho watu wa nje wanakiona ni bahati kwa wale waliofanikiwa, huwa hawayaoni maandalizi makubwa ambayo watu hao wamekuwa wameyaweka kwa muda mrefu kabla ya kukutana na fursa hiyo. Lakini pia bado kuna bahati nyingine ambazo huwa zinakutana na kila... Continue Reading →

Leo Ndiyo Siku Ya Mwisho Kabisa Ya Kupata Nafasi Ya Kushiriki Semina Ya Kisima Cha Maarifa 2018 Na Mambo Saba Muhimu Sana Unayopaswa Kuyajua.

Rafiki yangu mpendwa, Kwa zaidi ya miezi mitatu sasa nimekuwa nakupa taarifa za SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2018 ambayo utafanyika tarehe 03/11/2018 jijini dar es salaam. Na ili kupata nafasi ya kushiriki semina hii, unapaswa kuwa umelipa ada ambapo mwisho wa kulipa ada ni leo tarehe 31/10/2018. Nimechukua muda mrefu kukupa taarifa hizi na... Continue Reading →

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑