AMKA MTANZANIA

Chukua Hatua Juu ya Maisha Yako.

VITABU

Karibu kwenye ukurasa wa vitabu vya Kocha Dr Makirita Amani.

Habari rafiki,

Karibu sana kwenye ukurasa huu wa vitabu mbalimbali nilivyoandika kwa ajili yako wewe rafiki yangu, ili uweze kujifunza na kupiga hatua.

Kanuni kuu ya mafanikio ambayo ninaamini inaweza kumsaidia yeyote ni hii; MAARIFA SAHIHI + KUCHUKUA HATUA KUBWA = MAFANIKIO MAKUBWA.

Mimi nimejipa jukumu la kukupa wewe maarifa sahihi, wewe una jukumu la kuyatumia kuchukua hatua kubwa na hapo utaweza kufikia mafanikio makubwa kabisa.

Rafiki, vitabu vyote ninavyotoa ni softcopy, ambapo unaweza kusomea kwenye simu yako, kama unavyosoma hapa, unaweza kusomea kwenye tablet na pia unaweza kusomea kwenye kompyuta yako.

Vitabu vyote vinatumwa kwa njia ya email, hivyo unaweza kupata popote unapokuwa, huna haja ya kwenda popote ili kuvipata. Unachohitaji ni kuchagua kitabu, kulipia, kisha kutuma email na unatumiwa kitabu chako.

Vifuatavyo ni vitabu vinavyopatikana kwa ajili yako.

  1. KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI; Sababu 25 kwa nini watu wengi wanaendelea kuwa masikini.

Hichi ni kitabu kinachokupa msingi muhimu wa kifedha na kuondoka kwenye masikini.

Kitabu kinauzwa tsh elfu tano (5,000/=).

  1. JINSI YA KUFAIDIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA KWENYE MAISHA.

Maisha yanabadilika, iwe unataka au hutaki. Watu wengi wamekuwa wanachelewa mabadiliko kwa sababu hawayaoni haraka. Soma kitabu hichi uweze kuyaona mabadiliko na kuchukua hatua kabla hujaachwa.

Kitabu kinauzwa tsh elfu tano (5,000/=).

  1. JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG.

Tunaishi kwenye zama za taarifa, ambapo wenye taarifa sahihi na wanaoweza kuzitumia ndiyo wanaopiga hatua. Kitabu hiki kinakupa maarifa ya kuweza kutumia mtandao wa intaneti kutengeneza kipato ukiwa hapo ulipo sasa.

Kitabu hichi kinauzwa tsh elfu kumi, (10,000/=).

  1. KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO.

Hichi ni kitabu chenye kurasa za idadi ya siku za mwaka mmoja. Ni kitabu ambacho kila siku unapata nafasi ya kusoma ukurasa mmoja na kuwa na kitu cha kufanyia kazi ili kuwa na maisha ya mafanikio.

Kitabu kinauzwa tsh 10,000/=

  1. MIMI NI MSHINDI, Ahadi yangu na nafsi yangu.

Kila mtu amezaliwa kushinda, lakini wengi wameandaliwa kushindwa. Ili kudai ushindi uliopo ndani yako, unahitaji sana maarifa ya kitabu hiki. Unapaswa kusoma kitabu hiki kama unataka mafanikio makubwa kwenye maisha yako.

Kitabu kinauzwa tsh 10,000/=

  1. BIASHARA NDANI YA AJIRA, Anzisha na kuza biashara yako ukiwa umeajiriwa.

Watu wengi wanasingizia kwamba ajira haziwalipi vizuri na ndiyo sababu maisha yao ni magumu.

Hii siyo sahihi, hata kama ajira yako haikulipi, bado una nafasi ya kuongeza kipato chako kwa kuanzisha biashara ukiwa bado umeajiriwa.

Soma kitabu hiki na utaweza kupata mafunzo ya kuanzisha na kukuza biashara yako ukiwa kwenye ajira.

Kitabu kinauzwa tsh 10,000/=

7. PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU.

Kila mtu analalamika kwamba hana muda wa kutosha, lakini tatizo halijawahi kuwa muda, tatizo ni jinsi tunavyotumia muda tulionao. Kwenye siku yako unayoona upo bize, unaweza kupata masaa mawili ya ziada ambayo utaweza kuyatumia kufanya yale muhimu kwako.

Soma kitabu hichi na utaweza kupata muda wa kufanya yale muhimu kwako.

Kitabu kinauzwa tsh 5,000/=

8. IJUE BIASHARA YA MTANDAO (NETWORK MARKETING)

Biashara ya mtandao ni moja ya mapinduzi makubwa sana kwenye ufanyaji wa biashara, ambayo inamwezesha yeyote kumiliki biashara kubwa kwa kuanza kidogo.

Lakini siku za hivi karibuni, kumekuwa na makampuni mengi ya kitapeli ambayo yanatumia mgongo wa biashara hii kujinadi.

Kabla hujashawishika kujiunga na biashara yoyote ya mtandao (NETWORK MARKETING) unapaswa kusoma kitabu hiki, kitakusaidia kuepukana na utapeli.

Kitabu kinauzwa tsh 5,000/=

 

JINSI YA KUPATA VITABU HIVI.

Ili kupata kitabu chochote kati ya hivi, unahitaji kutuma fedha ya malipo ya kitabu au vitabu ulivyochagua.

Namba za kulipia ni MPESA 0755 953 887, TIGO PESA/AIRTEL MONEY 0717 396 253 majina ya namba hizo ni AMANI MAKIRITA.

Ukishatuma fedha, tuma ujumbe mfupi kwenda kwenye namba 0717396253 wenye jina la kitabu au vitabu ulivyolipia na email yako, kisha utatumiwa vitabu kwenye email yako.

Karibu sana upate maarifa sahihi, na uyatumie ili kuweza kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.

Rafiki na Kocha wako,

Dr. Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha

%d bloggers like this: