KWA NINI UNAFANYA KAZI KWA BIDII NA MAARIFA LAKINI BADO HUFANIKIWI?

  Hakuna anaeweza kubisha kwamba kufanya kazi kwa bidii na maarifa ndio msingi wa mafanikio. Lakini umekuwa unafanya hivyo na bado hupati mafanikio na wala huoni mwelekeo wowote wa kuyapata. Unajua tatizo liko wapi? Kwanza lazima ujue sio  kila kitu kinaweza kufanyika kwenye kila mazingira. Namaanisha inawezekana unachofanya hakiwezi kufanyika kwenye mazingira unayofanyia ama kwa njia unayofanyia. Hivyo basi kama unaona umeweka juhudi zako zote na maarifa yako yote na bado huoni mwelekeo ni vyema ukatafakari tena upya na ukafanya upembuzi yakinifu. Katika upembuzi huo angalia katika vyote unavyofanya ama umewahi kufanya ni vipi vimekuletea majibu mazuri na vipi havikukupatia majibu uliyotarajia.
  Ongeza juhudi na maarifa kwenye vile vitu vinavykupatia majibu mazuri. Vifanye kwa ubunifu zaidi na kwa kiwango kikubwa ili kuweza kupata matokeo makubwa, mazuri. Acha kufanya vitu ambavyo havikupatii majibu uliyokuwa unatarajia, badala yake tumia huo muda kufanya vile vinavyokupatia majibu mazuri. Huwezi kufanya kila kitu ila kuna baadhi ya vitu unaweza kuvifanya vizuri zaidi kuliko watu wengine. Vitambue vitu hivyo na uanze kuvifanya mara moja ili kufikia malengo yako.
  Kwa kutumia muda kidogo kufanya upembuzi yakinifu wa maisha yako na yale unayyafanya kunakusaidia mambo hayo makuu mawili. Kujua mambo ambayo ukiyafanya unapata majibu mazuri kulingana na malengo yako na kuokoa muda unaopoteza kufanya mambo ambayo hayakupatii majibu mazuri. Hivyo unaweza kuutumia muda huo kuongeza tija kwenye mambo yanayokupatia majibu mazuri.

  Hakikisha unafanya upembuzi yakinifu ikiwa ni pamoja na kuwauliza watu wako wa karibu kama huna uhakika ni kitu gani unaweza kufanya vizuri zaidi. Wakati mwingine unaweza kuwa njia panda usijue ni lipi unalifanya vizuri sana, ila ukimuuliza mtu anaekujua vizuri unaweza kupata picha ni jinsi gani wanavyoona kazi ama mambo yako. Usiamue tu kuacha kufanya jambo kwa sababu halikupatii majibu unayotaka, fanya upembuzi ili kujua kama kweli halifanyiki kwenye mazingira unayofanya ama hujajua njia bora ya kulifanya.

TAFADHALI WEKA MAONI YAKO HAPO CHINI KWA LOLOTE UNALOFIKIRI KUHUSIANA NA MADA HII. USIONDOKE BILA KUSEMA CHOCHOTE, MAONI YAKO NI YA MUHIMU SANA KWETU.
KAMA UMEIPENDA HII MADA TAFADHALI BONYEZA KIALAMA CHA FACEBOOK NA TWITTER KUSHOTO KWAKO KUWASHIRIKISHA RAFIKI ZAKO WA FACEBOOK NA TWITTER ILI UJUMBE HUU UWEZE KUWAFIKIA NA KUWABADILI WENGI. ASANTE SANA KWA USHIRIKIANO WAKO

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: