MASWALI MATATU MUHIMU YA KUJIULIZA KABLA HUJAJIAJIRI

  Hakuna anebisha kwamba ajira zimekuwa ngumu sana katika zama hizi. Makampuni na taasisi mbalimbali zinapunguza wafanyakazi kila kunapokucha. Wahitimu ni wengi na nafasi za ajira ni chache. Ajira zimekuwa ngumu kupatikana na walioko kwenye ajira wengi mambo yao sio mazuri sana.

  Hayo yote yanapelekea kujiajiri kuwa kimbilio pekee la wengi wanaomaliza elimu, wanaopunguzwa makazini na wanaozichoka kazi na kuamua kuondoka wenyewe. Pamoja na kujiajiri kuwa ndio kimbilio bado wengi wetu hatujajipanga vya kutosha tunapoingi kwenye sekta hii.

  Wapo wengi waliojiajiri na bado hawana tofauti kubwa na walioajiriwa, na wengine mambo yao ni magumu zaidi hata ya walioajiriwa. Wako wengi walioshindwa kabisa na kuamua kuacha kujiajiri na kukubali kulipwa hata kiwango kisichotosheleza mlo kamili ili japo maisha yendelee.

  Kama umejiajiri na mambo yako sio mazuri na unakaribia kukata tamaa, ama umeshakata tamaa na kuacha kujiajiri kuna vitu ulikuwa hujavijua ambavyo kwa kuvijua hapa leo vitakupatia mtizamo tofauti. Kama unampango wa kujiajiri utapata mtizamo mzuri wa kwenda kufanya kile unchotaka kufanya.

jiulize4

  Kabla hatujayaona maswali matatu ya kujiuliza kabla ya kujiajiri, tuangalie baadhi ya sababu zinazopelekea watu kushindwa kwenye kujiajiri.

1. Tabia, (soma; kama una tabia hii usijiajiri kabla hujabadili)

2. Kutokujua lengo la ajira(soma; usichokijua kuhusu ajira)

3. Kutojua tofauti ya kuajiriwa, kujiajiri na kutokuwa kwenye ajira kabisa(soma; kuajiriwa, kujiajiri na kutokuwa kwenye ajira kabisa)

  Pamoja na sababu hizo tatu, kuna maswali matatu muhimu sana ya kujiuliza ili kuweza kufanikiwa kwenye kujiajiri. Hata kama umeajiriwa na unataka kupata mafanikio makubwa kupitia ajira yako ni vyema ukajiuliza mwaswali haya na kuyajibu kwa usahihi.

  Maswali haya yamelenga kujitambua hivyo ni vyema kila mtu ukajiuliza ili kujua mwelekeo wako katika maisha.

 

  Swali la kwanza; WEWE NI NANI? Hilo ni swali muhimu la kujiuliza ili kujijua vizuri. Sio swali rahisi hata kidogo, ukijibu kwamba MIMI NI MAKIRITA(kwa jina lako), basi ni vigumu sana kufanikiwa kwa jambo la kujisimamia mwenyewe. Ni vyema ukaenda kwa bosi wako na akakuambia wewe ni nani na maisha yako yakaishia hapo. Unapoajiriwa unaambiwa wewe ni nani, unaajiriwa kuwa afisa masoko, karani, muuzaji, mjenzi na kadhalika. Kwa kutojua wewe ni nani ni sababu kubwa kushindwa kufikia malengo yako hasa kwenye kujiajiri.

jiulize3

 

  Swali la pili; KWA NINI UKO HAPO ULIPO? Kuna sababu imefanya uwe hapo ulipo na kufanya unachofanya. Kwa kuijua sababu hiyo ni rahisi sana kwa wewe kufanikiwa na kufanya vizuri zaidi. Unapoajiriwa mwajiri wako anajua uko pale kumfanyia kazi, wakati wewe unaweza kuwa unajua ama hujui sababu ya wewe kuwepo.

  Swali la tatu; MAISHA YAKO YANA MAANA GANI? Kama ulikuwa hujui, maisha yoyote hapa duniani yana maana, na kuijua maana ya maisha yako inarahisisha kuyaboresha na kuyafurahia. Maisha yako yana maana kubwa kwako na kwa wanaokuzunguka kwa kutoijua maana hiyo anaekuajiri atakuambia maana ya maisha yako ni kutumikia ajira mpaka utapofika miaka sitini kisha utapewa mafao kidogo kidogo huku ukisubiri kufa.

 

   Majibu ya maswali hayo matatu unayo wewe mwenyewe, hakuna anaeweza kukusaidia kuyajibu. Usijaribu kuyajibu kwa pupa, kaa chini yatafakari maisha yako kisha jiulize hayo maswali na upate majibu sahihi. Yaandike majibu hayo ili uweze kuyapitia mara kwa mara na uyaboreshe maisha yako.

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: