Baada ya kufanyika kwa semina kubwa ya kubadili maisha tarehe 18/01/2014 pale ubungo plaza, AMKA MTANZANIA imeandaa mafunzo mengine kwa njia ya mtandao.

  Mafunzo hayo yamelenga kubadili maisha ya washiriki kwa kiasi kikubwa kwa mwaka huu 2014. Kila atakayepata mafunzo haya na kuyaweka kwenye vitendo ni lazima atafikia mafanikio makubwa kwa mwaka huu na mingine ijayo.

                 2014 malengo

  Kwa kuwa mafanikio yote huanzia kwa kuwa na malengo na mipango mizuri mafunzo haya yatajikita kwenye namna bora ya kuweka malengo na mipango ambayo ni lazima utaifikia. Hakuna anayeweza kubeza umuhimu wa malengo katika jambo lolote analofanya kwenye maisha(soma;ni muhimu sana kuweka malengo)

  Mafunzo haya yatatolewa kwa njia ya email kwa siku tano mfululizo. Mafunzo yatafanyika mara moja tu na yataanza jumatatu tarehe 27/01/2014 mpaka ijumaa tarehe 31/01/2014. Kila mshiriki atatumiwa email moja kwa siku iliyochambuliwa na kuelezwa vizuri sana somo husika. Mshiriki ataweza kuuliza swali kwa kujibu email au kupiga simu. Pia mshiriki atakuwa akipewa maswali machache ili kujua kama anafuatilia mafunzo vyema.

  Mafunzo yatatolewa hivi;

1. Jumatatu; Umuhimu wa kuweka malengo na lengo kuu la maisha ambalo kila mtu analipigania, hata wewe.

2. Jumanne; Aina tano za malengo unayotakiwa kuweka kwenye maisha yako.

3. Jumatano; Hatua saba za kuweka malengo ambapo lazima utayafikia.

4. Alhamisi; Makosa makubwa unayoyafanya na ambayo umekuwa ukiyarudia unapoweka malengo na jinsi ya kuyaepuka.

5. Ijumaa; Unafanya nini baada ya hapa? Unaanzia wapi?

  Gharama ya mafunzo ni tsh 10,000?= na italipwa kwa njia ya Mpesa(0755953887), Tigo pesa(0717396253) ama njia nyingine kwa walioko nje ya nchi. Kama unataka kushiriki mafunzo haya tuma email kwenda amakirita@gmail.com kisha utapewa utaratibu wa malipo na mengine mengi kuhusu mafunzo haya.

  Mwisho wa kujiunga na mafunzo haya ni ijumaa tarehe 24/01/2014 baada ya hapo hakutakuwa na nafasi ya kujiunga tena. Kumbuka mafunzo haya yatafanyika mara moja tu na hayatarudiwa tena.

  Karibu kwenye mafunzo ambayo yatabadili maisha yako kwa kiasi kikubwa mwaka huu 2014.

  Nakutakia kila la kheri kwa mwaka huu na bado tupo pamoja.