Siku 61 Zimekufikisha Wapi?

  Kidogo kidogo mwaka unachanja mbuga, ni juzi tu tulisherekea mwaka mpya ila sasa tuko mwezi wa tatu. Leo ni siku ya 62 kwenye mwaka huu 2014, tumeshamaliza siku 61.

  Swali langu kwako ni je siku hizo 61 zimekufikisha wapi? Je umefanya nini kwenye siku hizo 61?

  Nakumbuka mwanzoni mwa mwaka huu ulikuwa ukisema mwaka huu ni wa mabadiliko kwako na utafanya mambo makubwa! Je bado unasema hivyo au ulikuwa unasema kwa sababu kila mtu alikuwa anasema? Je kuna chochote ulichofanikisha mpaka kufikia sasa?

kitabu kava tangazo

  Tafiti zinaonesha kwamba asilimia 90 ya watu wanakuwa wameshasahau malengo waliyojiwekea siku 60 baada ya kuyaweka. Na watu hawa ndio wanaoshindwa kufanikiwa kwenye jambo lolote wanalofanya. Asilimia chache sana ya watu wanakuwa bado wanakumbuka na kufuata malengo yao hata baada ya siku 60 kupita.

  Je wewe uko upande gani? Hebu leo tenga muda na ujiulize na kujibu maswali hayo. Andika yale ambayo mpaka sasa umekwisha fanikisha na pia angalia ni yapi ulipanga mpaka sasa uwe umekamilisha ila umeshindwa. Pia jua ni sababu zipi zilizokuzuia wewe kushindwa kukamilisha mipango hiyo mpaka sasa.

  Kama bado unakumbuka na kufuata malengo yako hongera sana kwani upo kwenye njia sahihi ikupelekayo kwenye mafanikio. Kama umeshasahau malengo uliyojiwekea hongera sana kama unasoma hapa. Nakupa hongera kwa sababu leo utakuwa mkweli na kuweka malengo yako wewe na sio kufuata mkumbo kama ulivyofanya mwanzoni mwa mwaka.

  Kama mpaka sasa mambo yako hayaendi vizuri usikate tamaa na kusema mwaka huu umeshaushindwa hivyo unasubiri mwaka mwingine. Kama tukiugawa mwaka kwenye ng’we sita ndio kwanza tumemaliza ng’we ya kwanza, hivyo tuna ng’we nyingine tano za kwenda ndio mwaka huu uishe.

  Kama umeshayasahau malengo yako au hukuweka malengo kabisa anza sasa. Usiseme kwamba umechelewa, hakuna kuchelewa bali kuna kujitambua.

Fungua sehemu yenye makala za malengo kwenye mtandao huu kisha usome makala mbalimbali zinazoeleza jinsi ya kuweka malengo, jinsi ya kuepuka makosa unayofanya wakati wa kuweka malengo na hasara unazopata kwa kutoweka malengo. Kufungua sehemu hiyo na kusoma makala hizi bonyeza maandishi haya.

  Kama unataka mwaka huu 2014 uzidi kuwa mwaka wa mabadiliko kwako pata kitabu KWA NINI MPAKA SASA WEWE NI MASIKINI. Kitabu hiki kitakufanya ujue sababu ishirini na tano zinazokuzuia wewe kuwa tajiri. Kitakuonesha makosa makubwa unayofanya kila siku yanayosababisha uendelee kuwa masikini. Kupata kitabu hicho bonyeza maandishi haya.

Bado unao muda wa kutosha kuendelea na mabadiliko mwaka huu 2014. Kama ulipitiwa kidogo na kutoka nje ya malengo yako rudi sasa na uendelee kuyafuata. Unastahili kupata mafanikio makubwa kwenye hicho unachofanya, hakuna wa kukupa au kukunyima, wewe pekee ndiye mwenye mamlaka hayo.

  Nakutakia kila la kheri.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s