Je ni lazima wote tuwe matajiri?

  Wakati natoa taarifa ya kitabu nilichoandika kinachoitwa KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIO TAJIRI, kuna baadhi ya watu waliniuliza swali hilo kwamba je ni lazima wote tuwe matajiri? Na wengine walikuwa na swali kama hilo ila waliuliza kwa njia nyingine. Kwa hiyo swali la msingi hapa ni je lazima wote tuwe matajiri?

kitabu kava tangazo

  Huenda na wewe una swali kama hilo, huenda unasita kukitafuta kitabu hiki kwa sababu umeshajiaminisha kwamba wewe huna haja ya kuwa tajiri kwa sababu maisha yako yanajitosheleza. Ila kabla hujajumuisha hivyo hebu tuangalie vizuri utajiri ni nini na kama kuna ulazima wowote wa wewe kuwa tajiri.

  Walioniuliza swali hilo niliwajibu sio lazima ila pia sio vibaya kuwa tajiri. Kwenye nafsi yangu nahisi sikuwapa jibu sahihi. Baada ya kufikiri maisha yetu binadamu kwa kina na pia baada ya kufikiri niliyoandika kwenye kitabu nimepata jibu kwamba NI LAZIMA KUWA TAJIRI na hata kama hutaki UNALAZIMISHWA KUWA TAJIRI.

  Katika dunia ya sasa ambayo thamani ya kila kitu inapimwa kwa kiwango cha fedha huna jinsi zaidi ya kutafuta fedha zaidi. Dunia ya sasa inawatenga matajiri na masikini wazi wazi kuanzia vyakula wanavyokula, mavazi wanayovaa na hata huduma muhimu wanazopata kama afya na elimu.

  Ni nani ambaye hapendi kula vizuri na kwa afya? Ni nani ambaye hapendi kupata elimu bora na hataki watoto wake wapate elimu bora? Ni nani ambaye hapendi kukaa kwenye nyumba bora na yenye hadhi ya kuishi binadamu? Ni nani ambaye hapendi akipata matatizo ya kiafya atibiwe kwenye hospitali bora na yenye huduma nzuri? Yote haya tunayatamani sana ila wengi tunayakosa. Kwa sababu gani tunayakosa? Kwa kuwa ni masikini au kwa lugha nyingine sio tajiri.

  Kwa namna moja au nyingine tunahitaji kuwa tunajitosheleza kifedha, na hata kama hatutaki kasi na mitindo ya maisha itatulazimisha kutafuta fedha zaidi ili tuweze kujitosheleza kifedha.

  Nimeandika kitabu hiki baada ya kuona jinsi watu wengi tunavyoteseka kuzipata fedha. Watu wanafanya kazi nyingi na ngumu ila wanaishia kupata fedha kidogo ambazo hazitoshelezi hata mahitaji yao. Watu wanakopa fedha sehemu nyingi mpaka baadae maisha yao yanakuwa ni ya kulipa madeni. Watu wanatembea ila kiuhalisia walishakufa na hawana tena ndoto kubwa.

  Kwa nini yote haya yanatokea? Kwa sababu hakuna sehemu ambapo tunapewa darasa hili la kuwa matajiri. Tunaishia kufundishwa vitu vingi ambavyo havina msaada kwenye maisha yetu ila tunanyimwa elimu hii muhimu.

  Katika hali hii ndipo unapohitaji kupata kitabu hiki ili uanze kuyabadili maisha yako. Utajiri ninaozungumzia kwenye kitabu hiki hauna kipimo. Hivyo unaweza kuwa tajiri wa kujitosheleza wewe binafsi au ukawa tajiri mkubwa sana hapa nchini na hata nje ya nchi. Lengo kubwa ni kwamba tufike mahali tunaishi maisha tunayoyafurahia zaidi ya kuishi maisha ambayo kila wakati tunahofu kuhusu fedha.

  Pata kitabu hiki, kisome na anza kutumia mafundisho yake kwenye maisha yako ili uondoke kwenye umasikini na ufikie utajiri au kujitosheleza.

  Kuna mengi sana ya kujifunza kwenye kitabu hiki ambayo siwezi kuyaelezea hapa hata kwa kufupisha. Pata kitabu hiki na uanze kuyabadili maisha yako.

  Kupata kitabu hiki bonyeza maandishi haya na ufate maelekezo.

  Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya mafanikio. Kumbuka tuko pamoja kwenye safari hii na tutafika tukiwa washindi.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: