Ugonjwa Mkubwa Unaotusumbua Tanzania Sio Ukimwi Wala Malaria Ni Huu hapa.

Kwenye nchi zinazoendelea Tanzania ikiwemo magonjwa ya kuambukizwa yameonekana kuwa ndio tishio sana kwa afya za wananchi. Magonjwa kama ukimwi, malaria, TB, kichocho, kipindupindu na homa za matumbo yamekuwa yakisumbua sehemu kubwa ya watu katika nchi hizi.

  Ili kuokoa afya za wananchi serikali za nchi hizi zinazoendelea zimekuwa zikiweka mipango kabambe ya kupambana na magonjwa haya. Mipango mingi iliyowekwa imefanikiwa ila sio kwa kiwango kikubwa sana. Hii ni kwa sababu kuna ugonjwa mwingine mkubwa zaidi ya magonjwa haya ya kuambukizwa unaosumbua wananchi.

  Kabla hatujaangalia ugonjwa huo hebu tuangalie tofauti kati ya mataifa yenye magonjwa ya kuambukizwa na yale ambayo hayana kwa kiwango kikubwa. Ukiangalia kwa makini utagundua kwamba mataifa yanayosumbuliwa sana na magonjwa ya kuambukizwa ni mataifa ambayo watu wake ni masikini sana. Na hata ndani ya taifa sehemu ambazo magonjwa haya yameshamiri ni sehemu ambazo watu ni masikini. Nina hakika unajua kipindupindu huwa kinatokea maeneo gani sana sana.

              MINOLTA DIGITAL CAMERA

  Kwa mantiki hii basi ugonjwa mkubwa unaoisumbua nchi yetu sio ugonjwa wa kuambukiza bali ni umasikini. Umasikini ndio ugonjwa mkuu ambao unapoteza maisha ya wananchi wengi. Umasikini ndio ugonjwa mkubwa unaofanya maisha ya wananchi wengi kuwa magumu. Na kwa kuwa kwenye mipango ya kupambana na magonjwa umasikini haujawekwa, basi hakuna anayefunguka macho kuuangalia.

                umaskini

  Ni umasikini unaofanya wengi kufanya ngono zembe na wakati mwingine ukahaba na kujikuta wanaambukizwa magonjwa ya zinaa na ukimwi. Ni umasikini unaofanya watu wakose maji safi na salama na kuishia kutumia maji machafu yanayowasababishia magonjwa ya tumbo na minyoo. Na ni umasikini unaofanya watu kukosa elimu na hivyo kushindwa kujikinga na magonjwa yanayoweza kuzuilika.

Tunawezaje kutokomeza ugonjwa huu?

  Kwa kuwa ugonjwa huu hauko wazi basi serikali haijaweka mikakati ya kupambana nao au kuutokomeza. Hata baadhi ya mipango mingi iliyowahi kuwekwa kupambana na ugonjwa huu haikuzaa matunda yaliyotarajiwa na mwishowe kufa.

  Mipango mingi imeshindwa kwa sababu serikali imekuwa ikiangalia sehemu isiyohusika kwenye kupambana na ugonjwa huu. Huwezi kuondoa umasikini kwa kutegemea misaada. Misaada haiondoi bali inaongeza umasikini.

  Njia pekee ya kuondoa umasikini ni kuwajengea watu uwezo wa kufanya kazi yenye manufaa kwa watu wengine. Kuzalisha bidhaa au huduma zinazohitajika na watu wengine hivyo kutengeneza biashara kwa ngazi ya kitaifa na baadae kitaifa.

  Serikali ingepaswa kuwajengea watu uwezo wa kuajiriwa, kujiajiri na kufanya biashara. Na kwa kuwa kuajiriwa nafasi hazitoshi basi kujiajiri na biashara ni njia nzuri za kupambana na ugonjwa huu. Kwa kuwa serikali haifanyi hivi je wewe unalala?

  Usilale, tulishakubaliana kwamba usimlaumu yeyote, AMKA na chukua hatua juu ya maisha yako. Jijengee uwezo wa kujiajiri na kufanya biashara ili uweze kuutokomeza ugonjwa huu mbaya kwako, kwa familia yako na kwa jamii inayokuzunguka. Kama watu wachache tutachukua hatua hii baadae itasambaa na kufanyika na watu wanaotuzunguka na hatimaye taifa zima.

Unawezaje kujijengea uwezo?

  Katika mtandao huu wa AMKA MTANZANIA tumeshajadili njia nyingi sana za kujijengea uwezo kwa kujifunza na kuchukua hatua. Anza kuzitumia njia hizi kwenye kazi na biashara zako na utaona mabadiliko makubwa. Kama wewe ni mgeni kwenye mtandao huu endelea kusoma makala nyingi utakutana na mawazo mengi juu ya kuchukua hatua na kubadilika.

  Ili uweze kujiondoa kwenye ugonjwa huu wa umasikini inabidi ujue ni nini kinakufanya mpaka sasa unateseka na ugonjwa huo. Kwa kujua sababu itakuwa rahisi kwako kupambana nazo na hatimaye kushinda. Unaweza kuzijua sababu hizo kwa kusoma kitabu KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIO TAJIRI. Kupata kitabu hiko bonyeza maandishi hayo.

  Njia kubwa ya kupambana na ugonjwa huu wa umasikini ni kujijengea uwezo. Na njia bora ya kujijengea uwezo ni kujifunza na kuchukua hatua ya kutekeleza yale unayojifunza. Kama unataka kujifunza zaidi juu ya biashara na mambo mengine jiunge na kisima cha maarifa na uchote maarifa yatakayokusaidia. Kujiunga na kisima cha maarifa bonyeza maandishi haya.

  Kuanzia sasa jua ugonjwa namba moja unaotakiwa kupambana nao ni umasikini na usifikiri msaada utakusaidia kuondokana na umasikini.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: