Kitabu; Rich Dad, Poor Dad.

  Katika utaratibu wa kutuma vitabu leo nakutumia kitabu Rich Dad, Poor Dad kilichoandikwa na Robert Kiyosaki. Katika kitabu hiki Robert ameelezea masomo aliyojifunza kutoka kwenye malezi ya baba yake ambaye alikuwa msomi lakini masikini na malezi kutoka kwa baba wa rafiki yake ambaye alikuwa sio msomi ila tajiri.

  Katika kitabu hiki Robert ameelezea jinsi gani mfumo wa elimu unatengeneza watu kuwa waajiriwa. Pia anaeleza ni kwa nini wanafunzi wanaofaulu sana darasani wanakuwa wafanyakazi wa wale ambao hawana elimu kubwa au hawakufaulu sana.

rich dad

  Nakiona kitabu hiki kama daraja la kuunganisha elimu ya darasani na elimu ya mtaani na mafanikio kwenye maisha. Kwa kuwa na elimu ya darasani pekee imeshadhibitisha kuwa vigumu sana kuchangamana na mtaa, kama ilivyo kwenye tatizo la ajira, kuna umuhimu wa kuwa na elimu hii mbadala.

  Kuna mambo mengi sana unaweza kujifunza kwenye kitabu hiki, hapa naweka kumi ambayo ni muhimu kuyajua.

1. Kwa watu wengi taaluma yao ndio kipato chao, ila kwa matajiri mali zinazozalisha(assets) ndio kipato chao.

2. Mapato ya ziada yanayopatikana kwenye uwekezaji inabidi yatumike kuwekeza zaidi.

3. Watu wengi wanaifanyia kazi fedha ila kwa matajiri fedha inawafanyia kazi wao kupitia uwekezaji.

4. Ni muhimu kuwa na uelewa kidogo kwenye nyanja nyingine utakaokusaidia kwenye biashara na uwekezaji. Ni muhimu kujua kuhusu biashara, sheria, kodi, mauzo na masoko, uongozi na uwekezaji.

5. Ni muhimu ujifunze uwekezaji kabla hujawekeza.

6. Watu matajiri wamepoteza fedha nyingi sana kwenye safari yao ya kufikia utajiri, masikini wanalinda sana fedha zao zisipotee.

7. Dhibiti hisia zako, usikubali kuendeshwa na woga au maoni ya watu wengine. Fanya maamuzi ya biashara au uwekezaji kutokana na mipango yako.

8. Zungukwa na watu ambao wana akili kushinda wewe, hii itakusaidia kufikiri zaidi na kupata mawazo mengi.

9. Jilipe wewe kwanza. Kila kipato unachopata kuwa na kiwango fulani unachojilipa wewe. Usiweke akiba fedha inayobaki baada ya matumizi bali tumia fedha inayobaki baada ya kuweka akiba.(soma; unamlipa kila mtu kasoro huyu mmoja wa muhimu)

10. Kwenye soko usijaribu kufanya kile ambacho kila mtu anafanya, usifuate kundi. Faida inapatikana wakati unanunua na sio wakati unauza.

  Kuna masomo mengi sana kuhusu maisha, biashara na uwekezaji unayoweza kujifunza kwenye kitabu hiki.

  Kitabu hiki kimutumwa kwa watu ambao wako kwenye mtandao wa AMKA MTANZANIA. Kama unataka kupata kitabu hiki na haupo kwenye mtandao huu tafadhali maandishi haya kisha uweke email yako, ukishakamilisha utatumiwa email yenye link ambapo utadownload kitabu hiki. Hakuna gharama yoyote ni bure kabisa.

  Kitabu hiki ni kifupi sana kina kurasa 130 tu hivyo kama una uvivu wa kusoma huwezi kushindwa kumaliza kitabu hiki.

  Nakutakia kila la kheri.

One thought on “Kitabu; Rich Dad, Poor Dad.

Add yours

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: