Kama tulivyoona kwenye makala zilizopita, ili kuweza kuanzisha na kukuza biashara ni muhimu sana kutengeneza thamani. Ni muhimu kutengeneza kitu ambacho watu wanakihitaji na wana uwezo wa kulipia bei unayouza ili kukipata kitu hicho. Katika kuanzisha biashara ubunifu mkubwa unahitajika ila huna haja ya kubuni kitu ambacho haipo kabisa kwenye mazingira ama dunia ya sasa.
maarifa
Katika mazingira yoyote kuna njia kumi na mbili za kutengeneza thamani, hapa namaanisha kuna njia kumi na mbili za kuweza kuanzisha biashara ambayo itakua sana kama utajipanga vizuri. Zisome njia hizi kisha angalia ni ipi unaweza kuitumia na kisha jifunze zaidi kuhusu njia hiyo.
1. Kutengeneza bidhaa.
Hapa unatengeneza bidhaa inayoonekana ama kutumika na kuiuza kwa watu wengine. Katika aina hii ya biashara unatakiwa kutengeneza bidhaa yako kwa gharama ndogo na baadae kuuza kwa bei ya juu kidogo ukilinganisha na gharama uliyotengenezea, hapo ndipo unapoweza kutengeneza faida.
Uzuri wa biashara ya bidhaa ni kwamba baadhi ya bidhaa unaweza kutengeneza mara moja tu na baada ya hapo ukawa unazalisha bidhaa nyingine kutoka kwenye hiyo moja.
2. Kutoa Huduma.
Hii ni biashara ambapo unamsaidia mtu na yeye anakulipa fedha. Ili kuweza kutengeneza biashara ya kutoa huduma inabidi uwe na ujuzi au uzoefu ambao watu wengine hawana ila wanahitaji sana. Kwa njia hii wanakuwa tayari kukupa fedha ili kunufaika na huduma yako. Huduma za ushauri, bishara za saluni, huduma za afya ni baadhi ya biashara ambazo zinatoa huduma muhimu kwa watu.
3. Vitu vinavyotumika na watu wengi.
Hii ni biashara ambapo mtu ananunua au kutengeneza vitu ambavyo vinaweza kutumika na watu wengi kwa wakati mmoja au kwa kubadilishana. Aina hii ya biashara inahitaji uwekezaji mkubwa mwanzoni ila baada ya hapo mmiliki anakuwa anakusanya mapato makubwa. Biashara kama sehemu za kufanyia mazoezi(gym club) au sehemu za burudani kama fukwe zilizotengenezwa vizuri ni mifano ya aina hii ya biashara.
4. Kujisaliji/kujiunga.
Hii ni aina ya biashara ambapo wateja wanajisajili kupata huduma fulani kwa kipindi fulani na kulipia usajili wao. Ili kutengeneza biashara ya aina hii ni muhimu mtu kuwa na huduma ambayo watu wanaihitaji na kuiboresha kadiri ya siku zinavyokwenda. Ili kukuza biashara hii ya kujisajili ni muhimu kwa mfanyabiashara kushawishi watu wengi zaidi kujisajili/kujiunga na biashara hiyo. Huduma za ving’amuzi vya tv ni mfano wa biashara hii. Kila mwezi unalipa ada fulani ili kuweza kuona chanel nzuri za tv.
KISIMA CHA MAARIFA pia ni aina hii ya biashara ambapo ulilipia ili kujiunga na mtandao huu ambao unakupa maarifa mbalimbali ya kukunufaisha kwenye maisha.
  Kuendelea kusoma aina nyingine nane za kutengeneza thamani kwenye biashara tafadhali jiunge na kisima cha maarifa. Kujiunga na kisima cha maarifa tafadhali bonyeza maandishi haya kupata taarifa zaidi kuhusu na kisima cha maarifa.