Naomba Ushirikiano Wako Kuiboresha AMKA MTANZANIA.

Mtandao wa AMKA MTANZANIA umefikisha mwaka mmoja tangu uanzishwe. Katika mwaka huu mmoja mtandao huu umeweza kuwafikia watu wengi na kubadili maisha ya watu wengi.

  Mafanikio haya ya AMKA MTANZANIA yametokana na wewe msomaji kusoma makala na kuchukua hatua. Pia kuwashirikisha watu wengine kumekuwa na mchango mkubwa katika ukuaji wa mtandao huu.

tanzania nakupenda

  Ili kuboresha makala na mafunzo yanayotolewa hapa AMKA MTANZANIA napendelea kupata picha ya wasomaji wakuu wa mtandao huu. Picha hii itanisaidia kuandaa makala na mafunzo yanayoendana na matatizo ambayo wengi wa wasomaji wanayapitia.

  Ili kupata picha hii nimeandaa utafiti mfupi sana wenye maswali kumi tu ambayo yatatoa picha ya wasomaji wa amka mtanzania. Tafadhali sana naomba ujibu maswali haya mafupi kumi ili usaidie kuboresha shughuli za AMKA MTANZANIA.

  Maswali ya utafiti huu yamelenga kujua wasifu wa msomaji kama eneo analotokea, umri, elimu na shughuli anazofanya. Tafadhali usione aibu kuweka jibu la kweli kwa sababu hakuna atakayejua majibu yako. Hakuna sehemu yoyote kwenye utafiti huu ambapo utaweka jina lako. Hivyo majibu yako ni siri na hakuna atakayejua nani kasema nini. Lengo ni kupata picha ya pamoja ya wasomaji.

  Tafadhali bonyeza maandishi haya ya UTAFITI MFUPI KUJUA WASOMAJI WA AMKA MTANZANIA na ukamilishe utafiti huu.

  Tafadhali nakuomba sana wewe kama msomaji usiache kukamilisha utafiti huu. Utakuwa na msaada mkubwa kwetu sote katika kufikia malengo yetu.

  Asante sana kwa kendelea kuwa msomaji wa AMKA MTANZANIA.

  Tuko pamoja.

Kama hujajibu maswali haya ya utafiti tafadhali bonyeza hapa kujibu utafiti mfupi kujua wasomaji wa amka mtanzania.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s