Haya Ndio Maisha Anayoishi Bwana Mike, Ana Uhakika Wa Kushindwa Kwa Asilimia 100.

Kutana na Bwana Mike ambaye ni mwajiriwa wa kampuni moja mjini. Bwana Mike ana mtindo wake wa maisha ambao kwa maisha ya sasa yalivyo anauhakika wa kushindwa kufanikiwa kwa asilimia 100. Japokuwa yeye halijui hilo ni vigumu sana kwake kufikia mafanikio kwa mtindo huu wa maisha. Na mtindo huu unafuatwa na watu wengi, hata wewe unaweza kuwa mmoja wao. Hebu tuone mtindo wake wa maisha ukoje.

Mike huwa anaamshwa na alarm yake saa kumi na moja asubuhi, mpaka alamu inapomwamsha anakuwa bado ana usingizi mzito. Anapoamka kitandani cha kwanza anachukua smartphone yake na kuangalia kama kuna simu, meseji au email zilizoingia wakati amelala. Baada ya hapo anaingia kwenye mitandao ya kijamii(facebook) na kuchungulia kidogo ni nini kilichotokea wakati alipokuwa amelala. Anakuja kustuka ni saa kumi na moja na nusu na anaona ameshachelewa kujiandaa kwa ajili ya kwenda kazini. Alikuwa amepanga kufanya mazoezi asubuhi ila alishindwa kutokana na muda aliotumia kwenye simu. Ili kuwahi foleni na afike ofisini mapema anaanza kujiandaa kwa kasi ya ajabu sana. Akiwa njiani kuelekea kazini anakwamba kwenye foleni kwa zaidi ya saa moja, anaendelea kuperuzi simu yake kwenye mitandao mbalimbali na muuza magazeti akipita ananunua na kuanza kusoma magazeti.

kitabu kava tangazo

Mike anafanikiwa kufika ofisini saa moja na nusu asubuhi anaingia tena kwenye kompyuta na kuangalia kidogo mtandaoni kuna nini kipya. Anaonekana yuko bize sana nyuma ya kompyuta. Baada ya muda anakwenda kwenye kikao na anarudi zaidi ya saa moja baadae. Anaporudi unakuwa muda wa chai, wakati huo wa chai anabishana kidogo na wafanyakazi wenzake juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea kwenye jamii, siasa na michezo. Baadae anarudi ofisini anafanya kazi baada ya muda kidogo anachungulia tena kwenye mtandao nini kinaendelea. Anajibu watu waliochangia kwenye mada zake za facebook, anajibu email na anajibu meseji za watu. Kabla hajamaliza hayo muda wa kula unakuwa umefika na anaenda kula.

Anarudi kutoka kwenye chakula amechoka na anajiskia kusinzia sinzia, kwa kuwa kampuni yao hairuhusu watu kulala mchana anajiweka bize bize nyuma ya kompyuta na kuzunguka zunguka na mafaili mpaka saa kumi inafika. Siku imeisha, hakuna kazi kubwa aliyofanya, anapanga kuifanya kazi yake kwa uhakika zaidi kesho.

Anarudi nyumbani, masaa mawili yuko kwenye foleni, anatoa kila lawama ni kwa jinsi gani serikali ilivyokuwa na uzembe na kushindwa kuondoa foleni, anaamua kusikiliza redio kupoteza poteza muda ili afike nyumbani. Huku akiendela kuperuzi mtandao.

Anafika nyumbani saa kumi na mbili au saa moja, amechoka na moja kwa moja anakwenda kukaa mbele ya TV. Anaanza kuangalia habari kwenye vituo mbalimbali vinavyozusha habari kwa nyakati tofauti, baada ya habari anaangalia tamthilia, huku akiendelea kupitia mtandao na mitandao ya kijamii.

Anakuja kustuka ni saa tano usiku, hajalala na kesho anatakiwa kuamka mapema ili awahi kazini. Anaenda kitandani na simu yake, huku akiiangalia angalia mara kwa mara. Anapotelea kwenye usingizi kama saa sita usiku na anaamshwa na alamu saa kumi na moja asubuhi kabla usingizi wake haujaisha vizuri. Anaanza tena ratiba ya jana upya.

Je maisha yako yanafanana na ya Bwana mike japo kwa kiwango kidogo?

Bwana Mike hawezi kufanikiwa kwa mtindo huu wa maisha, hivyo na wewe kama unafanya hivi hata kwa asilimia 30 tu upo kwenye njia moja na Mike, ya kutokufanikiwa.

Ni nini anaweza kufanya Mike ili aweze kufikia mfanikio?

Kitu cha kwanza kabisa anachotakiwa kufanya Mike ni kupangilia muda wake na kuweka vipaumbele vyake. Muda ni tatizo sana kwa kila mtu. Tuna vifaa vingi vya kupima muda ila hatuna muda kabisa.

Watu wanaofanikiwa sana na kufanya mambo makubwa wana masaa 24 kama hayo uliyonayo wewe. Nini kinafanya wao wafanikiwe na wewe uwe na maisha ya kawaida sana? Vipaumbele katika matumizi ya muda ndio tofauti kubwa kati ya wanaofanikiwa sana na wanaosukuma siku ziende.

Mwezi wa tano ndani ya KISIMA CHA MAARIFA tutazungumzia jinsi ya kujijengea tabia ya kujali na kutunza muda ili kuweza kufikia mafanikio. Kama unataka kujifunza tabia hii muhimu kwa ajili ya kufikia mafanikio jiunge sasa na kisima cha maarifa. Kumbuka utaratibu wa kujiunga na kisima umebadilika ambapo sasa unaweza kujiunga siku tatu kabla ya mwezi kuisha. Ukishindwa hapo itabidi usubiri mpaka mwezi unaoanza ufikie ukingoni. Kwa kuwa leo ndio siku ya mwisho wa mwezi huu wa nne, jitahidi ujiunge leo kama unataka kupata mambo haya mazuri ya mwezi wa tano. Kujiunga ni tsh elfu kumi tu na unakuwa mwanachama wa kudumu. Tuma fedha kwa mpesa/tigo pesa (0755953887/0717396253) na utume email yako ya GMAIL kisha uunganishwe. Kama huna email ya GMAIL unaweza kutuma fedha kidogo ya ziada(tsh elfu 5) na ukatengenezewa email hiyo na kuunganishwa moja kwa moja. Unaweza kutumia email nyingine tofauti na Gmail ila itakubidi uibadili kabla ya siku 30 kuisha.

Karibu sana katika safari hii ya kubadili maisha yetu ili tuweze kufikia mafanikio makubwa.

Kumbuka tuko pamoja.

JINA LA MIKE LIMETUMIKA KAMA MFANO TU.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: