Mambo Mapya Ndani Ya AMKA MTANZANIA; Kila Siku ya Jumatatu Kutakuwa Na Makala Ya Ushauri.

Wiki tatu zilizopita nilitoa utafiti mfupi kwa ajili ya kujua wasomaji wa AMKA MTANZANIA. Katika utafiti ule moja ya maswali ilikuwa ni kutaka kujua ni changamoto gani zinamzuia msomaji kufikia malengo yake aliyojiwekea. Utafiti mzima ulikuwa na maswali kumi.

Wasomaji 85 walijibu maswali ya utafiti huu mpaka mwisho. Nimepitia majibu ya kila msomaji aliyejibu utafiti ule. Kila mmoja alieleza changamoto inayomzuia kufikia malengo yake.

Nimepokea changamoto nyingi sana ila pia nyingi zinajirudia rudia. Karibu kila aliyejibu utafiti alisema changamoto kubwa ni mtaji. Pia kulikuwa na swali linauliza kama mtu anachofanya sasa ndio ndoto yake, asilimia 90 walisema sio ndoto zao. Wengi wanapendelea kufanya biashara ila kikwazo kikubwa ni mtaji.

Baadhi ya changamoto ambazo zilitolewa na wengi ni hizi hapa

1. Mtaji

2. Kuwa na idadi kubwa ya wategemezi.

3. Kukosa muda wa kufuatilia biashara za pembeni.

4. Elimu ya darasani na elimu ya biashara.

5. Kipato kidogo na matumizi kuwa makubwa kuliko kipato

6. Kukosa mtandao na watu muhimu kwenye kile unachofanya.

7. Kutokuaminiwa na kukosa ushirikiano.

8. Uvivu na kukosa msukumo kutoka ndani.

9. Ushindani mkubwa kwenye biashara.

10. Woga wa kuanza na jinsi ya kuanza biashara.

11. Jinsi ya kuacha ajira.

12. Wenza kwenye ndoa.

13. Uhaba wa wateja.

14. Rushwa na ubaguzi.

15. Uchache wa fursa(??)

16. Kuibiwa, kudhulumiwa, na wateja wasio waaminifu.

17. Kukatishwa na kukata tamaa.

18. Matumizi ya fedha bila mpango.

19. Mazingira magumu.

20. Changamoto ya wafanyakazi.

kitabu kava tangazo

Ukiangalia nyingi ya changamoto zilizotolewa hapa nimewahi kuzizungumzia kwenye makala mbalimbali hapa AMKA MTANZANIA.

Kutokana na changamoto hizi na kutokana na lengo la AMKA MTANZANIA kuwa ni kuwasaidia watanzania kuweza kuboresha maisha yao na kufikia malengo yao, nimetenga siku za jumatatu kuwa za kuweka makala maalumu kwa ajili ya kutoa majibu ya changamoto. Hivyo kwanzia jumatatu ijayo kutakuwa na makala inayochambua moja ya changamoto hizo.

Kwa kuwa mtaji ndio changamoto kubwa kwa karibu kila mtu nimeamua kuandika kitabu kwa ajili ya kujadili changamoto hii. Itanichukua siku kadhaa kukamilisha kitabu hiki na nitakitoa bure kabisa kwa wasomaji wote wa AMKA MTANZANIA.

Kumbuka sio kwamba mimi nina majibu yote ila tunajaribu kujadiliana jinsi ya kuweza kuvuka changamoto hizi na kuboresha maisha yetu. Hivyo katika makala hizi mtu yeyote atakayekuwa na ushauri wa ziada ataombwa kuuweka kwenye maoni ili anayesoma auone pia.

Karibu tuendelee kuwa pamoja ili kuendelea kuboresha maisha yetu. Endelea kutembelea AMKA MTANZANIA kila siku na waalike wengine nao watembelee ili tuweze kuleta mageuzi makubwa kwenye nchi yetu.

TUKO PAMOJA.

N.B Kama hukupata nafasi ya kujibu utafiti huu kuna nafasi 15 za kujibu zimebaki. Bonyeza maandishi haya kujibu utafiti huo. Ukifungua ukashindwa kujibu ujue utakuwa umeshafungwa, kama utakosa nafasi hii usihofu kutakuwa na utafiti mwingine baada ya kumaliza kujadili changamoto hizi.

 

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s