Mambo Makubwa Yanaendelea Ndani Ya Kisima Cha Maarifa Usipitwe na Zoezi Hili Muhimu La Kuboresha Maisha Yako.

Kama nilivyoahidi kila mwezi tutakuwa tukijadili tabia moja ya mafanikio na kuona jinsi gani inatuzuia kufikia mafanikio na njia zipi tunaweza kutumia kuboresha tabia hiyo ili tuweze kufikia mafanikio makubwa. Kila wiki siku ya jumanne kutakuwa na makala moja inayozungumzia tabia husika hivyo kila mwezi utakuwa na makala nne.Unaweza kuona makala nne ni fupi sana ila utapata vitu vingi sana ambavyo ukiweza kuvitumia utabadili maisha yako kwa kiwango kikubwa sana.

Kitu kikubwa sana kwenye kipengele hiki kipya cha KUJENGA TABIA ZA MAFANIKIO ni kwamba tutakuwa na mazoezi ya kufanya, yaani kuna vitu utahitajika kufanya ili uweze kwenda vizuri na mabadiliko haya ya tabia.

Mwezi huu wa tano tunazungumzia muda, kitu ambacho kinaonekana hakina thamani kubwa ila kinachoweza kuzuia au kutufikisha kwenye mafanikio yetu.

Wiki hii ya kwanza ya kwanza ya kuzungumzia muda tumepiga hesabu moja na kugundua kwamba mtanzania wa kawaida anapoteza siku182 kwa mwaka!! Hii ina maana nusu ya muda wako kwa mwaka unaipoteza na hujui unapotezea wapi.

Pia tumepeana zoezi zuri la kujua ni wapi muda wetu unapotelea kwa wiki nzima na wakati wa zoezi hili tutakuwa na majadiliano ya sehemu gani muda wetu unapotelea kwenye sehemu ya majadiliano ndani ya kisima cha maarifa.

Mambo haya ni mazuri sana kiasi kwamba nimesukumwa kukuambia kama kweli unataka kubadili tabia yako mbaya ya kupoteza muda unahitaji kufanya zoezi hili. Kutokana na umuhimu wa zoezi hili natoa nafasi ya upendeleo kwa siku ya leo tu, kama kuna mtu anataka kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA afanye hivyo kabla ya siku ya leo kuisha.

Hii ni nafasi ya upendeleo ambayo natoa kwako kwa sababu sitaki ukose sehemu hii muhimu sana ya kubadili na kuboresha maisha yako. Kumbuka utaratibu wa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA umebadilika na unaweza kujiunga siku tatu za mwisho wa mwezi, kwa leo natoa nafasi ya upendeleo, chukua hatua mapema kabla muda haujaisha. Ukikosa nafasi hii ya leo utasubiri mpaka tarehe 28/05/2014.

Kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA tuma fedha tsh elfu kumi kwa mpesa au tigo pesa(0755953887/0717396253) kisha tuma meseji kwenye moja ya namba hizo ilkiwa na email yako ya GMAIL kisha utaunganishwa na Kisima. Kama huna Gmail kwa sasa unaweza kutumia email yoyote uliyonayo na baadae ukaibadiki kabla ya siku 30, au ukasema na ukatengenezewa email ya GMAIL.

Nakushauri sana usikose hatua hii muhimu ya kubadili na kuboresha maisha yako ambayo tunafanya ndani ya wiki hii.

kitabu kava tangazo

Kolamu mpya ya ushauri ndani ya AMKA MTANZANIA.

Kama nilivyoahidi wiki iliyopita kwamba kila jumatatu kutakuwa na mada maalumu ya ushauri kwa changamoto ambazo zinawazuia watu wengi kufikia ndoto zao, wiki hii kuna makala inayozungumzia changamoto ya idadi kubwa ya wategemezi.

Watu wengi wanalalamika kwamba wana idadi kubwa ya watu wanaowategemea na kipato chao ni kidogo, hivyo inawawia vigumu sana kufikia malengo yao. Kwenye makala hii tumejadili mambo matano muhimu unayoweza kuyafanya na ukakabiliana na changamoto hii na kuweza kufikia malengo yako. Kama bado hujasoma makala hiyo bonyeza hapa;

Ushauri; Ni Jinsi Gani Unaweza Kufikia Malengo Yako Kama Una Idadi Kubwa Ya Wategemezi?

Nakutakia kila la kheri kwenye harakati zako za kuboresha maisha yako.

Kumbuka, TUKO PAMOJA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s