Punguza Changamoto Za Kufanikiwa Kwa Kutafuta Taarifa Sahihi.

MAKALA HII IMEANDIKWA NA JOHN MATIKU(johnmatiku1@gmail.com)

Kwenye mada hii nataka nijaribu kukumbusha au kugusia taarifa kadhaa muhmu ambazo kama  kweli wewe nimtafutaji wa mafanikio makubwa nilazima kwa vyovyote vile uzipate na uzielewe vyema.
HIvyo hapa nitakuandikia chache ambazo huenda huduma au biashara yako ikahitaji zaidi ila kwa mwanga utakaoupata hapa nina imani haitakua ngumu tena kutafuta taarifa hizo.

Dunia tunayoishi sasa  inakumbwa na uhalifu wa kiwango cha juu sana (hasa wizi) na ukiangalia kwa makini uhalifu huu unapata nafasi sana kutokana na tamaduni zetu za KUAMINIANA BILA TAHADHARI. Wezi na matapeli wanatumia mwanya huo kuwaibia watu wengi na kwa bahati mbaya watu wanaotafuta mafanikio na hasa ya kuwa na fedha kama wewe ndio walengwa wa uhalifu huo!

Uhalifu huu unaweza kukutana nao hasa katika mambo yafuatayo;

1. Kwenye kununua mali au huduma mbali mbali, mfano viwanja, mashamba, vyombo vya usafirishaji kulipa pango la chumba au nyumba ya biashara.

2. Mikataba mbali mbali, kama mikopo kutoka kwa watu binafsi, taasisi za fedha, huduma za bima.

3. Kwenye kununua na kuuza bidhaa ikiwa biashara yako ni ya muundo huo n.k

Sasa, ulimwengu wetu tunaoishi ni ulimwengu wa SHERIA na hivyo hakuna jinsi ya kuwa salama bila kuwa makini na kuegemea SHERIA. Yaani kila jambo unalotaka kufanya hasa kama linahusisha biashara au mabadilishano ya mali kwa mali au mali kwa fedha kwa lengo la kibiashara ni muhmu kwanza kujua wajibu na haki zako kwa mujibu wa SHERIA za nchi juu ya jambo hilo kabla ya kujiingiza kwenye kushiriki wa jambo hilo. Kwani kwa kutofanya hivyo unaweza kujikuta kwenye migogoro ya kisheria na hivyo ukajikuta unapoteza FEDHA, MALI na hata MUDA wako ambao ungeweza kuutumia kwenye mambo mengine ya msingi zaidi.

kufungwa

Ukiachana na hilo hapo juu, sehemu nyingine unayoweza kupata mgongano na mvutano mkubwa ikiwa hutatafuta taarifa hasa kuhusu matakwa ya sheria za nchi ni kutotambua wadau mbali mbali wa biashara yako au huduma unayoanzisha, unayofanya, au unayotarajia kufanya! Mfano unapotaka kuanzisha biashara au huduma yoyote kuna vyombo ambavyo vina mamlaka juu ya biashara au huduma hiyo.  Baadhi ya vyombo hivyo ni;

1. MAMLAKA YA BIASHARA NA LESENI.

2. MAMLAKA ZA KODI NA MAPATO

3. TAASISI ZA ULINZI NA USALAMA

4. VITENGO VYA DHARURA NA UOKOZI KAMA ZIMAMOTO.

5. MAMLAKA ZA CHAKULA NA DAWA (TFDA)

6. MAMLAKA ZA UDHIBITI WA UBORA WA BIDHAA (TBS)
na nyingine zenye mamlaka zilizopo kwa mujibu wa sheria za nchi.
Ziko faida kubwa za kutafuta taarifa muhimu kuhusu wadau mbalimbali

Mfano TRA
1. Utajifunza namna nzuri ya ukokotozi wa kodi unayotakiwa kulipa badala ya kukadiriwa,
2. Utapata taarifa kuhusu SHERIA YA KODI YA MAPATO
3. UTAFAHAMU MAANA YA BIASHARA KWA TAFASILI LASMI YA KISHERIA.

Ni vyema ukazitambua na ukatambua wajibu na uhusiano wako kisheria na kuzingatia uhusiano huo hivyo ukawa umejiepusha na mgongano wa kisheria na wadau hao muhImu wa biashara au huduma yako, kwani kwa kutofanya hivyo unaweza kujikuta kwenye matatizo kama kufungiwa, kusimamishwa kuendelea na biashara au huduma, kutozwa faini   na kadhalika.
Bila shaka baadhi yetu tutakua tumeshaona au kusikia migogoro hii
Mfano ni kufungwa kwa baadhi ya shule, zahanati, viwanda vya kutengengeneza mikate, viwanda vikubwa na kadhalika (Vyote hivi vikiwa ni vya watu binafsi) hii yote ikiwa ni kutozingatia uhusiano na ushirikiano  na baadhi ya mamlaka tajwa hapo juu, au nyingine kama hizo, hii yote kwa hakika inaweza fifisha ukamilifu ndoto yako.

Kwa vyovyote vile jiepushe na migogoro  na mamlaka za umma kadri iwezekanavyo.

ZINGATIA: kupata pesa ni kitu kimoja na kulea pesa ziendelee kuishi na wewe ni kazi nyingine  kubwa zaidi.
Asante.

kitabu kava tangazo

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: