Mimi huwa nasoma angalau kitabu kimoja kila wiki na wakati mwingine nasoma vitabu viwili au zaidi ndani ya wiki moja. Sitaki kurudia ni faida gani naipata kwenye kusoma vitabu hivi kwa sababu nilishaeleza sana kwenye makala; hivi ndivyo tabia ya kupenda kujisomea ilivyoninufaisha, inawezekana hata kwako pia.
Watu wengi huwa wananiuliza napata wapi muda wa kusoma vitabu vyote hivi? Ukweli ni kwamba nina mambo mengi sana ya kufanya ila nahakikisha katika masaa 24 ya siku sikosi dakika 30 za kujisomea. Nafikiri hata wewe pia unaweza kupata dakika hizi 30 kwenye siku yako kwa sababu unapoteza muda mwingi zaidi ha huu kila siku. Au huenda unapata hizo dakika 30 ila huwezi kusoma hata kurasa tano.
Unawezaje kuzitumia dakika 30 kujisomea?
Kuna mambo mengi sana yakuzingatia kama unataka kusoma vitu vingi ndani ya muda mfupi. Baadhi ya vitu hivyo ni;
1. Muda uliotenga kwa ajili ya kujisomea. Sawa umepanga kujisomea dakika 30 lakini ni muda gani? Kama umepanga kujisomea jioni baada ya kutoka kwenye kazi zako ukiwa umechoka ni vigumu sana kufanikiwa kusoma na kuelewa. Ila ukitenga muda wa asubuhi ndio ukawa unajisomea utaona unaelewa vizuri na kukumbuka zaidi.
2. Mazingira unayosomea. Kama unasomea kwenye mazingira ambayo yana usumbufu mwingi ni vigumu sana kuweza kusoma vizuri na kuelewa. Unapotenga nusu saa hii hakikisha unakuwa kwenye eneo tulivu, tena mbali kabisa na simu. Kama unataka kusoma huku unaangalia TV au kusikiliza redio au unasoma huku unapiga hadithi au unachat itakuwa vigumu sana kwako kupata ule ujumbe uliokusudia kuupata.
3. Aina ya usomaji. Kama bado unasoma kwa mtindo uliofundishwa shule ya msingi utajikuta una mwendo mdogo sana kwenye kusoma. Hii ni kwa sababu akili yako imejifunza kusoma neno moja moja na kulielewa ndio kwenda kwenye neno jingine. Ili uweze kusoma kwa kasi yako ya kusoma inakubidi ubadili mfumo wa kujisomea.
Mfumo wa kusoma kwa kasi na kuelewa zaidi.
Kuna mifumo mingi sana ya kuweza kusoma kwa kasi, kuelewa zaidi na kukumbuka yale uliyoyasoma. Mifumo hii haitofautiani sana kwani yote inakufundisha kubadili muundo wako wa kusoma na kujenga muundo mwingine.
Kwa mfano kwa dakika 30 unazopanga za kusoma unaweza kuwa unasoma ukurasa mmoja kwa dakika moja, hivyo kwa siku unasoma kurasa 30 na kwa wiki unasoma kurasa 210, umeshamaliza kitabu kwa sababu vitabu vingi vina kurasa 200.Hii ndio kasi niliyojifunza mimi kusomea, Wakati mwingine naweza kusoma kwa kasi ya kurasa mbili kwa dakika moja.
Hata wewe unaweza kuongeza kasi yako mpaka kufikia hapo au hata zaidi ya hapo. Watu wengi waliojifunza kuongeza kasi ya kusoma wanaweza kusoma mpaka kurasa 4 au 5 ndani ya dakika moja.
Ni njia zipi unatumia kuongeza kasi yako ya kusoma.
Kuna njia nyingi sana zinazoweza kukusaidia kuongeza kasi ya kusoma. Hapa nitazungumzia chache na nitatoa kitabu ambacho kimeeelezea zaidi.
1. Acha kusoma kwa sauti.
Japo kuwa hutoi sauti unaposoma lakini umejijengea tabia ya kutamka neno kwanza wakati unajisomea, tabia hii inakupunguzia kasi yako ya kujisomea kwa asilimia 50. Huna haja ya kutamka kila neno kwenye akili yako bali unatakiwa kulielewa na kwenda haraka kwenye neno lingine au maneno mengine.
2. Soma sentesi nzima na sio neno kwa neno.
Wakati mwingi huwa tunasoma neno moja halafu unaenda neno jingine hivyo hivyo. Kama unataka kuongeza kasi yako ya kusoma acha mfumo huu wa kusoma neno moja moja, bali soma sentensi nzima au soma kikundi cha maneno kwa mara moja. Hii itakusaidia kwenda haraka unaposoma.
3. Chukua muhtasari au weka alama.
Kama unasoma kitabu kilichochapwa unaweza kuwa unatumia rangi kuweka alama kwenye sehemu ambazo ni muhimu sana kwa kile unachosoma. Pia unaweza kuwa unachukua muhtasari wa baadhi ya vitu muhimu ulivyoelewa kadiri unavyosoma.
4. Tumia kifaa chochote kufuata mstari au sntesi unayosoma.
Kama unasoma vitabu vilviyochapwa unaweza kutumia kidole au hata kalamu kufuata sentensi unayosoma. Hii itakusaidia kuweka msisitizo wako pale unaposoma na kuacha kuangalia maneno mengine ya mbele zaidi auyaliyopita nyuma. Hata kama unasoma kwenye kompyuta au simu fuata na kidole na utaona kasi yako yakusoma inaongezeka.
5. Tafakari kila unapomaliza kusoma.
Usichukulie muda uliojiwekea kusoma kama kifungo kwamba unapoisha unakimbia haraka na kuanza kufanya mambo mengine uliyoacha kusoma. Jipe dakika chache za kutafaari yale uliyoyasoma na kufikiri kidogo zaidi. Hii itakusaidia kuelewa zaidi na pia kukumbuka zaidi. Wengi wetu ukishamaliza kusoma unakimbilia simu au tv au kupiga hadithi, hii inakufanya usahau haraka sana yale uliyojifunza. Hii inaumika pia hata kama unasoma na umetoka kufundishwa, au unafanya kazi na umetoka kwenye mkutano muhimu, tumia dakika chache kutafakari yale uliyofundishwa au uliyosikia.
Zipo njia nyingi sana za wewe kuweza kujifunza kuongeza kasi yako ya kujisomea. Ukianza na hizo chache utajikuta unaongeza kasi yako ya kusoma mara mbili ya unavyosoma sasa hivi. Utaweza kusoma vitabu vingi sana na utapata faida kubwa.
Kitu kimoja cha ziada nachoweza kukusisitiza ni KUWA NA KITABU POPOTE UENDAPO. Usidhubutu kabisa kwenda popote kama huna kitabu ambacho unaweza kujisomea wakati ambao utakuwa unapoteza muda.
ZOEZI LA WIKI.
Wiki hii tutafanya zoezi la kujifunza kuongeza kasi ya kusoma. Ili kupata mwanga zaidi nakupa kitabu kinachoitwa The Speed Reading Course, kitabu hiki kimeelezea mbinu za kuweza kuongeza kasi yako ya kusoma. Kukipata bonyeza maandishi hayo ya kitabu.
Kitabu hiki kina kurasa 40 tu hivyo kama ukiweza kusoma kwa kurasa moja kwa dakika moja itakuchukua dakika 40 tu. Nakushauri ukisome na kukirudia kama mara tatu ili uweze kuelewa kila kilichoandikwa.
Baada ya kusoma na kuelewa kitabu hiki, rudia mbinu ulizojifunza kusoma baadhi ya vitabu ambavyo nilishakutumia lakini bado hujaweza kuvisoma. Nina uhakika kuna vitabu vingi nimekutumia ila bado hujavigusa, huu ndio wakati muafaka wa kuvisoma.
Baada ya kusoma kitabu hiko tunaweza kushirikishana yale tuliyoelewa kwenye FORUM-MAJADILIANO ili tuweze kujadiliana zaidi.
Nakutakia kila la kheri katika yote unayofanya ili kuboresha maisha yako,
TUKO PAMOJA,
Asante Coach,
Je hisa zinazouzwa na voda ni salama ?
LikeLike
Kila uwekezaji una faida, hasara na hatari zake.
Hisa za vodacom kwa vile ndiyo mara ya kwanza zinaingia kwenye soko la hisa, zina ugumu wa kusema ni salama kabisa, au siyo salama kabisa. Hivyo hapo ni mwekezaji kupima uwezo wake wa kuchukua hatari.
Lakini ninachoshauri mimi, ni kila mwenye uwezo wa kuwekeza kwa sasa, asiache kuzinunua hisa za Vodacom, kwa sababu hata kama hazitakuwa na thamani inayotarajiwa, bado mtu hatapoteza kabisa, hasa kwa siku zijazo.
Namaanisha unaweza kununua na kukaa nazo kwa muda, ambapo lazima thamani itaongezeka, kulingana na aina ya biashara na ukuaji wake.
LikeLike
ni kweli kuna siku niliacha kununua mkate uchumi supermarket eti wauzaji wanasema niwaachie 200 hawana change au wanipe pipi…. ndo maana wamefilisika kwa vitu vidogo vidogo
LikeLike
Hakika,
Tabia ndogo ndogo kama hizo watu wanazichukulia kawaida lakini athari zake ni kubwa. Hasa zinapozoeleka na kuwa utaratibu wa kawaida, zinaendelea kutafuna na hatimaye zinaua kabisa kile ambacho watu wanataka kutengeneza.
LikeLike
Asante sana kocha kwa makala hii. NIDHAMU YA FEDHA ni jambo muhimu sana. Ni ujinga kuona fahari kwa kuwa na mikopo mingi.
LikeLike
Hakika,
Tatizo linakuja pale mtu akishaweka kwenye akili yake mikopo ndiyo kila kitu.
Anapopata shida kidogo haumizi akili yake juu ya njia mbadala za kutatua, badala yake anakimbilia kukopa. Hivyo anazidi kujichimbia kwenye shimo la madeni.
LikeLike
Nilianzisha ufugaji wa kuku wa mayai na nyama nikitumaini mwenza wangu (wife) atasimamia kwani Mimi ni mwajiriwa. Faida ipo na uwezekano wa kupanuka upo lakini mradi umedorora kabisa. Wateja wanalalamikia hali hii kwani walipenda ubora wa mayai na nyama pia. Ninapenda sana kilimo + ufugaji biashara kwani kwa mazingira nilipo biashara hii inalipa na eneo la kujiongeza lipo. Unanishauri nini coach?
LikeLike
Kwa kuwa umeshajua udhaifu uko wapi, basi fanyia kazi kuboresha zaidi.
Kaa chini na mwenza wako muweke mikakati pamoja ili kutoa mazao bora zaidi.
Na hata kama muda wako unakubana, hakikisha unapata muda wa kusimamia kwa karibu miradi hiyo.
Kama ni majukumu yanamzidia unaweza kumtafutia msaidizi ambaye watafanya mambo kwa pamoja.
Kingine muhimu weka mfumo wa wao kuandika kila wanachofanya kila siku kwenye mradi huo, iwe chakula, dawa, mayai na kadhalika. Kwa namna hii itakuwa rahisi kwako kufuatilia na pia wao wataweka umakini zaidi.
Kadiri utakavyokuwa karibu na mradi huo, ndivyo na wao watakavyokuwa makini nao.
Hivyo jitahidi sana uwe karibu, hata kama kazi zinakubana, hakikisha unajua kila kinachoendelea na kuweza kuingilia mapema pale mambo yanapokuwa hayaendi vizuri.
LikeLike
Asante coach umekumbusha jambo zuri sana maana wengi tunaowaiga na kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa hua tunaangalia kwa juu juu sana na kuondoka na jibu moja pekee la kwenda kufanyia kazi ili tuwe kama wao au tupitilize zaidi ya wao tunasahau ya kwamba kuna mengi ya kujifunza na kunachangamoto nyingi sana katika kufika kule tunakotaka….kikubwa hapo ni kuangalia na kujifunza zaidi na zaidi na kuhoji kila kitu kwa undani wake na kupata mawazo mazuri na hoja nzito za kufanyia kazi…wengi tumezoea kusema wengi wape..na hii inatupelekea hata kwenye kujifunza eti mbinu aliyotumia yule na mimi nitumie ile ile na nitafanikiwa.kumbe mambo ni ya kuchimba kiundani zaidi
LikeLike
Ni kweli kabisa Ilomo,
Na hili limepelekea wengi kukimbilia kufanya mambo na kushindwa, kwa kuwa hawakuchimba ndani na kujua kipi hasa wanapaswa kufanya.
Ni vyema kuchimba ndani zaidi, siyo kujikatisha tamaa, ila kuhakikisha tuna uelewa wa kutosha pale tunapofanya maamuzi.
LikeLike
Ujumbe mzuri sana kocha! Nitaacha kuridhisha kila mtu…….. Nitaacha kujionea huruma kabisa………. Nitasema hapana kwa mambo yote yasiyo na umuhimu kuelekea kwenye ukuu wa maisha yangu………. Na kamwe sitakubali kuchinja ng’ombe wangu kwa oda ya maini!
Ubarikiwe sana
LikeLike
Hongera sana kwa hatua hizo ulizopanga kuchukua.
Kila la kheri.
LikeLike
Shukrani kwa makala nzuri ya kufanya mtu kutambua ukuu wake
LikeLike
Karibu sana.
LikeLike
Nimejifunza katika shughuli za kila siku, michakato mingine muda au subira ni hatua ya lazima Ili kupata matokeo yanayotarajiwa.kwa mfano, ktk kutengeneza sabuni ya mche kuna mchanganyiko ambao lazima uusubirishe kwa siku kadhaa kabla ya hatua nyingine ya kuelekea kupata sabuni. Na usipotii hatua hii ya kusubiri hupati sabuni hata kama vionjo vingine umechanganya kwa kiasi na masharti yanayohitajika.
LikeLike
Ni kweli kabisa,
Bila ya subira, ni vigumu kupata kile ambacho mtu unataka.
Kwa sababu hakuna kinachokuja kirahisi.
LikeLike
asante sana kwa tafsiri yako ktk makala hii.
ubarikiwe sana
LikeLike
Karibu
LikeLike