Hiki Ndio Kikwazo Kikubwa Cha Watanzania Wengi Kushindwa Kufanikiwa.

Wiki iliyopita na wiki hii niliweka makala ya kuwashauri vijana wa kitanzania ambao bado wanatafuta ajira ila bado hawajapata kuangalia mpango mwingine wa kujitengenezea kipato. Nilisema wazi umefika wakati mtu aache kulaumu serikali au taasisi nyingine yoyote na achukue hatua juu ya maisha yake mwenyewe. Kama hukusoma makala hiyo isome hapa; Barua ya wazi kwa wahitimu ambao bado wanatafuta ajira.

Katika makala hiyo nilielezea mustakabali wa ajira Tanzania na duniani kwa ujumla na nikatoa mapendekezo matano ya njia mbadala za kujiajiri na kujitengenezea kipato. Njia nilizopendekeza ni njia ambazo zinafanyika na vijana wa kitanzania na zimewaletea mafanikio makubwa, mimi mwenyewe nikiwa mmoja wao.

Baada ya kushirikisha watu makala hii kwenye mitandao ya kijamii kulikuwa na mrejesho tofauti wa kile nilichoandika. Leo nataka nikuoneshe wazi wazi ni nini kinazuia watanzania wengi kuweza kufanikiwa.

Hapa chini naweka baadhi ya maoni ya watu kuhusiana na makala niliyoandika kuhusu kujiajiri.

“Makirita Amani nimesoma kila kitu ulichoandika ila nakwambia ukweli usitake kuwadanganya watu kwa kufanya mambo ambayo hayana faida mbeleni mfano
Kilimo na ufugaji!!! Hv katika nchi yetu wananchi wenye kipato cha chini wako katika sector ipi?? Jibu la haraka ni kilimo na ufugaji nadhan ukipiga tathimin utapata ukweli.
Suala la ujasiriamali wa mtandao ndo hakuna kitu kabisa unakuta kampuni inauza bidhaa kwa bei kubwa huku bidhaa hy hy inapatikana kwa bei nafuu zaidi mtaani.
Nadhan mambo meng uloandika hayana uhalisia nadhan ningepata mda ningeandika zaidi.”

“Swala la kujiajiri ni gumu coz mtaji! Ukienda brela taratibu zote za kuanzisha biashara c chini ya mil 30!!! Hata ingekuwa mil kumi. Kwa graduate totally impossible. Jamii kama za kihindi, waarabu, wasomali wataendelea kutawala biashara tzania. Cjui ije mkakati gani! Atoke genious! Kutoka na kuendelea kwa graduate bongo kwa kujiajiri ni unthinkable. Labda wazazi wapo uko ngazi za juu, wakupe msukumo. Maadhara ya rushwa! Uwiii! Bongo 50% r corrupt! 50% r benefiting from.”

“mtoa post uko timamu? hivi mhitimu wa chuo anapata ujuzi gan wa kujiajiri? mfumo wa elim unaobase kwenye karatasi unasaidiaje kujiajiri? kilimo cha kutegemea mvua kitakupekka wap”

“Napata ukakasi kidogo na hoja zako, kwanza nataka ufahamu kuwa watanzania tatizo la ajira wanalijua, na ndio maana unaona kila siku vita vya wamachinga na wagambo haviishi. Matatizo ya mama ntilie, wafugaji, wakulima na wengine wengi, hao wote wamejiajiri. Watanzania wanataabika na mipango mibovu ya serikali ya nchi yao, mipango ya zima moto, porojo za kisiasa katika nchi makini ni lazima iwe na uwiano wa ongezeko la kiuchumi na ongezeko la kipato kwa raia wake. Na lazima kuwe na mipango ya ongezeko la watu na upatikanaji wa fursa za ajira. Hii haina maana kuwa lazima serikali itoe ajira, bali ina wajibu wa kutengeneza mazingira ya raia wake waweze kujiajiri. Sasa leo wamachinga wanafukuzwa halafu eneo linapewa gobachori, mama ntile wanapigwa mateke bila kuelekezwa wait waende, kama ndugu yangu umefanikiwa kimaisha acha kubeza watu, nimeamini kweli wajaliwao huzisifia akili zao. Watanzania sio mbumbu kiasi hicho unachofikiri wanahangaika wanakwamishwa na serikali yao.”

Hayo ni baadhi ya maoni hasi niliyopenda kukushirikisha, yapo mengi zaidi ya hayo.

Leo sisemi lolote ila nataka wewe mwenyewe upate picha ni jinsi gani mambo haya yanavyoweza kuwa magumu kutokana na mitazamo ya watu wenyewe.

Mambo waliyoandika hao wenzetu ni ya kweli kabisa, na kama wewe una mtizamo hasi unaweza ukakubaliana nao kimoyo moyo kwa kusema lakini ni kweli. Lakini kwa msomaji mzuri wa AMKA MTANZANIA atakuwa ameshaweza kujibu yote yaliyoibuliwa hapo. Maana tumeshajadili sana kuhusu kubadili mtazamo, kwamba lazima utakutana na vikwazo, jinsi gani ya kuvuka changamoto na ufanye nini pale unaposhindwa au kupata hasara.

Mawazo haya ni hatari sana kwa maendeleo ya mtu binafsi na taifa kwa ujumla. Kama wewe umeweza kupata elimu iliyokusaidia kubadili mtazamo wako na kuacha kuangalia kushindwa tu tafadhali washirikishe na wenzako ili tuweze kulikomboa taifa letu.

Tafadhali endelea kuwaalika marafiki zako kulike page yetu ya facebook. Bonyeza maandishi haya na kisha like halafu nenda sehemu ya invite friends kisha waalike nao walike ukurasa huu ili tuweze kuwafikia wengi zaidi. Naomba sana ushirikiano wako kwenye hili na utakuwa balozi mzuri wa kuwaamsha watanzania wenzetu. Asante sana kwa ushirikiano wako.

Nakutakia kila la kheri, kumbuka vikwazo ni sehemu ya safari yoyote, kushindwa ni sehemu ya kujifunza na mafanikio ndio maisha yako.

TUKO PAMOJA.

kitabu kava tangazo

2 thoughts on “Hiki Ndio Kikwazo Kikubwa Cha Watanzania Wengi Kushindwa Kufanikiwa.

 1. ALFRED GEOFREY June 19, 2014 / 6:08 am

  Pole sana kaka kwa comments hasi ulizozipata, lkn naami mtu atafanikiwa tu pale atakapobadili mtizamo wake, kwa sababu mafanikio yote yanaanza kwa mawazo. Songa mbele, those should be you steping stones

  Like

 2. Makirita Amani June 20, 2014 / 3:02 am

  Asante sana mkuu.
  Kwa kweli siwezi kukata tamaa kwa maoni hasi kama haya, nilishazoea kuyapata na zamani yalikuwa mengi sana. Nashukuru sasa hivi kidogo watu wameanza kuona uhalisia na wanachukua hatua.
  Nimewashirikisha hili ili mpate picha kwa nini wenzetu itawachukua muda sana mpaka kuweza kufikia mafanikio kwenye maisha yao.
  TUKO PAMOJA.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s