Sababu Kumi Kwa Nini Ni Muhimu Sana Wewe Kuwa na Blog.

  Blog ni sehemu ndogo ya mtandao wa internet ambapo unaweza kuweka maoni au maandiko yako na yakaonekana dunia nzima. Tofauti na website(tovuti), blog ni rahisi kuanzisha, rahisi kuendesha na haihitaji gharama kubwa, unaweza kuendesha bure kabisa.

  Kuna faida nyingi sana za wewe kuwa na blog, katika makala, tengeneza blog yako leo na upate faida hizi tano niliongelea faida za kiuchumi za kuwa na blog. Leo nitaongelea faida za maendeleo yako binafsi kwa kuwa na blog yako. Hapa nazungumzia blog za kuandika mambo yenye msaada kwa watu wengine na sio za kuripoti habari za udaku.

blog2

  Hizi hapa ni sababu kumi kwa nini ni muhimu wewe kuanzisha blog yako leo hii na sasa hivi;

1. Kuendesha blog ni changamoto na changamoto zinakufanya ukue.

Wote tunajua kwamba bila ya changamoto huwezi kukua kiakili na kimawazo. Unapokuwa na blog na kujiwekea ratiba ya kuandika kwenye blog yako kuna wakati inakuwa vigumu kabisa kwako kuweza kuandika kitu chenye maana. Lakini kama utaweza kukaa chini na kuandika hata kama hujisikii kuandika inakujengea nidhamu kubwa na utaweza kufanya mambo mengine makubwa kwenye maisha yako.

2. Kujifunza mambo mapya.

Kuwa na blog ni sehemu nzuri sana ya kujifunza mambo mazuri tena kwa bure kabisa. Kwanza kabisa utajifunza kuandika kitu ambacho kitakusaidia sana kwenye shughuli zako. Pili utajifunza zaidi kuhusu mada unazopendelea kuandika. Kwa njia hii utajua mengi zaidi na yatakusaidia kwenye kazi na biashara zako.

3. Kuleta tofauti kwenye maisha ya watu.

Chochote utakachoandika kwenye blog yako ambacho kinakusaidia wewe, jua kuna mtu mwingine pia akikisoma kitamsaidia sana. Kwa kuandika mambo ambayo yanawasaidia watu na wakakutafuta kukushukuru kwa maandiko yako inakupa moyo na kukufanya uandike zaidi. Hii imekuwa ikitokea kwangu karibu kila siku.

4. Unakuwa mtaalamu.

Unapokuwa na blog na ukachagua mada fulani ukawa unaziandikia mara kwa mara itakufanya wewe kuwa mtaalamu wa mada hizo, na baadae watu watakufuata kwa ushauri. Kwa mfano kama una blog na unaandika kuhusu kilimo na ufugaji watu watakapokuona ukiandika kwa muda mrefu inakuwa rahisi kwao kukufata na kutaka ushauri zaidi kuhusiana na mambo hayo. Kwa njia hii unaweza kutengeneza biashara nzuri baadae.

5. Unayaweka mawazo yako kwenye mtandao mkubwa.

Kwa kuwa na blog iliyounganishwa na mitandao ya kijamii ni rahisi kwa watu kusambaza ujumbe wako kwenye mitandao yao. Kama unaandika vitu vyenye msaada kwenye maisha ya watu ni rahisi kwao kuwashirikisha wengine. Hii itakuza sana blog yako na itatengeneza fursa ya biashara baadae.

6. Kujenga uzoefu mpya.

Kama umeajiriwa na kazi yako haina hamasa kubwa ni rahisi sana kuwa na msongo wa mawazo. Ila kama ukiwa na blog yako unakuwa na uzoefu mpya ambapo utakuwa na utaratibu wa kujifunza zaidi, kuandika na kushirikisha dunia mawazo yako. Pia itakuwa rahisi kwako kujadiliana na wasomaji wako kuhusu mada mbalimbali. Hivyo badala ya kutumia internet yako au ya ofisi kwa kuangalia mambo yasiyo na maana kwenye mtandao, hebu anzisha blog yako leo na uanze kufurahia maisha yako.

7. Kukutana na watu wapya.

Kwa kuwa na blog inayoandika mambo mazuri inakuwa rahisi sana kwako kukutana na watu wapya na wa muhimu sana kwenye mada unazoandika na hata biashara. Kupitia blog nimeweza kukutana na watu wengi sana ambao mpaka sasa tunashirikiana kibiashara na katika mambo mengine muhimu ya maendeleo.

8. Kuandika kuhusu maisha yako.

Kuwa na blog sio lazima uandike mada kwa ajili ya watu wengine. Unaweza kuwa na blog utakayoandika safari ya maisha yako. Uzuri ni kwamba unaweza kuifanya blog kuwa private hivyo ukaiona wewe tu au watu utakaowaruhusu waione.

9. Kukabiliana na hofu zako.

Blog ni njia moja nzuri sana ya kukabiliana na hofu zako. Kama una hofu ya kupingwa hivyo unashindwa kutoa maoni yako kwenye vikao muhimu anzisha blog yako leo. Mada yoyote utakayoandika kwenye blog yako lazima kuna mtu atakupinga, kwa njia hii utajifunza kukabiliana na upinzani wa aina hii na moja kwa moja unaondoa hofu ya kupingwa. Moja ya makala nilizokuwa naandika mwanzoni kabisa wakati naanzisha AMKA MTANZANIA ni umuhimu wa watu kujisomea vitabu ili kujiendeleza binafsi. Nilipata upinzani mkubwa sana kutoka kwa baadhi ya watu kama vile niliwashikia fimbo na kuwalazimisha. Iliniumiza sana mwanzoni lakini baadae nilijifunza ni sehemu ya uandishi.

10. Kutengeneza fursa za kibiashara.

Kuwa na blog ni njia rahisi ya kutengeneza fursa mpya za biashara. Unaweza kutafutwa kutokana na utaalamu wako kwenye mada unayoandika na kuwa mshauri mzuri. Unaweza kuuza bidhaa zako zinazotokana na mada unayoandika kupitia blog yako. Kuna fursa nyingi za kibiashara utazipata kwa kuwa na blog.

  Kama mpaka sasa huna blog anzisha blog yako leo. Sahau chochote kuhusu biashara au kutengeneza fedha kupitia blog hiyo. Anza kwa kutengeneza utaalamu wako kupitia mada unayochagua kuandika, baadae fedha zitakufuata zenyewe.

COVER

  Huna utaalamu wa kuanzisha blog? Usihofu, kila kitu kiko hapa.

  Kama umeweza kusoma hapa basi nakuhakikishia unao uwezo wa kuanzisha blog yako chini ya nusu saa. Unachohitaji ni kuwa na kompyuta na internet, baada ya hapo utafuata maelekezo rahisi na yenye picha kwenye kitabu JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG na kukamilisha blog yako ndani ya muda mfupi. Kwa shilingi elfu kumi tu za kitanzania utaweza kupata maarifa muhimu ambayo yatakusaidia sana kuboresha maisha yako. Utajifunza jinsi ya kutengeneza na kukuza blog, kuwa mwandishi mzuri, kuanzisha na kukuza biashara na mengine mengi muhimu.

Kitabu hiki kinapatikana katika mfumo wa PDF na kinatumwa kwa email. Kupata kitabu hiki tuma fedha tsh elfu kumi(10,000/=) kwa mpesa 0755953887 au tigo pesa 0717396253 na utume email yako kisha utatumiwa kitabu.

Karibu sana, TUKO PAMOJA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: