Mpango Wa Ushauri Kwa Wahitimu Kuhusu Uhalisia Wa Mtaani.

Huu ni wakati ambao miaka ya kitaaluma ya vyuo na taasisi nyingine za elimu ya ujuzi nchini inafikia mwisho. Ndani ya mwezi mmoja ujao wahitimu zaidi ya elfu arobaini(40,000) wataingia mtaani baada ya kumaliza masomo yao. Wapo wanaomaliza ngazi ya cheti, wengine stashahada, shahada na hata wengine shahada ya uzamili. Wahitimu hawa wanaingia mtaani wakiwa na matumaini makubwa kwamba baada ya kupambana na kujituma darasani sasa muda wa kula matunda ya kazi yao umewadia.

Lakini mtaani uhalisia uko tofauti sana na mawazo ya wahitimu hawa. Wengi wao walikuwa wakipeana hadithi nzuri za ulimwengu wa kazi kwa kuwaangalia watu wachache ambao wanawafahamu na wanafanya kazi zinazoonekana kuwa nzuri. Hawakuwahi kupata muda wa kuangalia upande wa pili wa shilingi ambapo kuna wenzao wengi wana mwaka, niamaka miwili na hata zaidi mtaani wakihangaika kusaka ajira bila ya mafanikio yoyote.

Hali ni mbaya sana ila sehemu kubwa ya wahitimu hawa hawajalijua hili, labda watashtuka wakishakaa mwaka mzima mtaani bila ya ajira.

Ili kuondoa adha hii kwa wahitimu hawa, AMKA MTANZANIA kwa miezi miwili, mwezi wa saba na mwezi wa nane, kila siku ya jumatano itawekwa makala moja yenye ushauri wa kina na unaoweza kufanyika kwa wenzetu ambao wamehitimu masomo yao. Kwa miezi hiyo miwili kutakuwa na jumla ya makala nane, kama mtu akizisoma makala hizo na kuchukua hatua ataweza kuboresha maisha yake mapema kabla hajapoteza muda mwingi kuzunguka na bahasha.

kitabu kava tangazo

Makala hizi zitakusaidia nini wewe mhitimu?

Kuna wengi wanasema kama mtu amesoma miaka yote hiyo makala hizi zitamsaidia nini? Makala hizi zitakuwa na msaada mkubwa sana kwa yeyote atakayechukua hatua.

1. Zitakusaidia kubadili mtazamo wako juu ya maisha, ajira na mafanikio. Kwa muda mrefu umekuwa ukiaminishwa soma kwa bidii na utapata ajira nzuri na kufanikiwa, lakini ajira zenyewe hakuna.

2. Zitakupa hali halisi ya mtaani. Unapokuwa kwenye masomo kuna mambo mengi sana huwa mnadanganyana mnapokuwa kama kundi, ila unaporudi mtaani mwenyewe kuna vitu unaviona vya tofauti kabisa na ulivyokuwa unajidanganya.

3. Zitakuonesha kila kitu kinawezekana. Mpaka sasa huenda unaamini njia pekee ya kufanikiwa kwenye maisha yako ni kupata kazi kwenye kitengo kizuri. Na kama ukikosa kazi hiyo maisha yako yatakuwa magumu. Kupitia makala hizi utaona mambo mengi yaliyofanywa na watanzania wenzako bila hata ya kuajiriwa.

Kama utakuwa na nia ya kweli ya kujifunza, utapata mengi sana ambayo yatakusaidia. Ila kama utadharau na kupita utakuja kuyakumbuka haya baada ya mwaka mmoja kupita ukiwa unazunguka na bahasha.

Kuhakikisha hukosi makala hizi jiunge na mtandao huu kwa kubonyeza maandishi haya na kuweka email yako. Pia waalike marafiki zako ili nao wapate mambo haya mazuri waweze kuboresha maisha yao.

Wakati tukisubiri kuanza kwa makala hizo nakusihi uendelee kutembelea AMKA MTANZANIA na usome makala zilizopo zitakuwaidia sana. Katika makala zote utakazosoma nakuomba usome na kurudia kusoma tena makala hizi mbili;

1. Kabla hujaanza kuzunguka na bahasha soma hapa.

2. Barua ya wazi kwa wahitimu ambao bado wanatafuta ajira.

Soma makala hizo mbili mara nyingi uwezavyo na utaanza kupata mwanga wa nini kinaendelea mtaani.

Ombi kwa wasomaji wengine wa AMKA MTANZANIA.

Natoa ombi kwa wasomaji wengine wa AMKA MTANZANIA kuwa sehemu ya makala hizi za ushauri. Naamini kila mmoja wetu amewahi kuhitimu masomo kwa ngazi fulani na alipoingia mtaani kuna changamoto alikutana nazo. Kutokana na changamoto ulizopitia kuna kitu unaweza kumshauri mtu anayeingia mtaani kutokea masomoni.

Nakuomba sana uandike vitu vichache ambavyo ungependa kumshauri mtanzania mwenzako ambaye anaingia mtaani avijue. Usihofu kama hujui kuandika, wewe andika kile unachoweza mimi nitafanya marekebisho ili kuwa na mpangilio mzuri. Tusaidiane sisi watanzania ili yuweze kuendelea sisi wenyewe na taifa letu kwa ujumla.

Nategemea kusikia chochote kutoka kwako, ukiandika unaweza kunitumia kwa email amakirita@gmail.com

Tusaidiane kupunguza yale yaliyotokea uwanja wa taifa kwa waombaji zaidi ya elfu kumi kuitwa kwenye usaili wa nafasi sabini. Waombaji jumla walikuwa zaidi ya elfu ishirini.

Tafadhali endelea kuwaalika marafiki zako kulike page yetu ya facebook. Bonyeza maandishi haya na kisha like halafu nenda sehemu ya invite friends kisha waalike nao walike ukurasa huu ili tuweze kuwafikia wengi zaidi. Naomba sana ushirikiano wako kwenye hili na utakuwa balozi mzuri wa kuwaamsha watanzania wenzetu. Asante sana kwa ushirikiano wako.

TUKO PAMOJA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: