Njia Tatu Zinazoweza Kukusaidia Ujiamini Zaidi.

Makala hii imeandikwa na  Mwakatika Geofrey

Unapojitazama kwenye kioo, unavutiwa na kile unachoona? Unaona kwamba una ustadi mbalimbali unaojivunia? Unaweza kusimama imara unaposongwa na vijana wenzako? Unakubali unapokosolewa kukiwa na msingi? Unaweza kustahimili wengine wanaposema mambo yanayoudhi juu yako? Unahisi kuwa unapendwa? , Wewe hutunza afya yako? Wewe hufurahi wengine wanapopata mafanikio?

Ikiwa umejibu hapana kwa baadhi ya maswali hapo juu, huenda unakosa kuona vipawa fulani ulivyo navyo kwa sababu ya kutojiamini. Makala hii imekusudiwa kukusaidia kutambua sifa hizo nzuri!    Vijana wengi wanahangaishwa sana na sura yao, uwezo wao, na pia vile vijana wenzao wanavyowaona. Je, unahisi hivyo pia? Ikiwa unahisi hivyo, basi hauko peke yako. “Kutokamilika kwangu hunifanya nishuke moyo. Kwa kawaida, adui yangu mkubwa ni mimi mwenyewe.”—julieth. “Hata uwe mrembo au mwenye sura ya kuvutia kadiri gani, bado utakutana na wengine ambao wana sura nzuri kuliko wewe.”—joyce.

Ikiwa wewe huhisi kama vijana waliotajwa hapo juu, usife moyo. Unaweza kupata msaada. Hizi hapa ni njia tatu zinazoweza kukusaidia ujiamini zaidi na pia uwe na maoni yanayofaa kujihusu.

1. Jitoe KuwasaidiaWengine.

Jambo la msingi “Kuna furaha zaidi katika kutoa kuliko ilivyo katika kupokea.” Maana yake. Unapowasaidia wengine, unafaidika pia. Jinsi gani? “Mtu mkarimu atafanikishwa,” yasema methali moja ya Biblia. Maneno hayo ni kweli kabisa— utakuwa na hali njema unapowasaidia wengine!  . Tahadhari: Usiwasaidie wengine kwa sababu tu wewe pia utafaidika. Ikiwa nia si nzuri, utaambulia patupu. Kwa kawaida watu huona unafiki!

2. Tafuta Marafiki

Andiko la msingi. “Rafiki wa kweli anapenda nyakati zote, naye ni ndugu aliyezaliwa kwa ajili ya wakati wa taabu.” Maana yake. Rafiki wa kweli anaweza kuwa utegemezo mkubwa wakati wa taabu. Hata kule kujua tu kwamba mtu fulani anakujali kunaweza kukutia moyo. Kwa hiyo, fanya urafiki na wale walio na uvutano mzuri kwako. Tahadhari:Hakikisha kwamba ushirika pamoja na marafiki wako hutokeza sifa zako ulizo nazo—bali si kujibadili uwe mtu bandia ili tu ukubalike machoni pao. Ukifanya mambo ya kipumbavu ili tu kuwapendeza wengine, mwishowe utajidharau na kuhisi kwamba umetumiwa vibaya.

3. Usife Moyo Unapofanya Makosa.

Upende, usipende, wewe si mkamilifu. Kwa hiyo, nyakati nyingine utasema au kutenda jambo lisilofaa. Ijapokuwa huwezi kuepuka kufanya makosa, unaweza kuamua jinsi unavyoyashughulikia. Tahadhari: Usitumie kutokamilika kwako kuwa kizingizio  cha kutenda kosa Kufanya jambo lisilofaa kimakusudi, kutakufanya upoteze kibali cha maana zaidi.

KUMBUKA KUJIAMINI NI MBINU MOJAWAPO YA WEWE KUFIKIA MAFANIKIO YAKO

Unaweza kusoma makala nzuri zaidi za Mwakatika Geofrey kwa kutembelea blog yake geofreymwakatika.blogspot.com bonyeza hiyo link kufungua.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: