USHAURI; Jinsi Ya Kukuza, Kustawisha Na Kuendeleza Biashara.

Moja ya changamoto kubwa kwenye biashara nyingi ni jinsi ya kuzikuza na kuendelea zaidi. Kuna biashara nyingi huku mitaani ziko vile vile miaka nenda miaka rudi. Pamoja na kuwepo hivyo hivyo kila mwaka bado wamiliki wa biashara hizi jawajapata mafanikio waliyotegemea kuyapata. Hili limekuwa tatizo kwa watu wengi sana na huenda ni tatizo ambalo limekusumbua wewe muda mrefu.

Kabla ya kuona ni jinsi gani unaweza kukuza, kustawisha na kuendeleza biashara yako naomba tuone alichoandika msomaji mwenzetu wa AMKA MTANZANIA.

Mimi ni mfugaji wa ng’ombe,mbuzi na kondoo pia nina duka la rejareja mwaka wa 3 sasa.Shida yangu ni namna ya kukuza ,kustawisha na kuendeleza biashara hii ya duka hadi kiwango cha kukidhi mahitaji ya wateja wote. Nimeplan mara nyingi kufikisha kiwango fulani cha mauzo mwisho nikifanya tathmini sijafikia ama nimeshuka kiwango.Naomba msaada ni mbinu zip nawezatumia kufikia lengo langu la kuikuza bishara.

Kama alivyosema msomaji mwenzetu hapo juu hii ni kiu ya wafanyabiashara wengi sana, jinsi ya kukuza biashara zetu.

Inawezekana unaweka mipango mizuri ila bado huoni matokeo mazuri. Kuna mambo mengi unaweza kufanya kukabili changamoto hii, hapa nitaeleza mambo manne ambayo unaweza kuanza kufanya na ukaona mabadiliko makubwa.

1. Weka malengo na mipango mizuri ya kufanikiwa.

Huu ndio mwanzo kabisa wa safari ya mafanikio katika jambo lolote unalofanya. Ila pia inawezekana umeshafanya hivi na bado umeshindwa kupata mafanikio. tatizo inakuwa nini?

Tatizo linaweza kuwa unaweka malengo yako vibaya au huweki mipango yako vizuri. Malengo na mipango unayoweka hakikisha inaeleza kwa kina kabisa ni kitu gani utafanya wakati gani na ni marekebisho gani unahitaji kufanya ili uweze kufanikiwa. Kusema tu labda baada ya miezi sita nataka nifikie mauzo ya milioni kumi haitoshi kukufikisha hapo. Ni lazima uchambue ni nini utabadili sasa ili uweze kufikia malengo hayo ya kuuza milioni kumi.

Kuna mambo mengi sana ya kurekebisha kwenye biashara hasa za reja reja ili kuweza kufikia mafanikio makubwa. Mambo kama jinsi unavyofanya biashara, muda unaofungua na kufunga, wafanyakazi unaoajiri, jinsi unavyochangamana na wateja na hata imani yako kwenye biashara yana nafasi kubwa sana kwenye mafanikio ya biashara yako. Hakikisha haya yamekaa vizuri kwanza kabla hujaona mafanikio makubwa kwenye biashara yako.

kitabu kava tangazo

2. Jua ni wapi unakosea na ufanye marekebisho haraka.

Kama unaweka malengo na mipango ila bado unashindwa kuifikia ni dhahiri kuna sehemu unakosea kwenye mipango yako au uteklezaji wa mipango yako. Na ili uweze kujua hilo ni lazima kila unaposhindwa kufikia lengo ujifanyie tathmini ya yote uliyofanya ili kujua ulikosea wapi. Sisi ni binadamu hivyo tunakosea mara nyingi sana, kitu kizuri ni kwamba tunapokosea ndipo tunapojifunza. Tumia makosa yako kama sehemu ya kujifunza ni njia ipi bora kwako kufikia malengo yako.

Sio kila mipango utakayokuwa nayo kwenye biashara yako itakuletea mafanikio. Jipime kila mara na jua ni mipango ipi inaleta mafanikio na ipi haileti mafanikio.

3. Kua wewe kwanza.

Moja ya sababu kubwa kwa nini biashara yako haikui ni kwa sababu wewe mwenyewe hukui. Biashara yako haiwezi kukua kama wewe mwenyewe hukui, sahau kabisa kuhusu hilo. Cha kushangaza asilimia kubwa ya watu wanataka biashara zao zikue wakati wao bado wako vile vile na wanafikiri vile vile, kitu ambacho hakiwezi kutokea. Wewe unakuaje? Unakua kwa kujifunza kuhusu biashara kupitia kujisomea vitabu, makala nzuri kama hizi, kuhudhuria mafunzo na hata semina mbalimbali. Kujua zaidi kuhusu wewe na biashara yako kukua soma; Hii ndio sababu kubwa kwa nini biashara yako haikui.

4. Epuka chuma ulete kwenye biashara yako.

Tatizo jingine kubwa kwenye mafanikio ya biashara zetu ni chuma ulete. Chuma ulete ameturudisha nyuma sana kwenye biashara zetu na wengine wamejikuta wakifunga biashara zao kabisa. Ubaya wa chuma ulete huenda mpaka sasa hujamjua vizuri na hivyo hutoweza kabisa kupambana naye. Nilishaandika kwa kirefu sana kuhusu chuma ulete na jinsi ya kupambana naye. Kusoma jinsi gani unaweza kuepuka chuma ulete bonyeza maandishi haya na kuielewa vizuri dhana ya chuma ulete na jinsi ya kujikomboa wewe na biashara yako jiunge na KISIMA CHA MAARIFA. Kupata maelezo zaidi jinsi ya kujiunga bonyeza hayo maadhishi.

Kukua na kustawi kwa biashara yako ni jambo ambalo linawezekana vizuri sana kama utajua ni wapi unataka kwenda na utafikaje pale. Anza kufanya mambo hayo manne na utaona mabadiliko makubwa sana kwenye biashara zako.

Kwa ushauri zaidi wa kivitendo wa namna ya kuiondoa biashara yako hatua moja mpaka nyingine tafadhali wasiliana na mimi kwa mawasiliano hayo hapo chini.

Nakutakia kila la kheri katika safari hii ya mafanikio.

Kumbuka TUKO PAMOJA. 

Kama una changamoto ambayo inakuzuia kufikia malengo yako unaweza kuitoa kwa kubonyeza maandishi haya na kujaza fomu. Changamoto yako inaweza kuwa moja makala zijazo kila siku ya jumatatu. Kama unahitaji ushauri wa haraka wasiliana na mimi kwa email amakirita@gmail.com au simu 0717396253/0755953887.

2 thoughts on “USHAURI; Jinsi Ya Kukuza, Kustawisha Na Kuendeleza Biashara.

Add yours

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: