KITABU; Chagua Kuwa Tajiri, Tabia Nane Za Mamilionea Wenye Furaha.

Msomaji wa AMKA MTANZANIA na mmiliki wa blog GEOFREY MWAKATIKA alinishirikisha kitabu ambacho nimekisoma na kuona ni kizuri sana. Wakati naendelea kukisoma kitabu hiki nilikuwa nasukumwa sana kuwashirikisha wasomaji wote kwa sababu mambo yaliyoandikwa kwenye kitabu hiki yatabadilisha maisha yako mara moja, kama ukiyaelewa na kuyafanyia kazi.

Kitabu hiki kinaitwa Choose to Be Wealthy, 8 Habits of the Happy Millionaire kilichoandikwa na Bo Sanchez.

BO

Bo ni mmishionari, mtu ambaye amejitolea maisha yake kufanya kazi ya kidini. Tofauti na mtazamo wa wengi ulivyo kwamba ukishakuwa mtumishi au kiongozi wa kidini basi huna haja ya kuwa na fedha nyingi, Bo ameelezea ni jinsi gani ameweza kufanya kazi yake ya umishionari vizuri na kuwafikia wengi kutokana na kuwa na fedha nyingi.

Hiki ni kitabu ambacho kama ukikisoma na kukitumia hutabaki kama ulivyo. Kwa sababu kitabu hiki imeanza na kubadili mtazamo wako kuhusu fedha na utajiri, kinakupeleka taratibu kuanzia kwenye kuweka misingi ya kuingeza kipato chako, kukitunza na kuwekeza zaidi.

Pia kimetumia mifano mbalimbali kuonesha jinsi ambavyo watu wamefanikiwa kwa kuwa na misingi hii.

Moja ya mafundisho niliyofurahia sana kwenye kitabu hiki ni kuwa na mashine/mfumo wa kutengeneza fedha na sio kuwa na fedha pekee. Katika fundisho hili ametumia mfano wa kuku wa dhahabu na yai la dhahabu kueleza jinsi ambavyo wafanyakazi wengi wanaishia kuwa watumwa wa fedha. Soma na ukifika sehemu hii soma kuelewa zaidi. Nitakuja kuandikia hili siku nyingine ila kama utakuwa umesoma ndio utaelewa vizuri.

Nakusihi sana sana usome kitabu hiki, hata kama kuna kitabu kingine nimekutumia bado hujamaliza kusoma naomba ukiweke pembeni kwa muda na soma hiki kwanza. Ni kitabu kifupi sana na kimepangiliwa kwa mfumo ambao hauchoshi kusoma.

Ukikaa kukisoma haitakuchukua muda mrefu na utafurahua kukisoma kutokana na mpangilio wake na ujumbe unaoupata.

Kupata kitabu hiki bonyeza maandishi haya ya kitabu Choose to Be Wealthy, 8 Habits of the Happy Millionaire kilichoandikwa na Bo Sanchez na utaanza kukidownload.

Nakusihi sana uendelee kujifunza na kuyatumia yale unayojifunza kwenye maisha yako. Kama ukifanya hivi utaona mabadiliko makubw akwenye maisha yako.

Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kufikia mafanikio na uhuru wa kifedha.

TUKO PAMOJA.

3 thoughts on “KITABU; Chagua Kuwa Tajiri, Tabia Nane Za Mamilionea Wenye Furaha.

 1. AYMAN MAHAMBA July 5, 2014 / 5:28 am

  Hakika wewe ni muwazi na mkweli pia hauna choyo.
  Mafundisho yako ni sahihi na ni ya manufaa sana- Ahsante sana.

  Like

 2. Makirita Amani July 5, 2014 / 5:20 pm

  Asante sana, washirikishe na wengine pia ili nao wapate mambo haya mazuri.

  Like

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s