Acha Chochote Unachofanya na Usome Hapa Kwa Dakika Mbili Tu.

Habari za leo mpenzi msomaji wa AMKA MTANZANIA naamini unaendelea vizuri na harakati zako za kuboresha maisha yako kila siku. Pia najua unapitia magumu mengi mpaka unaona ndoto kubwa unazotarajia haziwezi kufikiwa.

Leo naomba uchukue dakika zako tano tu, mbili kusoma hapa na tatu kufanya maamuzi ya maisha yako. Najua muda wako ni mdogo sana na hivyo dakika tano kwako zinaweza kuwa nyingi sana. Ila nakusihi sana utumie dakika hizo tano tu na ubadili maisha yako.

maisha1

Naomba ukae chini na kujiuliza maswali yafuatayo kuhusu maisha yako;

1. Je utaendelea na maisha hayo mpaka lini? Maisha ya kulalamika, maisha ya kukimbiza fedha, maisha ya kuishi kwa ugumu yatakwenda mpaka lini?

2. Je utaendelea kufanya kazi au biashara usiyoipenda mpaka lini. Hupendi kabisa kazi unayoifanya, kazi ni ngumu malipo ni kidogo kila siku inapoanza unatamani iwe imeisha.(soma; kama unataka kufanikiwa usifanye kazi.)

3. Je utaendelea kuishi maisha ya udalali mpaka lini? Maisha ambayo unapata fedha kwenda kulipa madeni na baada ya kulipa madeni unabaki bila fedha unaanza tena kukopa. Hebu fikiri kwa kina maisha haya utaenda nayo mpaka lini?(soma; hivi ndivyo unavyofanya udalali wa maisha yako.)

Fikiria maswali hayo na leo hii fanya maamuzi ambayo miaka michache ijayo maisha yako yatabadilika sana.

Maisha ni mafupi sana kuendelea kuishi kwa mateso au kwa maigizo. Unaweza kuishi maisha yale unayotaka wewe kama tu ukiamua kuishi hivyo.

Sehemu kubwa ya maisha yako inatokana na kuiga wengine wanafanya nini. Unanunua vitu vinavyokuingiza kwenye madeni kwa sababu wengine nao wananunua au unataka uonekane. Unafanya kazi ya ajira kwa sababu ndio heshima kwenye jamii inayokuzunguka. Unafanya biashara kwa sababu kuna watu wengine wanafanya biashara hapo ulipo.

Haya yote yamekufikisha hapo ulipo na unaona hakuna kingine kinachowezekana zaidi tu ya kusukuma siku.

Leo nataka uache kuishi maisha hayo ya mazoea, nataka utengeneze maisha yako mwenyewe na sio kuishi yale ambayo yametengenezwa na wengine.

Hilo linawezekana kama utaamua kufanya hivyo.

Chukua maamuzi sasa, kama kuna kitu chochote ambacho hukipendi kwenye maisha yako unaweza kukibadili sasa. Sehemu nzuri ya kujifunza mabadiliko haya kwa kina ni kwenye KISIMA CHA MAARIFA bonyeza maandishi hayo na upate maelekezo ya kujiunga ili uweze kuboresha maisha yako.

Nakutakia kila la kheri katika harakati za kuboresha maisha yako.

TUKO PAMOJA.

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out / Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out / Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out / Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out / Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: