Tumia Muda Huu Mchache Kufanya Mabadiliko Makubwa Na Endelevu Katika Maisha Yako.


Kuwa na mafanikio ni jambo ambalo kila mtu analihitaji katika maisha yake kila siku. Kutokana na umuhimu wa mafanikio, binadamu hujikuta anafanya kila linalowezekana ili kutimiza malengo na ndoto zake alizojiwekea. Na kufanya mabadiliko katika maisha yako ni kitu ambacho kinawezekana  sana endapo wewe mwenyewe utaamua kubadilika kwanza na kufanya vitu muhimu vitakavyokufikisha katika kilele cha mafanikio.
Mara nyingi ikumbukwe kuwa ili tuwe na mafanikio makubwa tunalazimika kabadili tabia zetu za ndani zilizotukwamisha na kutufikisha hapa tulipo kwa muda mrefu.  Tatizo walilonalo watu wengi ni kutojua nini cha kufanya kuweza kubadili tabia hizi mbaya na pengine kwa muda mfupi. Ni muhimu sana kubadili  tabia zinazokurudisha nyuma na kujenga tabia za mafanikio ya kudumu katika maisha yako.
Kwa vyovyote vile iwavyo unatakiwa kubadili tabia zako kwa kiasi kikubwa ili kufanya mabadiliko makubwa ya maisha yako. Unaweza kujiuliza ni muda kiasi gani unahitajika wewe ili kuweza kujenga tabia za kudumu za mafanikio? Kwa kawaida inamchukua binadamu muda wa siku 30 kujenga tabia za mafanikio ndani yake na kufanya mapinduzi makubwa ya maisha yake. Huu ni muda mchache sana lakini utakuletea mabadiliko makubwa kama utautumia vizuri.
Kama unataka kujenga tabia bora za mafanikio zitakazo kuongoza siku zote za maisha yako makala hii ni muhimu sana kwako kuifatilia. Katika makala hii leo,  tutajadili ni kwa jinsi gani na ufanye vitu gani angalau kwa mwezi mmoja ili kujenga tabia za kudumu za  mafanikio. Ni kwa vipi sasa utatumia muda huu mchache wa siku 30 na kufanya mabadiliko makubwa katika maisha yako.
Hivi ndivyo unavyoweza kutumia muda huu mchache wa siku wa siku 30 kufanya mabadiliko makubwa katika maisha yako:-
1.     Jifunze kufanya vitu vipya kila siku.
Katika kipindi cha siku 30 jifunze vitu vipya kila siku. Tumia angalau dakika thelathini kujisomea, hii itakusaidia wewe kujifunza vitu vingi sana vipya vitakavyokuwa msaada mkubwa katika maisha yako ya leo na baadae.Ukifanikiwa kumaliza siku thelathini kujisomea kila siku utakuwa umejenga tabia bora itakayokusaidia kufikia  malengo makubwa uliyojiwekea.
 
2.     Tenga muda mchache wa kutafakari juu ya maisha yako.
Ukitaka kuwa na mafanikio makubwa katika maisha yako hakikisha unatenga muda mchache kwa siku wa kutafakari juu ya maisha yako. Unaweza ukatumia dakika kumi tu kutafakari wapi unatoka, wapi unakwenda, na wapi ulipokwama.
Hii itakusaidaia kuona udhaifu wako na kubadili mwelekeo pale unapoona unakwama.Ukijifunza kutumia muda mchache kwa siku ndani ya siku 30,  baada ya muda mfupi nakupa uhakika utakuwa mbali sana katika maisha yako.

3.     Jifunze kufanyia kazi malengo yako uliyojiwekea kila siku.

Katika muda huu mfupi wa siku 30 hata kama una malengo mengi vipi jifunze kufanyia kazi malengo yako kila siku. Utafanikisha hili endapo tu utaweza kuyagawa malengo yako sehemu kwa sehemu. Unapozidi kufanya kidogokidogo katika malengo yako mwisho utajikuta unamaliza na kufanikisha ndoto zako.

4.     Jifunze kuwa chanya.

Hiki ni kipindi cha kujifunza  kuwa chanya. Achana na mawazo hasi ambayo umekuwa nayo muda mrefu. Chochote unachotoa katika maisha ndicho unachokipata. Ukitoa na kuwaza mawazo chanya uwe na uhakika utapata mawazo chanya zaidi. Na unapokuwa na mawazo chanya hii itakusaidiasana kufikia ndoto na malengo yako kwa urahisi zaidi.
Ukiweza kuwa chanya ndani ya mwezi mmoja utakuwa umejenga na umebadili maisha yako kwa sehemu kubwa sana. Kuwa mtulivu na tuliza fikra zako kwa mwezi huu uone matokeo makubwa. 
5.     Punguza muda wa kuangalia TV.
Ukiweza kupunguza muda wa kuangalia Tv na angalau ukawa unaangalia kwa dakika thelathini tu kwa siku basi utakuwa umefanya mabadiliko makubwa sana katika maisha yako. Katika kipindi hiki cha mwezi mmoja utakuwa umeokoa muda mwingi sana ambao utautumia kufanyia mambo mengine katika maisha yako.
Watu wengi sana wanajikuta wanapoteza muda wao mwingi katika Tv na hii imekuwa kama ugonjwa fulani hivi. Kama Tv inakupotezea muda achana nayo wa muda huu wa mwezi mmoja, mwisho utazoea na itakuwa ndio tabia yako. 
6.     Amka asubuhi na mapema kila siku.
Katika kipindi cha mwezi mmoja, tenga muda wa kuamka kila siku mapema. Unaweza ukajiwekea utaratibu wa kuamka saa kumi na moja kamili. Na unapoamka huu kwako ndio unakuwa muda mzuri wa kutafakari namna utakavyoweza kupangilia siku. Pia unaweza ukaamua kujifunza kidogo kwa kujisomea vitabu au kutembelea blog nzuri kama hii ya AMKA MTANZANIAinayohamasisha mambo mazuri ya mafanikio.
( Unaweza kusoma pia hili ndilo saa moja ya maajabu maishani mwako)  
7.     Futa tabia mbaya usizopenda.
Je, wewe ni mwongeaji sana bila vitendo? Unaangalia sana Tv? Au wewe ni mlalamikaji sana? Lakini vyovyote vile iwavyo ndani ya mwezi huu mmoja hakikisha unafanya mabadiliko juu ya maisha yako  na kufuta tabia zote usizozipenda na ambazo zimekufisha hapo ulipo. Ukiweza kufuta tabia hizi mbaya ambazo umekuwa nazo kwa muda sasa utaona mabadiliko makubwa katika maisha yako.  
8.     Jifunze kuyafurahia maisha.
Yafurahie maisha kwa uzuri wake. Jenga tabasamu kila siku hii itakusaidia sana kuwa mtu wa watu na pia utaweza kujenga nguvu nyingi chanya ambazo zitakusaidia kukufanikisha katika safari ya mafanikio.
Weka katika vitendo na ubadili maisha yako. Utakavyomudu kufanya vitu hivi katika kipindi cha siku 30 utakuwa umeweza kufanya mabadiliko makubwa sana katika maisha yako  kwa sababu utajifunza kujenga tabia muhimu za mafanikio utakazo zitumia katika maisha yako yote.
Nakutakia kila la kheri katika safari ya ukombozi wa maisha yako iwe ya ushindi zaidi.
DAIMA TUPO PAMOJA!
IMANI NGWANGWALU– 0767048035/ingwangwalu@gmail.com  

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google photo

You are commenting using your Google account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

Create a website or blog at WordPress.com

Up ↑

%d bloggers like this: