Mpendwa msomaji wa AMKA MTANZANIA ninayo furaha kukujulisha kwamba sasa unaweza kusoma makala mbalimbali kwenye AMKA MTANZANIA kwenye simu yako ya smartphone au tablet yako kwa urahisi zaidi.

Kuna application moja inaitwa NewsHome, ambayo inakuwezesha kusoma blogs na website mbalimbali zinazotoa habari. Kupitia application hii unaweza kupata makala mpya za amka mtanzania moja kwa moja kwenye simu yako kila inapowekwa.

newshome (1)

Kupata application hii fuata hatua hizi;

1. Nenda kwenye PLAY STORE ambapo huwa unapata application mbalimbali.

2. Nenda kwenye search kisha weka jina NewsHome. Utaletewa application, imeandikwa NewsHome App, ina kialama cha nyumba na background orange.

3. Download na kisha install application hiyo.

4. Baada ya kuinstall ifungue(open) na itakuletea ukurasa wenye vyanzo kadhaa vya habari.

5. Chagua vyanzo viwili vya kuanzia(unaweza kuviondoa baadae), kisha endelea kwa kubonyeza DONE.

6. Baada ya kufungua na kuanza kutumia nenda kwenye options kulingana na simu yako na bonyeza ADD SOURCES utaletewa vyanzo vingine na hapo utaweza kuichagua AMKA MTANZANIA. Pia unaweza kuondoa zile ulizochagua mwanzo kama huzipendelei.

newshome (2)

Fanya hivi na mwambie na mwenzako pia ili tuweze kupata makala na habari kwa urahisi zaidi na pia tuweze kukuza kazi zilizofanywa na watanzania wenzetu.

Uzuri ni kwamba kazi hii imefanywa na mtanzania mwenzetu ambaye ni mjasiriamali wa mambo ya teknolojia ya habari na mawasiliano. Tumuunge mkono na pia tufaidike.

Nakutakia kila la kheri,

TUKO PAMOJA.