Tanzania ni moja ya nchi ambazo watu wengi sana wanaamini katika uchawi. Watu wengi wanaamini katika imani za kishirikina ili kuweza kupata mafanikio kwenye kazi, biashara na hata maisha kwa ujumla. Zaidi ya asilimia tisini ya watanzania wanaamini katika imani za kishirikina. Yaani kuna wale ambao wanazitumia kufanikisha mambo yao na kuna wengi ambao hawazitumii ila wanaamini kuna wanaozitumia kufanikisha mambo yao.
Hakuna haja ya kudhibitisha sana hili kwa sababu tumeshuhudiia mauaji ya vikongwe, na pia tumeshuhudia sana mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi au albino. Tumekuwa kila siku tukiona watu wanahubiri kuhusu freemason na habari nyingine za kichawi na pia tumeona watu wakishuhudia kwamba walikuwa wanafanya mambo haya ya kichawi na hivyo kuua watu au kufanya mambo mengine ya hatari ili kufikia mafanikio.
UCHAWI
Swali ni je imani hizi ni za kweli? Je ni kweli watu wanafikia mafanikio makubwa kupitia imani hizi za kishirikina?
Haya ni maswali ambayo nitayajibu kwenye makala zitakazokujia hapa AMKA MTANZANIA kila jumatano kwa mwezi huu wa tisa.
Sitaki nikupe jibu rahisi tu kwamba uchawi haupo au uchawi hauna nguvu kama ambavyo mmekuwa mkipata majibu haya rahisi. Mimi nitakwenda taratibu na kuingia ndani kidogo kuona ni jinsi gani imani hizi zinaweza kuwa na nguvu au zisiwe na nguvu.
Pia nitakupatia njia nzuri ya wewe kuweza kufikia mafanikio makubwa bila hata ya kutumia uchawi.
Katika mijadala hii nitakayoleta hapa nitatumia uelewa na uzoefu wa kawaida na pia nitatumia sayansi ya tabia(behavioural science) na saikolojia ya bonadamu(human psychology) kuona ni jinsi gani yale yanayozungumzwa na kufanywa ni ya kweli au ya uongo.
Karibu kwenye mijadala hii ambayo itakupatia mwanga mkubwa sana na kuweza kuingia kwenye mawazo yako na kufungua milango ya mafanikio bila ya kuvaa hirizi au kuaminishwa vitu visivyo vya kweli.
Kwa wiki nne tutajifunza yote yanayohusiana na mafanikio na uchawi na mwisho tutaondoka na fomula ambayo tutaweza kuitumia kufikia mafanikio makubwa.
Kuhakikisha hukosi mambo haya mazuri endelea kutembelea AMKA MTANZANIA na pia jiunge na mtandao huu kwa kubonyeza maandishi haya na kuweka email yako.
Nakutakia kila la kheri katika safari yako ya kufikia mafanikio makubwa.
TUKO PAMOJA.
KWA-NINI-SIO-TAJIRI